SHIRIKA LA UMEME TANZANIA
KATIZO LA UMEME –
MKOA WA KINONDONI KASKAZINI
Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) linawataarifu
wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme
kama ifuatavyo.
MUDA: 3:00
asubuhi hadi 10:00 jioni
TAREHE: 8 Februari, 2016 (JUMATATU)
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya BB5,
kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti hali
ya kukatika kwa umeme mara kwa mara,
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Kunduchi
yote, baadhi ya maeneo ya Salasala, Kilongawima na Mbezi beach, Recruitment
Training School (RTS) of TPDF, Mbuyuni, MECCO, JKT machimbo, Tegeta darajani,
Benaco, shule ya Green Acres, Majumba sita, Kinzudi pamoja na maeneo yanayozunguka.
TAREHE: 9 Februari, 2016 (JUMANNE)
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya MK
6, kwa ajili ya kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kudhibiti
hali ya kukatika kwa umeme mara kwa mara,
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Baadhi ya
maeneo ya barabara ya Mwaya na Chole, mtaa wa Uganda, kota za bandari na UNDP,
flati za NASAKO na IFM, Valahala na Baobao Village, hosteli za chuo cha Muhimbili,
Kipepeo apartments, Sea cliff court, hoteli ya Alexander pamoja na maeneo
yanayozunguka.
Tafadhali
usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba
za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 022
2701602, 0784 768584, 0716 768584 au namba za kituo cha miito ya simu 2194400
na 0768 985100
Uongozi unasikitika kwa
usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na:- OFISI
YA UHUSIANO,
TANESCO
– MAKAO MAKUU.
Huku kimara kuja mbezi, hili tatizo la umeme limekuwa sugu week ya pili saivi. Tatizo lipo wapi? Na lini mambo yatakaa sawa.
ReplyDelete