Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawatarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini
kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.
TAREHE: 19 Septemba, 2016. (JUMATATU)
MUDA: 3:00
Asubuhi 10:00 Jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya MAKUMBUSHO (MAK 4), kwa ajili ya
kuhamisha laini ya msongo 11KV na kupisha ujenzi wa laini mpya ya msongo 33KV
wa kituo kipya cha kupooza umeme cha Mwananyamala
ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
MAENEO
YATAKAYOATHIRIKA:
Baadhi ya maeneo ya Mwananyamala, Makumbusho, Dawasa limited, ABB Office, Mwananyamala hospital pamoja na maeneo ya jirani.
1.LAINI YA TEGETA (TG3)
TAREHE: 20 Septemba, 2016 (JUMANNE)
MUDA: 3:00
Asubuhi hadi 10:00 Jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya TEGETA(TG3) kwa ajili ya
matengenezo yatakayoambatana na ukataji miti inayogusa laini za umeme na
kubadilisha nyaya zilizochakaa ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
MAENEO
YATAKAYOATHIRIKA:
Maeneo
yote ya Bunju, Madale, Mivumoni na Mabwepande, baadhi ya maeneo ya Bagamoyo,
Wazo Kisanga, Mbweni mpiji, Tegeta maeneo ya Kibo complex pamoja na maeneo ya
jirani.
2. LAINI YA WAZO 2.
TAREHE: 20 Septemba, 2016. (JUMANNE)
MUDA: 3:00
asubuhi hadi 10:00 jioni
SABABU: Kuzimwa kwa laini ya WAZO 2, kwa ajili ya kubadili
nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
MAENEO
YATAKAYOATHIRIKA
Maeneo yote
ya Goba, baadhi ya maeneo ya
Mbezi juu na Salasala pamoja na maeneo ya
jirani.
Tafadhali usishike waya uliokatika, toa
taarifa kupitia namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni
Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au namba za kituo cha miito ya simu 2194400
na 0768 985100.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na:- OFISI
YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO MAKUU.
No comments:
Post a Comment