Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, akitoa taarifa za athari hizo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba na ujumbe wake
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba na ujumbe wake, mara baada ya mazungumzo yao, Septemba 17, 2016
Meja Jenerali Kijuu, akiagana na Mhandisi Mramba na ujumbe wake
Fundi wa TANESCO mkoani Kagera, akiondoa nyaya za umeme baada ya kukata umeme kwenye nyumba moja eneo la Hamugembe, ikiwa ni hatua ya kuchukua tahadhari
Mhandisi Mramba, akitembelea maeneo yaliyoathirika na tetemeko hilo huko Hamugembe
Mhandisi Mramba, akiongea na waanishi wa habari kwenye eneo moja lililoathirika vibaya na tetemeko la ardhi huko Hamugembe
Bi Slivia Philip, akiwa ameketi nje ya nyumba yake iliyoharibiwa vibaya na tetemeko eneo la Hamugembe-Mkishenyi mkoani Kagera, Septemba 17, 2016
Violet Anaclet, mkazi wa Hamugembe-Mkishenyi, akiwa na mawazo wakati akijipumzika kwenye eneo la wazi baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuharibiwa na tetemeko, Septemba 17, 2016
Mhandisi Mramba, akisalimiana na Afisa Mtendaji wa Kata ya Hamugembe, Sudi Ahmada, Septemba 17, 2016
Kaimu Meneja wa TANESCO Kanda ya Ziwa, Mhandisi Kalisa, (kulia), akizungumza na fomeni wa genge la TANESCO Kanda ya Ziwa, Freddy Lusama, wakati Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Mramba alipowatembelea wafanyakazi wa Shirika hilo waliokuwa wakiendelea na kazi kwenye eneo la Hamugembe mkoani Kagera, Septemba 17, 2016
Meneja wa TANESCO mkoani Kagera, Mhandisi Francis Maze, (katikati), akiwa amezungukwa na wafanyakazi wa shirika hilo akiwapa maelekezo, Septemba 17, 2016
Mhandisi Mramba, alipofika eneo la Hamugembe, kuona jinsi wafanyakazi wa Shirika hilo wakiendelea na kazi
Kwa bahati nzuri hakuna nguzo za umeme zilizoathirika na tetemeko hilo, hata hivyo TANESCO imeamua kuchukua tahadhari kwa kukagua ili kuona kama kuna nguzo yoyote iliyoathirika na kuchukua hatua za kubadilisha, kama ambavyo lori hili lililoonekana maeneo ya Hamugembe likiwa na nguzo hizo
Genizora Magili, anayehusika na masuala ya nyaya za umeme, akiwa amebeba vifaa vya kazi
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la
Umeme Tanzania, 9TANESCO), Leila Muhaji, akitoa ufafanuzi kuhusu masuala
mbalimbali ya kiusalama ambayo wananchi wanapaswa kuzingatia pindi
waonapo nyaya zilizoanguka au kutilia shaka yoyote kuhusiana na
miundombinu ya Shirika
Na Henry Kilasila
Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Mhandisi Felchesmi
Mramba amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu, Ofisini
kwake.
Awali Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali (mstaafu), Salum Kijuu,
Akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji na ujumbe wake alielezea athari, uharibifu na
maafa yaliyosababishwa na tetemeko lililotokea Jumamosi ya Septemba 10, 2016.
“Nawapongeza TANESCO pamoja na tetemeko hili
miundombinu yao haikuleta athari kwa wananchi, hakuna vifo vilivyotokana na
umeme”
Aliongeza Mkoa umekuwa ukipokea misaada kutoka Ofisi
ya Waziri Mkuu na wadau mbalimbali kama madawa, vyakula, vifaa vya ujenzi
maturubai.
“Tetemeko hili lilianzia sehemu za Misenyi na limesababisha
uharibifu wa majengo takribani 200, vifo 17, majeruhi 253 kati ya hao wamebaki
majeruhi 43 huku 23 kati ya 43 wakihitaji huduma ya upasuaji”. Alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi
Felchesmi Mramba kwa niaba ya TANESCO alimhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Kagera
kwamba hakuna madhara yoyote kwenye miundombinu ya umeme na ipo salama.
Eidha TANESCO imeshiriki kikamilifu kupitia Ofisi ya
msajili wa Hazina, pia wafanyakazi wanajikusanya mmoja mmoja ili kuweza
kuchangia.
“Tumetoa maagizo kwa mafundi wetu kufanya kazi masaa
ishirini na nne, pia tumeongeza nguvu kutoka Mikoa ya Mwanza, Geita na Mara
pamoja na Wilaya za jirani ambazo hazikupata madhara”. Alisema Mhandisi Mramba
Mhandisi
Mramba alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa upatikanaji wa umeme Mkoani Kagera utakuwepo
bila shaka yoyote isipokuwa tu kwenye maeneo ambayo nyumba zimeathirika vibaya
ili kuepusha athari zozote zinazoweza kutokea kutokana na kuguswa kwa nyaya za
umeme.
No comments:
Post a Comment