Fundi wa TANESCO, akifunga kikombe wakati wa kazi ya kubadilisha miundombinu ya kusafirisha umeme kwenye kituo kikuu cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo, jijini Dar es Salaam |
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji, akizungumza na waandishi wa habari kwenye eneo la mradi |
Kazi inaendelea |
Fundi wa TANESCO akiwa kazini |
Raphael Mjata, Msimamizi Mkuu wa Njia Kuu za Umeme, akionyesha uwezo wa kituo cha Ubungo cha kupooza umeme wenye kilovolti 132
Tamai Masayuki, Mwakilishi wa kampuni ya Kijapani ya Yachiyo Engineering Co. Limited, akizungumza na waandishi wa habari kuhsuu maendeleo ya uboreshaji huo |
Wahandisi wakijadiliana jambo
Mafunzi wa TANESCO na kampuni ya National Construction Company Limited, wakivuta nyaya hizo mpya |
Mafundi wa TANESCO, wakitayarisha nyaya hizo mpya
Mhandishi Bayona, akielezea waandishi wa habari mwenendo wa kazi hiyo |
Tsutomu Sato, wa kampuni ya Takaoka ya Japan, akiwa kazini
Meneja Mwandamizi wa Usambazaji Umeme wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), ambaye pia ndiye Meneja wa Mradi wa kuimarisha miundombinu ya Umeme, Injinia Theodory Bayona.(katikati), Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Leila Muhaji, (kulia) na Afisa Habari wa Shirika hilo makao makuu, Henry Kilasila, (wakwanza kushoto) na waandishi wa habari, wakitembelea eneo la mradi mapema leo asubuhi Septemba 3, 2016 ambapo kazi ilianza kwa kasi
Wafanyakazi wa TANESCO chumba cha ufuatiliaji mwenendo wa umeme (control room) wakiwa akzini
Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO makao makuu, Leila Muhaji, na Afia Uhusiano wa Shirika hilo, Henry Kilasila, wakiwa kazini
Mhandisi Bayona (kulia), akijadiliana jambo na Wahandisi wenzake, Yasutaka Osawa, (kushoto), ambaye ni mwakilishi katika mradi wa kuboresha umeme jiji la Dar es Salaam, kutoka kampuni ya Takaoka Engineering Co Ltd, na Mhandisi Ahmed Mmingwa, ambaye ni Msimamizi wa Mradi kutoka TANESCO
Chumba cha kufutialia mwenendo wa umeme jijini Dar es Salaam, (Control room), cha TANESCO-Ubungo sub station)
Na Henry Kilasila
WAHANDISI,
na mafundi wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), kwa kushirikia na
wale wa kampuni ya Kijapani ya Yachiyo Engineering Co Limited, wameanza kazi ya
uboreshaji miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza
umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam, Septemba 3, 2016.
Kazi
kubwa inayofanyika hivi sasa ni kubadilisha laini kutoka umeme mdogo kwenda
umeme mkubwa, lakini pia kubadilisha vifaa vingine muhimu ili kuwezesha
usafirishaji umeme uweze kuwafikia watumiaji katika ubora ulio juu.
“Ikumbukwe
kwamba, hapa tulikuwa na laini mbili (waya mbili) zilizokuwa na uwezo wa
kusafirisha umeme kiasi cha Megawati 120 kila moja, kutoka hapa Ubungo kwenda
kituo cha Ilala, lakini kazi inayofanyika sasa, ni kubadili njia hizo (waya za
umeme), ambazo zitakuwa na uwezo wa kupitisha kiasi cha umeme wenye Megawati 220 kila moja,” Alifafanua Meneja Mwandamizi
wa Usambazaji Umeme wa Shirika hilo, ambaye pia ndiye Meneja wa wa Mradi wa
kuimarisha miundombinu ya Umeme, Mhandisi Theodory Bayona.
Kwa
mantiki hiyo, kazi inayofanyika leo hii itawezesha umeme utakaokuwa
ukisafirishwa kutoka hapa Ubungo kwenda Ilala, kuwa na jumla ya Megawati 440
kwa laini zote mbili, tofauti na hapo awali ambapo uwezo wa kusafirisha umeme
ulikuwa Megawati 240 tu,” Alisema.
Kazi
ikikamilika wakazi wa jiji la Dar es Salaam, watakuwa wakipata umeme wa uhakika,
na ulio bora, alifafanua Injinia Bayona
Naye
Kaimu Meneja Uhusiano wa Shirika la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), Leila Muhaji,
amewaomba wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambapo Shirika linafanya
juhudi kubwa za kuwapatia umeme wa uhakika wananchi kwa kuimarisha miundombinu
yake,.
“Ili
kuwawezesha mafundi wetu kufanya kazi katika mazingira salama, tutakuwa
tukikata umeme kuanzia leo hii Septemba 3 na
umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa
utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba
17-18, na Septemba 24-25, 2016.” Alifafanua Leila, na kuwaomba wananchi kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki.
Mradi huu ulioanza Februari 2015 na unaotarajiwa kukamilika
Juni 2017 unatekelezwa na Serikali kupitia TANESCO kwa ufadhili wa Shirika la
Maendeleo la Japan (JICA) .
No comments:
Post a Comment