Picha
ya pamoja ya watumishi wa TANESCO ,
Waalimu pamoja na baadhi ya wanafunzi wa
Kirando Sekondari.
|
Mkoa wa Rukwa ni
miongoni mwa Mikoa ambayo kwa kiasi kikubwa itanufaika na upatikananaji wa
umeme wa uhakika kupitia mradi wa
usambazaji umeme vijijini REA,
Katika awamu ya pili
ya mradi huu ambao unakaribia kumalizika
mwishoni mwa mwezi huu( August 2016)
jumla ya vijiji 74 vitanufaika
ambapo zaidi ya kaya 16,422 zitaunganishiwa umeme,
Naye Afisa uhusiano Bi Grace Kisyombe akizungumza na wananchi katika mikutano hiyo
alisema Hii ni fursa pekee ambayo Serikali imetoa kwa kuifadhili miradi ya
umeme vijijini ili wananchi wapate huduma ya umeme ambayo ni muhimu kwa
maendeleo yao, hasa ikizingatiwa kuwa Tanzania inaelekea kuwa na uchumi wa
viwanda , ni vema kila mwananchi katika kaya awe na huduma ya umeme ambayo
itamuwezesha mwananchi mmoja mmoja au vikundi kuanzisha viwanda vidogo ambayo
vitawawezesha kujipatia kipato , pia alisisitiza kuwa gharama za kuunganishiwa
umeme katika miradi hii ya umeme vijijini ni nafuu sana , kwani mteja ambaye atahitaji kuunganishiwa umeme wa
njia tatu (three phase ) atalipia
shilingi 139,120/= tofauti na wakati
ambapo miradi hiyo itakuwa imekamilika na kukabidhiwa kwa TANESCO , ambapo
taratibu za malipo za shirika zitatumika ambapo itampasa mteja huyo kulipa
gharama ya zaidi ya shilingi laki tisa kupata umeme huo wa njia tatu. Na kwa
wateja watakao taka kuunganishiwa umeme kwaajili ya matumizi ya kawaida ya
majumbani wao katika kipindi cha mradi watatakiwa kulipia
kodi ya ngezeko la thamani ( VAT ) ambayo ni sawa na sahilingi 27,000/= pekee.
No comments:
Post a Comment