Pages

November 5, 2017

Naibu Waziri Nishati afanya ziara Mradi wa umeme Chamazi-Dovya kwa Mzala1-3, Mbande kwa Masista, Chamazi Vigoa.



Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu (Pichani) leo jumapili Novemba 5, 2017 anafanya ziara pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka na Viongozi wa TANESCO kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Mhe. Mgalu anatembelea Mradi wa umeme Chamazi-Dovya kwa Mzala1-3, Mbande kwa Masista, Chamazi Vigoa.

Mradi ambao unatekelezwa na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO), upo katika eneo la Mbagala na unatarajiwa kusambaza umeme kwa Wananchi wote wa Chamazi Dovya ambao hawajapata umeme.

 Mradi umekamilika katika mchanganuo ufuatao, Chamazi Dovya -miradi 3 Mbande kwa masista - miradi 4 jumla miradi 7 huku kila mradi ukiwa na transfoma 2 kila mmoja.


No comments:

Post a Comment