Leo Novemba 14, 2017 Wafanyakazi wa TANESCO Makao Makuu wakiongozwa na
Meneja Mwandamizi kanda ya Dar es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende
Mugaya kwa Niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito Mwinuka
wamekabidhi hundi ya Shilingi Milioni kumi Taslimu kama mchango wa
kugharamia matibabu ya watoto 5 wenye matatizo ya moyo katika Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete.
Mbali ya mchango huo wa Shirika wafanyakazi walichangia vifaa mbali
mbali vya watoto kujikimu kama sabuni, maji ya kunywa, pampers n.k
Msaada huo ulikabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Profesa Mohammed Janab
No comments:
Post a Comment