Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu Februari 22, 2018
amewasha Kituo cha kupokea na kupoza
umeme cha Mbagala chenye uwezo wa 50 MVA na hivyo kuimarisha upatikanaji wa
umeme katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar s Salaam, Mhe. Mgalu alisema kuwashwa
kwa Kituo hicho kutaondoa changamoto ya
umeme iliyokuwa ikiyakabali maeneo ya Mbagala, Kigamboni, Mkuranga, Tandika na
Kurasini, Maeneo hayo yatapata umeme wa uhakika.
Aliongeza kituo cha Mbagala kilikuwa kimezidiwa kutokana na
mahitaji makubwa ya umeme katika maeneo hayo, kutokana na mitambo kuwa chakavu.
“Niwashukuru Bodi ya TANESCO kwa kusimamia hili vizuri,
Menejimenti pamoja na Watendaji wa TANESCO kwa kazi kubwa wanayoifanya ya
kuboresha miundombinu ya umeme”. Alisema Mhe. Mgalu.’
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO
Dkt. Alexander Kyaruzi aliwataka Wananchi wa Mbagala kuchangamkia fursa hiyo,
kwani umeme wa uhakika sasa utapatikana katika maeneo hayo. “Ndani ya siku tatu
Wananchi wa Mbagala wataanza kuona tofauti, hii ni kutokana na kuwashwa kwa
Kitu”. Alisema Dkt. Kyaruzi.
No comments:
Post a Comment