Pages

February 26, 2019

KATIBU MKUU NISHATI ATEMBELEA MIRADI YA UMEME KINYEREZI

Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua ametembelea Kituo cha kufua umeme wa Gesi Asilia Kinyerezi I extension na Kinyerezi II jijini Dar es Salaam.
Lengo la ziara yake alisema ni kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa miradi ya Kinyerezi II na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion)
Mradi wa Kinyerezi II ambao unazalisha kiasi cha Megawati 240 tayari umekamilika na umeme umekwishaingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
“Tunashukuru kwamba tunaenda vizuri hasa Kinyerezi II ambayo kiukweli mradi umeshamalizika sasa hivi tunapata umeme kilichobaki ni masuala ya kuweka kila kitu sawa baina ya Mkandarasi na wataalamu wetu.” Alisema Dkt. Mwinyimvua baada ya kupokea taarifa ya miradi hiyo miwili toka kwa Meneja Miradi, Mhandisi Stephene Manda.
Alisema kwa upande wa mradi wa upanuzi Kinyerezi I, (Kinyerezi I extension) kazi imeanza ingawa kulikuwepo na ucheleweshwaji wa vifaa bandarini na kuagiza Uongozi wa TANESCO kukutana na taasisi zinazohusika na masuala ya kodi na utoaji mizigo bandarini ili kupanga utaratibu wa jinsi ya kulipa kodi mbalimbali bila ya kuathiri utoaji wa mizigo hiyo (vifaa na mitambo) bandarini.
“Nakumbuka mlipewa wito na Mheshimiwa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akiwataka mjitahidi isifike mwezi wa nane, ikiwezekana hata mwezi wa tano muwe mmemaliza kazi.” Alisema.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu alifuatana na Kamishna wa Nishati kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Innocent Luoga wakati kwa upande wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO, waliongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Dkt. Tito Mwinuka.
Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu na ujumbe wake, Meneja Miradi wa TANESCO, Mhandisi Stephene Manda, alisema wakati Mradi wa Kinyerezi II Megawati 240 ambao umekamilika tangu Desemba mwaka jana (2018), mradi wa Kinyerezi I ambao unafanya kazi una Megawati 150 na ule wa kufanya upanuzi (Kinyeerzi I extension) utakuwa na Megawati 185 na kazi tayari imefikia asilimia 76%
“Tunategemea mtambo wa kwanza wa mradi huu wa upanuzi tutakuwa tumeuwasha ifikapo mwezi Mei, 2019 na kukamilika kabisa kwa mradi mzima itakuwa Agosti 2019.” Alibainisha Mhandisi Manda na kuongeza Jumla ya umeme utakaokuwa unazalishwa hapa Kinyerezi kufikia Agosti mwaka huu itakuwa Megawati 575.” Alisema
Akifafanua zaidi alisema kutoka pale Kinyerezi I Extension tutakuwa na extension ndogo ya kutoa umeme kwa ajili ya mradi wa SGR.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (katikati) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi, Mhandisi Stephene Manda (kushoto), wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa Gesi Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion), jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (watatu kulia), Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, (watano kulia), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi wa Shirika hilo. Mhandisi Stephene Manda (aliyenyoosha mikono) wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa Gesi Kinyerezi I (Kinyerezi I expansion), jijini Dar es Salaam, Februari 25, 2019.
Katibu Mkuu pia alijionea kituo cha kupokelea gesi kikiwa tayari kwenye eneo la mradi huo.

KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, akipatiwa maelezo.
Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga(kushoto), akiwa na Mkandarasi eneo la mradi.
Katibu Mkuu Dkt. Mwinyimvua na ujumbe wake wakimsikiliza mkandarasi anayetekeleza mradi wa upanuzi Kinyerezi I, kuhusu mwenendo wa mradi huo.
Kiongozi wa zamu wa chumba cha udhibiti mitambo, kwenye mradi wa umeme wa gesi Kinyerezi II, Mhandisi Chidololo Enzi, (kulia) akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Hamisi Hassan Mwinyimvua (katikati), alipotembelea kujihakikishia kukamilika kwa mradi huo unaozalisha Megawati 240.
Kiongozi wa zamu wa chumba cha udhibiti mitambo, kwenye mradi wa umeme wa gesi Kinyerezi II, Mhandisi Chidololo Enzi, (kulia) akitoa maelezo mbele ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Hamisi Hassan Mwinyimvua(kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kushoto).
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua (wapili kushoto), Kamishna wa Nishati, Mhandisi Innocent Luoga, (wakwanza kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO Dkt. Tito Mwinuka (wapili kulia), wakiongozwa na Meneja Miradi wa Shirika hilo. Mhandisi Stephene Manda (aliyenyoosha mkono) wakati Katibu Mkuu akikagua maendeleo ya mradi wa Kinyerezi II jijini Dar es Salaam Februari 25, 2019 ambapo alielezwa kuwa tayari umekamilika.
Hii ndiyo Kinyerezi II kama inavyoonekana Februari 25, 2019 wakati wa ziara ya Katibu Mkuu Nishati, Dkt. Mwinyimvua.




No comments:

Post a Comment