Pages
▼
December 30, 2010
December 28, 2010
RATIBA MPYA YA MGAO WA UMEME.
- Kinondoni Kusini
- Temeke
- Tabora
- Ilala
- Shinyanga
- Morogoro
- Tanga
- Dodoma
- Mbeya
- Mwanza
- Mara
- Kinondoni Kaskazini
- Singida
Ratiba za mikoa mingine tutaendelea kuziweka kadiri zitakavyokuwa tayari zimeandaliwa..
December 27, 2010
JEDWALI LENYE KUONYESHA ONGEZEKO LA BEI YA UMEME KWA UNITI BAADA YA NYONGEZA ILIYOIDHINISHWA NA MAMLAKA YA UDHIBITI WA NISHATI NA MAJI (EWURA)
Makundi ya Watumiaji | Bei ya Matumizi (kWh) | Bei ya sasa Kuanzia 1-Jan-08 (TSh) | Bei Mpya Kuanzia 1-Jan-11 (TSh) | Tofauti kati ya Bei Mpya na ya Zamani(Tsh) | |
D1 | Matumizi madogo madogo ya Nyumbani | Gharama ya chini 0 – 50 kWh/mo | 49/= | 60/= | 11/= |
T1 | Matumizi ya kawaida | Gharama za nishati kwa uniti | 129 /= | 157 /= | 28/= |
T2 | Mahitaji ya juu ya msongo mdogo | Gharama za nishati kwa uniti | 85 /= | 94/= | 9/= |
T3/T3a | Mahitaji ya juu ya msongo mkubwa | Gharama za nishati kwa uniti | 79 /= | 84/= | 5/= |
T5/T3b | Shirika la Umeme Zanzibar | Gharama za nishati kwa uniti | 75 /= | 83 /= | 8/= |
December 24, 2010
TANESCO honours outstanding performers in PDP
TANESCO last Friday(December 17, 2010) honoured best performers of the newly introduced (Performance Development Plan). The Plan, in its initial stage involves Kinondoni North, Kinondoni South, Temeke, Ilala and Coast regions. The evaluation of the performance covered a period of three months starting September this year. The evaluation focused on Financial, Technical and Customer perspectives. While the winners were awarded trophies for their outstanding performances, poor performers were given certificates of concern.
Deputy Chairman of the TANESCO Board of Directors, Mr. Semindu Pawa salutes TANESCO Employees |
The Guest of honour, TANESCO Leadership, TUICO Leaders and Invited guests Sing a famous Workers Union song – Solidarity forever |
TANESCO Managing Director ENG. William Mhando addressing Employees on the success and Challenges facing PDP. |
The Guest of honour Mr. Humphrey Swai on behalf of the Permanent Secretary of MEM addressing TANESCO Employees on PDP |
The Uganda National Water and Sewarage Corporations External Services Director Dr. Silva Mugisha Explains how the quarterly Evaluation of PDP was conducted. |
Five Trophies for presentation to overall winner, winner in the Technical perspective, winner in customer perspective, winner in Financial Perspective and runner up Overall Winner. |
The Managing Director Eng. William Mhando Presenting a Certificate of Concern to Ilala Regional Manager Mr. Innocent Luoga for emerging as the worst Performer in the Technical Perspective |
The Guest of Honour Mr. Humphrey Swai Presenting a trophy to Temeke Regional Manager Mrs. Fatuma Chungu for emerging as the best performer in the Technical perspective. |
The Guest of Honour Mr. Humphrey Swai presenting a Trophy to Regional Manager Ilala Mr. Innocent Luoga for emerging as the best performer in the Financial perspective. |
The Managing Director Eng. William Mhando presenting a certificate of concern to Temeke Regional Manager Mrs. Fatuma Chungu for emerging as the worst Performer in the Financial Perspective. |
Deputy Chairman of the Board Mr. Semindu Pawa presenting a Trophy to Acting Regional Manager Coast Mr. Raymond Seya for emerging as the best performer in the Customer perspective. |
The Managing Director Mr. William Mhando presenting a certificate of Concern to Kinondoni North Regional Manager Mr. Christopher Masasi for emerging as the overall worst Performer. |
Deputy Chairman of the Board Mr. Semindu Pawa presenting a Runner up overall winner trophy to Coast Region acting Regional Manager Mr. Raymond Seya. |
The Guest of Honour Mr. Humphrey Swai presenting an overall Winner Trophy to Kinondoni South Regional Manager Mr. Richard Nsulau. |
A Section of TANESCO employees during the event. |
December 17, 2010
Kishoka mwingine mikononi mwa polisi
Kishoka Abdallah baada ya kukamatwa |
Afisa Usalama Mkoa wa Kinondoni Kusini Bw. Lugazia Cyprian alifanikiwa kumtia mbaroni kishoka Jidah Abdallah akiwa na mfuko wenye sare (koti la mafundi wa TANESCO) na viatu vya kupandia nguzo vyote vikiwa mali ya TANESCO.
December 9, 2010
Kakakuona aonekana TANESCO Mtera
Mnyama ambaye huonekana kwa nadra Kakakuona ameonekana katika kituo cha kuzalisha umeme wa maji cha Mtera kinachoendeshwa na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania TANESCO. Wakazi wa eneo hili walijumuika kufanya tambiko kama ilivyo kawaida ambapo mnyama huyo hutakiwa kutoa utabiri. Kwa mujibu wa Mzee Magomba ambaye ni mmoja wa wazee walioongoza tambiko hilo alisema ni muda mrefu tangu Kakakuona alipoonekana eneo hilo hivyo wanategemea neema kubwa. Baada ya kumaliza tambiko Kakakuona aliruhusiwa kuondoka.
Mzee Magomba akimpaka mafuta na maji Kakakuona kama ishara ya kumuonyesha upendo |
Mzee Magomba akihojiwa na vyombo vya habari vilivyofika eneo hilo |
December 8, 2010
NGELEJA ATEMBELEA MITAMBO YA KUFUA UMEME
Waziri wa Nishati na Madini, Mh. William Ngeleja ametembelea mitambo ya kuzalisha umeme iliyopo jijini Dar es Salaam kujionea hali halisi ya ufuaji wa umeme nchini.
Katika ziara yake hiyo iliyohusisha maafisa wa juu wa Shirika la Umeme nchini TANESCO, iliambatana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Mitambo aliyotembelea ni pamoja na Songas wenye uwezo wa kuzalisha 180MW ambapo kwa sasa unaingiza wastani wa 132MW kwenye gridi ya taifa, IPTL yenye uwezo wa kuzalisha 100MW leo umefikia 70MW na Mtambo wa Tegeta wenye uwezo wa kufua 45MW ambazo zote zinafuliwa kwa sasa na kuingia kwenye gridi ya taifa.
Waziri alipotembelea kituo kikuu cha kudhibiti gridi ya taifa kilichopo Ubungo jijini Dar es Salaam, alipata maelezo kuwa asubuhi ya leo hakukuwa na mgawo wa umeme sehemu zozote nchi nzima mbali na makatizo mengine ya kawaida.Hii inatokana na kuongezeka kwa maji kwenye bwawa la maji la Kihansi.
Aidha waziri alipotembelea mtambo wa Songas aliahidiwa kurejeshwa kwa mtambo mwingine wenye uwezo wa kuzalisha 32MW uliokuwa kwenye matengezo kabla ya mwisho wa wiki hii.
Mh. William Ngeleja akiwa na Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Mhandisi William Mhando wakiingia kwenye kituo cha kuzalisha umeme cha Songas |
Meneja Mtambo wa Songas, Bw. Robert Kofsky akitoa maelezo kuhusu uzalishaji wa kituo hicho |
Meneja Mtambo wa Songas akimuonesha Mh. Ngeleja mtambo uliokuwa kwenye matengenezo unaotarajiwa kuanza kufanya kazi mwishoni mwa wiki hii |
Mh. Ngeleja na maafisa wengine wa TANESCO wakibadilishana mawazo kabla ya kuelekea kwenye mitambo ya Songas |
Mh. Ngeleja akiongea na waandishi wa habari wakati wa ziara hiyo |
Mkurugenzi Mtengaji wa TANESCO, Mh. William Mhando akitoa maelezo kuhusu kituo cha kudhibiti gridi ya Taifa kilichopo Ubungo |
Mh. Ngeleja(wa pili kulia) akipotembelea ndani ya kituo cha kudhibiti gridi cha Ubungo kujionea teknolojia mpya ya digitali inayotumika katika kituo hicho kwa sasa |
Mh. Ngeleja(katikati) alipokuwa anatembelea mitambo ya kufua umeme wa mafuta cha IPTL |
Mh. Ngeleja akioneshwa shughuli ya upakuaji wa mafuta katika kituo cha kufua umeme cha IPTL |
Mh. Ngeleja alipotembelea mitambo ya kufua umeme cha Tegeta akiongozwa na Meneja wa kituo hicho Mhandisi Mohammed Kissiwa (aliyeshika bahasha) |
Meneja Mkuu wa TEKNOHAMA TANESCO, Bi. Salome Nkondola akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu tatizo la LUKU katika vituo mbalimbali vya kuuza LUKU nchini. |
December 7, 2010
UJENZI HOLELA CHINI YA NJIA ZA UMEME
Imetoka kwa mdau wa blog, Innocent Usangira (usangira@gmail.com).
Heshima kwenu wakuu,
Tafadhali naomba kupitia blog zenu tuwasaidie watanzania wenzetu ambao hawajui kuwa si ruhusa kiusalama kufanya shughuli yoyote ile chini ya Tanesco Transmission lines.
Nimeambatanisha picha hii ambayo nimeipiga maeneo ya Tabata
(Kinyerezi) ambako kuna makazi mengi mapya lakini uvunjaji mkubwa wa sheria hizi umeanza kufanyika. Aidha mamlaka husika, Tanesco ikiwa mojawapo hazijawaelimisha wananchi juu ya hili.
Katika picha hii wananchi hawa wanaendelea kujenga majengo ya biashara na makazi chini ya HT Line.Miaka 5 au zaidi baadaye Tanesco au Tanrods itawabomolea majengo yao.Hii ni hatari kwa uchumi wa nchi kwa kuwa ni pesa zinatumika hapa.
Aidha Tanesco wanatakiwa kufanya utaratibu wa kuweka alama za kuwataarifu wananchi kutoendelea kujenga.Watu wengi wanapoteza rasilimali zao kutokana na Mamlaka husika hazitoi elimu ya kutosha kwa wananchi na pia zimekuwa kimya uvunjaji wa taratibu.
Asante
December 6, 2010
TANESCO NA MAENDELEO YAANZA RASMI
- Ni kipindi kipya TBC1
- Kurushwa kila Jumanne saa 1:00 jioni
- Kuchukua nafasi ya kipindi cha Bwana umeme
Kipindi kimepewa jina jipya la “ TANESCO NA MAENDELEO” na kitakuwa kinarushwa na televisheni ya taifa (TBC1) kwa ajili ya kuelimisha jamii na umma ujumla juu ya shughuli, huduma na vipaumbele vya shirika la TANESCO.
Mtakumbuka huko nyuma kulikuwa na kipindi cha kuelimisha umma kiitwacho “Bwana umeme” ambacho kilisitishwa kwa ajili kukiboresha na kukifanya kiendane na wakati ili kuweza kukidhi mahitaji ya wakati huu ambao kuna changamoto nyingi ndani na nje ya shirika.
TANESCO NA MAENDELEO DAIMA!
TAARIFA KWA UMMA - DOWANS Vs TANESCO
The following is brief summary on the awards issued by the International Chamber of Commerce (ICC) in November, 2010 on the Arbitration Cases instituted by Richmond Development Company (Richmond)and Dowans Holdings SA (Costa Rica)/Dowans Tanzania Limited (Dowans) against TANESCO.
BACKGROUND:
Richmond submitted a request for arbitration at the International Commercial court (ICC Tribunal) in September, 2008. The claim amounted to USD 169 million for alleged defamation and damages for termination of the Agreement. The matter was heard in April 2010 in Dubai.
Similarly Dowans submitted a request for arbitration at the ICC Tribunal in November 2008 claiming damages for alleged repudiatory breach of contract and for partially unpaid capacity charges. The claim amounted to USD 149 million. The case was heard in June 2010 in Dar es Salaam.
THE TRIBUNAL’S AWARD
1.1 Arbitration matter No. 15910/VRO RDEVCO LLC d/b/a Richmond Development Company (USA) Versus Tanzania Electric Supply Company Limited.
Richmonds’ claim amounted to USD 169 million. TANESCO has successfully won the case and has been awarded USD 1,201,933.08 million being fifty percent (50%) of TANESCO’s legal and other cost while Richmond was awarded USD 50,000 (United States Dollars Fifty Thousand only) for defamation claim against TANESCO.
1.2 Arbitration matter No. 15947/VRO between Dowans Holdings SA (Costa Rica) and Dowans Tanzania Limited Versus Tanzania Electric Supply Company Limited.
- TANESCO shall pay the sum of U.S. Dollars Twenty-Four million One Hundred Sixty Eight Thousand Three Hundred Forty-Three and Eighty Three cents (US$24,168,343.83), plus simple interest at Seven and One-Half percent (7.5%) per annum on the aggregate principle sum of US$19, 955,626.71from 15th June 2010 to the date of payment.
- TANESCO shall pay the sum of U.S. Dollars Thirty-Nine Million Nine Hundred Thirty-Five Thousand Seven Hundred and Sixty-Five and Fifty cents (US$39,935,765.50) plus simple interest at Seven and One-half percent (7.5%) per annum on the aggregate principle sum of US$36,705,013.94 from 15th June 2010 to the date of payment.
- TANESCO shall pay to Dowans jointly their legal and other costs in the amount of One Million Seven Hundred and Eight Thousand Five Hundred and Twenty One
U.S. Dollars (USD1,708,521).
The actual amount payable to Dowans (the amount awarded including interest) has yet to be calculated based on the Award and the Award has yet to be registered with the High Court of Tanzania as required by law.
TANESCO has requested the Tribunal to register the award with the High Court of Tanzania as is required by law being the process by which foreign arbitral awards allow TANESCO to take any action should it consider necessary.
Despite the rules of arbitration requiring that the award details be confidential, TANESCO is, as a result of the articles published in the local media, entitled to disclose such information about the Award as it finds necessary to protect its interests. TANESCO is still reviewing the Award of the above arbitration matter and where necessary may release more information so that the Awards are not distorted.
December 2, 2010
Kamati za Wahandisi zazinduliwa upya
Picha ya pamoja ya wajumbe wa kamati za wahandisi za Shirika la Umeme Tanzania - TANESCO. |
Kamati za wahandisi za Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) zilizokuwepo kabla ya utawala wa Net Group Solutions zimezinduliwa upya hivi karibuni chini ya Mwenyekiti wake Mhandisi Stephen Mabada ambaye pia ni Meneja Mkuu Ufuaji Umeme.
Kamati hizo zinahusisha wahandisi wa fani zote ndani ya Shirika na zina jumla ya wajumbe 24.
Mhandisi Mabada akisoma risala kwa niaba ya mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Mhandisi William Mhando.
Katika risala yake, Mhandisi Mhando aliwashukuru wajumbe wa Kamati hizo kwa kurejesha tena vikao hivyo ambavyo ni vya juu kabisa vya masuala ya kihandisi ndani ya Shirika.
Mhandisi Mhando alisema atatoa kipaumbele cha kwanza kwa wahandisi kwani ndio msingi wa shughuli kuu za Shirika letu lakini bila kusahau fani nyingine ndani ya shirika.
Akirejea mwito wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw.David Jairo kwenye Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TANESCO lililomalizika hivi karibuni, alisema wahandisi inabidi wapewe kipaumbele ili kufikia malengo ya Shirika.
Mhandisi Mhando pia kwenye risala yake alisema Shirika lina matatizo mengi yanayohitaji wahandisi akitaja tatizo la kufua umeme kwa gharama kubwa na viwango vidogo, upotevu wa umeme wakati wa usafirishaji na usambazaji, wingi wa ajali zitokanazo na kazi za kihandisi na wizi wa miundombinu mbalimbali ya Shirika.
Risala yake pia ilisisitiza matarajio yake kuwa kamati hizo za kihandisi zitasadia kutatua matatizo hayo ya kihandisi na hatasita kuwazawadia wahandisi ambao ubunifu wao utaleta mafanikio katika kutatua matatizo hayo na ubunifu pia wao utapunguza gharama za kutumia washauri kutoka nje ya Shirika.
Shirika la Umeme TANESCO kwa sasa lina jumla ya wahandisi 338 licha ya kuwa zipo sehemu mbalimbali ambazo bado zinahitaji wahandisi, idadi hii ni hazina kubwa kwa Shirika.
Kishoka mwingine ahukumiwa miaka mitatu jela
Kishoka Mansoor mwenye T-shirt ya TANESCO akiwa na mwenzake Jose Kifman |
Vishoka hao wakiteremshwa na polisi |
Kishoka maarufu Mansoor Ibrahim (pichani) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli za TANESCO huku akiwa si mfanyakazi wa TANESCO mbele ya hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Kisutu Mhe. Mwaseba.
Kishoka huyo alikamatwa mwezi machi mwaka huu maeneo ya Tabata Kilungule akitaka kumrubuni mteja wa TANESCO Bw. Seleman Njonanje. Alifunguliwa jalada kituo cha Polisi Kati na hatimaye mahakamani kwa kesi namba CC.236/09.
Kishoka huyo Bw. Mansoor akiwa na kitambulisho chenye jina la Mwijage na sare za Shirika alimghilibu mteja kuwa mita yake ni mbovu na anakwende kuibadilisha na akapatiwa Sh. 500,000/-.