Pages

June 9, 2011

TANESCO na ACB wazindua mkataba wa kuwezesha wateja kupata mikopo ya kuunganishiwa umeme

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi William Mhando akitoa ufafanuzi kuhusu huduma ya “ACB Umeme Loan”.


Baadhi ya viongozi wa TANESCO wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa huduma ya “ACB Umeme Loan”.

Baadhi ya viongozi kutoka Akiba Commercial Bank  waliowakilisha wafanyakazi wa benki hiyo katika uzinduzi wa huduma ya “ACB Umeme Loan”.

Mkurugenzi Mtendaji wa ACB, Bw. John Lwande akihutubia katika uzinduzi wa “ACB Umeme Loan”.

Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi William Mhando (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa ACB,Bw. John Lwande wakiwasha king’ora kuashiria uzinduzi wa huduma ya “ACB Umeme Loans”.

Mwakilishi kutoka CRB (Contractors Registration Board), Mhandisi Consolata Ngimbwa akitoa shukrani zake kwa kuanzishwa kwa huduma hiyo ya “ACB Umeme Loan”.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Leonidas Gama akitoa nasaha zake katika siku ya uzinduzi wa huduma hiyo.


Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na  Akiba Commercial Bank, wamezindua Mkataba wa pamoja unaomwezesha mteja  kupata Mkopo wa kuunganishiwa Umeme,(service line) kwa urahisi.


Mkataba huo baina ya TANESCO na Akiba  ulizinduliwa tarehe 3 Juni mwaka huu na Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco Mhandisi William Mhando na Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank, John Lwande. Hafla hiyo ilifanyika Makao  Makuu ya TANESCO, Ubungo (UMEME PARK).


Huduma hiyo imelenga kuwasaidia wale wote wanaohitaji kuunganishiwa umeme lakini hawana uwezo wa kulipia gharama husika kwa mkupuo mmoja.


Huduma hiyo pia itawanufaisha wakandarasi wa ndani walioshinda zabuni ya kujenga mitandao ya usambazaji wa umeme kwa kuwapa mkopo ambao utawasaidia kupata vifaa vitakavyotumika kupanua mtandao wa umeme kulingana na ukubwa wa mradi.


Kwa mujibu wa mkataba huo, mikoa itakayonufaika na mikopo hii ni pamoja na Dar es salaam, Arusha na Kilimanjaro. Hii ni mikoa ambayo ACB in matawi ya kutolea huduma. Kwa mkoa wa Mwanza watakaonufaika na mkopo huu ni wakandarasi tu kwani mkoa huu hauna tawi la ACB.
“Huduma hii imeanzishwa kukidhi mahitaji ya wateja wetu wapya wanaoshindwa kulipia gharama kwa ajili ya kuunganishiwa umeme kwenye nyumba zao. Faida zitakazopatikana ni pamoja na uhuru wa upatikanaji wa mkopo, unafuu wa gharama za malipo, uhuru wa kuchagua muda wa marejesho ya mkopo ambayo ni kati ya miezi sita na ishirini na nne, pamoja na fursa ya kupata huduma nyinginezo za kibenki kama amana mbalimbali,” alisema Mhandisi Mhando.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank  aliwahakikishia wananchi kwamba ushirikiano huu kati ya ACB na TANESCO ni wa kudumu na si huduma ya msimu, na cha msingi mteja awe na vigezo vya kumwezesha kupata mkopo huo kwa urahisi.
Bwana Lwande alitaja sifa za mwombaji wa mkopo huo kuwa ni: 
Mkopaji awe mmiliki halali wa makazi/nyumba inayoombewa mkopo,mwombaji atatakiwa awasilishe ACB nyaraka zinazohakiki umiliki wa nyumba yake kama hatimiliki au leseni ya makazi aua hati ya mauziano au barua ya serikali ya mtaa anakoishi.


Sifa nyingine ni: awe tayari amepewa na TANESCO makadirio ya gharama za kuunganisha umeme, awe na chanzo cha mapato kinachothibitika kama biashara au ajira halali, awe mwombaji mwenye historia nzuri ya ulipaji mikopo kutoka ACB au benki nyingine.

4 comments:

  1. Ni mpango maridhawa unaokidhi kiu ya walengwa.
    Wakati hayo yakirindima huko ACB na TANESCO sina hakika sana iwapo elimu iliyotolewa kwa umma ni ya kiwango sahihi.

    ReplyDelete
  2. Maisha ya wakati wetu yanaboreshwa na kuangazwa na umeme kuanzia mijini hadi vijijini.Ni vema sasa gharama za kuunganishiwa umeme zifanyiwe marekebisho kulingana na maisha ya mwananchi wa kawaida ili pale inapowezekana maisha ya kila mwananchi yaangazwe na kuboreshwa na nishati ya umeme kutoka Tanesco.

    ReplyDelete
  3. Thanks and that i have a super provide: Who Repairs House Foundations home renovation in canada

    ReplyDelete