Pages

August 29, 2013

KAGERA

KATIZO LA UMEME MKOA WA KAGERA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linasikitika kuwatangazia wateja wake wa mkoa wa Kagera kwamba  kutakua na katizo la umeme katika siku za IJUMAA, JUMAMOSI NA JUMAPILI kuanzia saa 12:30 asubuhi hadi 12:30 jioni kwa mfululizo wa wiki AROBAINI (40). Katizo hili litaanza JUMAPILI ya tarehe 01/09/2013. Sababu ni Uboreshaji wa njia kuu ya usafirishaji wa umeme utakaofanywa na Kampuni ya umeme ya  Uganda nje ya mipaka
ya Tanzania nchini Uganda. 

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:-
Maeneo yote ya Wilaya za Muleba, Karagwe,  Bukoba vijijini na Bukoba mjini.
Shirika linaomba radhi kwa wateja wake wote kwa usumbufu utakaojitokeza.
 
Tanesco tunaangaza maisha yako.
 
 
IMETOLEWA NA:  OFISI YA UHUSIANO
TANESCO -  MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment