Pages

December 4, 2014

TAARIFA KWA UMMA




TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKOSEKANA KWA UMEME
KWA BAADHI YA MAENEO NCHINI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linanapenda kutoa ufafanuzi kwa wateja wake kuhusu sababu za kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo nchini kwa nyakati tofauti kama ifuatavyo:-

Mosi, Kuanzia Novemba 26, 2014 hadi Desemba 1, 2014 Mikoa yote iliyoungwa kwenye gridi ya taifa ilikuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo kutokana na kuharibika kwa mashine moja ya Mtambo wa Kufua Umeme wa Kidatu yenye uwezo wa kufua megawati 50. Mtambo huo kwa sasa umetengamaa na hakuna Mkoa wenye upungufu wa umeme.

Pili, Novemba 29, 2014 Kulitokea hitilafu ya kulipuka na kuungua kwa Kikata Umeme (Circuit Breaker) kwenye Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha Ubungo upande wa msongo wa kilovolti 33 na hivyo kusababisha gridi nzima ya taifa kutoka saa 11.38jioni na kurejesha saa 3.03 usiku kwa mikoa yote baada ya kutengeneza kifaa kilichoharibika. Hata hivyo baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) yaliendelea kukosa umeme kwa siku 2 mfululizo hadi tulipo funga Kikata Umeme kingine. Tatizo hilo limesha patiwa ufumbuzi na Mkoa huo kwa sasa unapata umeme kama kawaida.

Tatu, Kuanguka kwa nguzo kwa baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam kutokana na kuanza kwa kipindi cha mvua.

Nne, Matengenezo yanayoendelea ya ukarabati wa miundombinu kwa mikoa yote ya nchini. Kazi zinazofanyika kwenye zoezi hilo kwa sasa ni kubadilisha nguzo zilizooza, kunyanyua nguzo zilizoinama, kuvuta nyaya zilizolegea na kukata miti inayogusa nyaya za umeme. Zoezi kama hili hufanyika kwa kila mkoa kwa nchi nzima kama tahadhari kabla ya kuanza kwa kipindi cha masika ambacho kinaambatana na mvua na upepo mkali.

Kwa sababu hii kubwa, kumekuwa na usumbufu wa kukatwa kwa umeme kwa baadhi ya maeneo kwa nyakati tofauti kulingana na ratiba ya mkoa husika ili kupisha zoezi hilo ambalo tunatarajia litakamilika mwezi huu wa Desemba.

Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Imetolewa na
Ofisi ya Uhusiano,

1 comment:

  1. Izo ni kisingizio tuu.. nie tanesco ni shirika ambao mnatutoza pesa kushinda shirika yoyote nchini, tuna nunua nguzo, wire, machine ya luku, na umeme tushailipia hata kabla hatujaitumia, pia kila mwezi mnatoza kodi za kuonganisha kwenye grid... baado hapa kigamboni hamjaeza kuimuudu. Mkakaata umeme leo hi kuanzia asubuhi, hadi saa 3 usiku na baada kisaa 1 tuu, kwenye saa 4 mkakata tena. Majuzi hapa umeme ilikua ina fluctuations (kuongezeka na kupunguzwa volti). Kweli mnachofanya haifahmiki wala hameleweki.
    Hongera ka miaka 53 wa utawala uzalendo.
    Achebi na management corruption!!!

    ReplyDelete