TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKOSEKANA KWA UMEME
KWA BAADHI YA MAENEO NCHINI
Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) linanapenda kutoa
ufafanuzi kwa wateja wake kuhusu sababu za kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya
maeneo nchini kwa nyakati tofauti kama ifuatavyo:-
Mosi, Kuanzia Novemba 26, 2014 hadi Desemba 1, 2014 Mikoa yote iliyoungwa
kwenye gridi ya taifa ilikuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo
kutokana na kuharibika kwa mashine moja ya Mtambo wa Kufua Umeme wa Kidatu yenye
uwezo wa kufua megawati 50. Mtambo huo kwa sasa umetengamaa na hakuna Mkoa
wenye upungufu wa umeme.
Pili, Novemba 29, 2014 Kulitokea hitilafu ya kulipuka na kuungua kwa
Kikata Umeme (Circuit Breaker) kwenye Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha
Ubungo upande wa msongo wa kilovolti 33 na hivyo kusababisha gridi nzima ya
taifa kutoka saa 11.38jioni na kurejesha saa 3.03 usiku kwa mikoa yote baada ya
kutengeneza kifaa kilichoharibika. Hata
hivyo baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) yaliendelea kukosa
umeme kwa siku 2 mfululizo hadi tulipo funga Kikata Umeme kingine. Tatizo hilo
limesha patiwa ufumbuzi na Mkoa huo kwa sasa unapata umeme kama kawaida.
Tatu,
Kuanguka kwa
nguzo kwa baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam kutokana na kuanza kwa
kipindi cha mvua.
Nne, Matengenezo yanayoendelea ya ukarabati wa miundombinu kwa mikoa
yote ya nchini. Kazi zinazofanyika kwenye zoezi hilo kwa sasa ni kubadilisha
nguzo zilizooza, kunyanyua nguzo zilizoinama, kuvuta nyaya zilizolegea na kukata
miti inayogusa nyaya za umeme. Zoezi kama hili hufanyika kwa kila mkoa kwa nchi
nzima kama tahadhari kabla ya kuanza kwa kipindi cha masika ambacho kinaambatana
na mvua na upepo mkali.
Kwa sababu hii kubwa, kumekuwa na usumbufu
wa kukatwa kwa umeme kwa baadhi ya maeneo kwa nyakati tofauti kulingana na
ratiba ya mkoa husika ili kupisha zoezi hilo ambalo tunatarajia litakamilika
mwezi huu wa Desemba.
Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa
usumbufu wowote uliojitokeza.
Imetolewa
na
Ofisi
ya Uhusiano,
Izo ni kisingizio tuu.. nie tanesco ni shirika ambao mnatutoza pesa kushinda shirika yoyote nchini, tuna nunua nguzo, wire, machine ya luku, na umeme tushailipia hata kabla hatujaitumia, pia kila mwezi mnatoza kodi za kuonganisha kwenye grid... baado hapa kigamboni hamjaeza kuimuudu. Mkakaata umeme leo hi kuanzia asubuhi, hadi saa 3 usiku na baada kisaa 1 tuu, kwenye saa 4 mkakata tena. Majuzi hapa umeme ilikua ina fluctuations (kuongezeka na kupunguzwa volti). Kweli mnachofanya haifahmiki wala hameleweki.
ReplyDeleteHongera ka miaka 53 wa utawala uzalendo.
Achebi na management corruption!!!