Pages

August 24, 2016

mradi wa maboresho ya umeme mkoani arusha (tedap project)



SCOPE YA MRADI:
1.       Ujenzi wa miundo mbinu mipya ya kilovolti 33 na uongeza ukubwa wa waya(size) kutoka 50sqmm mpaka 150sqmm(Upgrading of Arusha Distribution Lines) na Laini hizi mpya hupita kwenye maeneo zilikopita laini za zamani(zinazohudumia wananchi kwa sasa)  kutokana na ufinyu wa njia(wayleave)
Njia hizo ni:- Kutoka kituo kikuu cha Njiro kwenda Njiro B(Engutoto-Kituo Kipya),Njiro B(Engutoto-Kituo Kipya)  kwenda kituo kikuu cha Njiro, Kituo kikuu cha Njiro kwenda kituo cha Awali cha Themi ,Kituo kikuu cha Njiro kwenda kituo cha awali cha Mt. Meru, Kutoka kituo cha Mount meru kwenda Sakina Substation (Hiki ni Kituo Kipya-Kipo Ngaramtoni ya juu)  NA kituo kikuu cha Njiro kwenda kituo cha Awali cha Kiltex na kituo cha Unga ltd, Laini ya unga limited kwenda SINONI

2.       Ujenzi wa Mzunguko wa njia za umeme kuwezesha upatikanaji wa njia Mbadala pindi kituo kimoja cha Awali  kinapokuwa na hitilafu(ring circuit).
Njia hizo ni: Kuunga Kiltex na Ungaltd, Kuunga Unga Limited na Sakina Kituo kipya, Kuunga Mt. Meru na Sakina Substation (Ngaramtoni ya juu).

3.       Upanuzi wa Vituo vinne vya zamani (primary substation) kutoka 5MVA mpaka 15MVA ili kwenda na kasi ya ukuaji wa jiji la Arusha.
     Vituo hivyo ni Mt. Meru, Kiltex, Themi, Unga Limited

4.       Ujenzi wa vituo viwili vipya vya Primary substation ambavyo ni SAKiNA (Ngaramtoni ya Juu) na Njiro B( kilichopo Engutoto kuelekea  Njiro kwa Msola).

5.       Uwekaji wa Transfoma za upili(Mashine umba-secondary substations) sehemu  43 katika maeneo mbalimbali yaliyoanishwa kuwa na umeme mdogo mkoani Arusha hasa Arusha Mjini.

6.       Ujenzi wa njia za Matoleo kwenye kituo  kikuu cha Njiro na vituo vya awali vinavyojengwa au kuongezwa uwezo. Nayo imekuwa ni sababu ya umeme kuzimwa jiji Arusha.

Sababu za Kujengwa kwa Mradi huu wa TEDAP ni
·         -Kuongeza upatikanaji wa umeme wenye ubora (Voltage improvement) na upatikanaji wa umeme wa uhakika.
·         Kuepusha kukatika  kwa umeme mara kwa mara  kutokana vituo kuzidiwa uwezo na kuweka  ring circuit kwa maeneo ili kuwahudumia wateja pindi upande mwingine unapokuwa na hitilafu .
·         Kujiandaa na changamoto za maendeleo za ukuaji wa viwanda na ukuaji wa mji (new master plan).Mfano Satelite cities plan( Salian City, Safari city, Bondeni city  n.k) , Maendele ya viwanda hasa uwepo wa wewekezaji wa viwanda vikubwa na upanuzi wa vilivyopo mkoani Arusha. Na kwa kuzingatia sera za serikali yetu tukufu ya Awamu ya tano.


SABABU YA KUKATIKA KWA UMEME:
Mambo sita(6) yaliyoainishwa hapo juu ndizo sababu  za uzimaji wa  umeme unaoendelea maeneo mbalimbali mkoani Arusha. Uzimaji huu unaenda kwa ratiba ya siku tatu kwa wiki kwa maeneo mengi ya Arusha (One day on-one day off – 0.800 am – to 17.00hrs) kwa mwezi wa saba(7) na wa nane(8).
Hatuna budi kusifu na kupongeza serikali kwa Miradi hii inayotekelezwa kwa  manufaa ya wananchi wa Arusha. Miradi ikikamilika italeta huduma bora na kuongeza kasi ya maendeleo ya mkoa kwa miaka mingi ijayo.

Mwisho: Tunawaomba wananchi wetu wa Arusha kuwa na subira wakati huu ambao serikali imewekeza gharama kubwa ili kuboresha huduma ya umeme mkoani kwa manufaa yetu, na vizazi vijavyo.

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO!!!

No comments:

Post a Comment