SCOPE YA MRADI:
1.
Ujenzi wa miundo mbinu mipya ya kilovolti 33 na
uongeza ukubwa wa waya(size) kutoka 50sqmm mpaka 150sqmm(Upgrading of Arusha Distribution
Lines) na Laini hizi mpya hupita kwenye maeneo zilikopita laini za zamani(zinazohudumia
wananchi kwa sasa) kutokana na ufinyu wa
njia(wayleave)
Njia hizo ni:- Kutoka kituo kikuu cha Njiro
kwenda Njiro B(Engutoto-Kituo Kipya),Njiro B(Engutoto-Kituo Kipya) kwenda kituo kikuu cha Njiro, Kituo kikuu cha
Njiro kwenda kituo cha Awali cha Themi ,Kituo kikuu cha Njiro kwenda kituo cha
awali cha Mt. Meru, Kutoka kituo cha Mount meru kwenda Sakina Substation (Hiki
ni Kituo Kipya-Kipo Ngaramtoni ya juu)
NA kituo kikuu cha Njiro kwenda kituo cha Awali cha Kiltex na kituo cha
Unga ltd, Laini ya unga limited kwenda SINONI
2.
Ujenzi wa Mzunguko wa njia za umeme kuwezesha
upatikanaji wa njia Mbadala pindi kituo kimoja cha Awali kinapokuwa na hitilafu(ring circuit).
Njia hizo ni: Kuunga Kiltex na Ungaltd,
Kuunga Unga Limited na Sakina Kituo kipya, Kuunga Mt. Meru na Sakina Substation
(Ngaramtoni ya juu).
3.
Upanuzi wa Vituo vinne vya zamani (primary
substation) kutoka 5MVA mpaka 15MVA ili kwenda na kasi ya ukuaji wa jiji la
Arusha.
Vituo hivyo ni Mt. Meru, Kiltex, Themi,
Unga Limited
4.
Ujenzi wa vituo viwili vipya vya Primary
substation ambavyo ni SAKiNA (Ngaramtoni ya Juu) na Njiro B( kilichopo Engutoto
kuelekea Njiro kwa Msola).
5.
Uwekaji wa Transfoma za upili(Mashine umba-secondary
substations) sehemu 43 katika maeneo
mbalimbali yaliyoanishwa kuwa na umeme mdogo mkoani Arusha hasa Arusha Mjini.
6.
Ujenzi wa njia za Matoleo kwenye kituo kikuu cha Njiro na vituo vya awali
vinavyojengwa au kuongezwa uwezo. Nayo imekuwa ni sababu ya umeme kuzimwa jiji
Arusha.
Sababu za Kujengwa
kwa Mradi huu wa TEDAP ni
·
-Kuongeza upatikanaji wa umeme wenye ubora
(Voltage improvement) na upatikanaji wa umeme wa uhakika.
·
Kuepusha kukatika kwa umeme mara kwa mara kutokana vituo kuzidiwa uwezo na kuweka ring circuit kwa maeneo ili kuwahudumia
wateja pindi upande mwingine unapokuwa na hitilafu .
·
Kujiandaa na changamoto za maendeleo za ukuaji
wa viwanda na ukuaji wa mji (new master plan).Mfano Satelite cities plan(
Salian City, Safari city, Bondeni city
n.k) , Maendele ya viwanda hasa uwepo wa wewekezaji wa viwanda vikubwa
na upanuzi wa vilivyopo mkoani Arusha. Na kwa kuzingatia sera za serikali yetu
tukufu ya Awamu ya tano.
SABABU
YA KUKATIKA KWA UMEME:
Mambo sita(6) yaliyoainishwa hapo juu ndizo
sababu za uzimaji wa umeme unaoendelea maeneo mbalimbali mkoani
Arusha. Uzimaji huu unaenda kwa ratiba ya siku tatu kwa wiki kwa maeneo mengi
ya Arusha (One day on-one day off – 0.800 am – to 17.00hrs) kwa mwezi wa
saba(7) na wa nane(8).
Hatuna budi kusifu na kupongeza serikali
kwa Miradi hii inayotekelezwa kwa
manufaa ya wananchi wa Arusha. Miradi ikikamilika italeta huduma bora na
kuongeza kasi ya maendeleo ya mkoa kwa miaka mingi ijayo.
Mwisho: Tunawaomba wananchi wetu wa Arusha
kuwa na subira wakati huu ambao serikali imewekeza gharama kubwa ili kuboresha
huduma ya umeme mkoani kwa manufaa yetu, na vizazi vijavyo.
TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO!!!
No comments:
Post a Comment