|
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani |
|
|
|
|
|
|
|
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwa katika ziara ya kukagua
mitambo ya kuzalisha umeme kwa njia ya gesi asilia Mkoani Mtwara,
amekitembelea Kijiji cha Kalipembe kitakacho nufaika na mradi wa umeme
Vijijini Awamu ya Tatu.
Kijiji hicho kipo Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara, ambapo Wananchi
wamekuwa wakihitaji na adha ya kutokuwa na umeme licha ya njia ya
imepita kuelekea Wilaya ya Newala miaka 18.
Dkt. Kalemani akiambatana na Viongozi wa TANESCO na REA aliwahakikisha
Wananchi wa Kijiji hicho kupata umeme kupitia Awamu ya Tatu ya umeme
Vijijini.
"Ndugu zangu Wananchi kazi yetu ni moja tu kuhakikisha mnapata umeme,
Serikali ya Awamu ya Tano imekusudia kuleta maendeleo kwa Wananchi wote,
bila kujali itikadi kwani suala la maendeleo halina vyama". Alisema
Dkt. Kalemani.
Aidha, alitoa maagizo kwa Mkandarasi kuanza kazi mara moja ya kuchimbia
nguzo, na kuutekeleza mradi huo bila kuruka Kijiji, Kitongoji hata
Kaya, ambapo Mkandarasi aliahidi kuanza kazi mapema Wiki ijayo.
Akiongelea hali ya upatikanaji wa umeme Mikoa ya Lindi na Mtwara, Dkt.
Kalemani alisema hivi sasa Mkoani wa Mtwara hakuna tatizo la umeme baada
ya Matengenezo kukamilika.
"Kwa Mkoa wa Lindi tumeunda tume ya watu wa tano ili kufuatilia tatizo
lipo sehemu gani katika miundobonu, tunawaahidi hali kuimarika baada ya
muda mfupi". Alisema Dkt. Kalemani.
Aliongeza, Mikoa ya Kusini inatarajiwa kupata suluhisho la kudumu la
tatizo la umeme itakapoingizwa katika Gridi ya Taifa, ambapo mwakani
Mwezi Aprili inatarajiwa kituo cha Kuzalisha umeme cha Megawati 300
kuanza kujengwa.
Dkt. Kalemani anaendelea na ziara yake ambapo amekagua kituo cha
kuzalisha umeme cha Tunduru, na cha Namtumbo vilivyopo Wilaya ya Ruvuma
akiwa anaelekea katika Mradi wa Makambako - Songea.