March 23, 2012

Balozi wa Japan nchini atembelea Chuo Cha TANESCO Masaki

Balozi wa Japan Mr. Masaki Akodo, akielezea jambo, Chuo Cha TANESCO jana.

Balozi wa Japan nchini Bw. Masaki Okoda, Machi 22, 2012 ametembelea  Chuo Cha TANESCO, kilichopo Masaki Jijini Dar es Salaam ikiwa ni ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Shirika la Ushirikiano la Kimataifa la Japan  (JICA).  JICA wamekuwa wakishirikiana na chuo hicho katika kuandaa mitaala na pia wamekuwa wakilisaidia Shirika la umeme Tanzania  (TANESCO) kwa ushauri katika masuala ya ufundi na teknolojia.

March 19, 2012

TANESCO yatoa ufafanuzi - kukatika katika Umeme






Mkurugenzi wa Tanesco Tanzania, Mhandisi. William Mhando ameongea na waandishi wa habari kuelezea hali ya umemeilivyo kwa sasa nchini pia kutoa  ufafanuzi wa tatizo la umeme lililojitokeza katika maeneo tofauti ya jiji la Dar es Salaama.

March 16, 2012

Jamii yaamua kuzuia wizi wa mafuta ya transfoma za TANESCO

Wakazi wa Mtaa wa Kondo Bahari Beach uliopo Kata ya Kunduchi, wameamua kujengea uzio transifoma za umeme zilizopo katika mtaa wao ili kuzuia wizi wa mafuta, ambao umekithiri katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es salaam. Wizi huu hufanya transifoma kulipuka na kuungua hivyo kuwaacha wateja wakiwa gizani lakini pia unaliingizia Shirika hasara kubwa kwa kununua transifoma mpya. 

March 12, 2012

Tunaomba radhi kwa wateja wetu wa Upanga na Katikati ya Mji (CITY CENTRE)


Hii ndio Transifoma iliyoharibika
Shirika la Umeme Tanzania – TANESCO linapenda kuwaomba radhi wateja wake wote wanaoishi maeneo ya Upanga Mashariki, Eneo la Sea View ,Eneo la kituo cha polisi Daraja la Salender  ,Hospitali ya  Agakhan ,  Mtaa wa  Azikiwe, Mtaa wa Mkwepu, Mtaa wa Makunganya, Bilicana Club, Maeneo yaliyoko kando kando ya barabara ya  Bibi Titi, Mahakama ya Kisutu ,Maktaba kuu ya Tanganyika, NSSF, DIT-Chuo cha ufundi, Upanga Magharibi, Maeneo ya ofisi za zima moto, Diamond Jubilee,Hospitali ya  Tumaini , JWTZ Upanga,Hoteli ya  Movenpik Serena , Barcklays House na maeneo yanayoizunguka kwa tatizo la kukosa umeme kuanzia tarehe 06/03/2012 jioni   hadi tarehe 9/03/2012 kutokana na kuharibika kwa transfoma kubwa iliyopo katika kituo chetu cha City Centre cha kusambazia umeme kwenye maeneo hayo kilichopo mkabala na  mahakama ya kisutu.

Kazi ya dharura ya kurejesha umeme maeneo hayo ilikamilika tarehe 09/03/2012 majira ya saa tisa usiku.
                                                                                                 
Uongozi wa mkoa wa Ilala pamoja na uongozi wa Shirika kwa ujumla unaomba radhi na kuwapa pole wateja wote kwa usumbufu wote walioupata kutokana na tatizo hili.

Kwa msaada na  matukio ya dharura tafadhali piga simu namba :
022 213 3330, 0784 768586, 0715 768586 ofisi ya mkoa Ilala, 0715 76 85 84 au 0688 00 10 71 ofisi ya wilaya ya Gongo la Mboto, 0684 00 10 68 ofisi ya wilaya ya Tabata na 0684 001066 ofisi ya wilaya ya viwandani. Nama za kituo cha huduma kwa wateja( Call centre numbers) 2194400 au 0768 985 100

Imetolewa naOfisi ya Uhusiano
TANESCO
Makao Makuu.

March 8, 2012

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME


Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-


TAREHE: 10/03/2012; Jumamosi


SAA: 3:00 Asubuhi- 12:00 Jioni


SABABU: Kufanya kazi za Matengenezo kwenye njia ya umeme Ilala-Buguruni

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA: 


Maeneo ya Vingunguti , Jambo plastics, Sehemu ya maeneo ya Kiwalani, sehemu ya maeneo yaliyoko kandokando ya barabara ya Nyerere kuanzia TAZARA hadi kiwanda cha PEPSI,Kiwanda cha Bakhresa Food Products cha Buguruni na Maeneo yanayokizunguka.

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:


022 213 3330, 0784 768586, 0715 768586 ofisi ya mkoa wa Ilala Samora, 0715 76 85 84 or 0688 00 10 71 Ofisi ya wilaya Gongo la Mboto, 0684 00 10 68 Ofisi ya wilaya Tabata na 0684 001066 Ofisi ya wilaya ya viwanda. (Call centre numbers) 2194400 au 0768 98 51 00


Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza

Limetolewa na: Ofisi ya Uhusiano

TANESCO Makao Makuu

March 6, 2012

Statnett - Norway- waongea na wadau kuhusu taswira yaTANESCO


Makamu wa Rais wa Statnett, anayeshughulika Masuala ya Kimataifa, 
 Bw. Tor Inge Akselsentoka,(wa kwanza kutoka kulia), 
akiongea na wahandishi wa habari, hawapo pichani. , 
Bi. Kari Vestgarden (katikati) na Bw.Anders Moe 

Wawakilishi wa Kampuni ya Statnett kutoka Norway inayojishughulisha na masuala ya usafirishaji umeme nchini humo, wapo nchini kwa ajili ya kulijengea uwezo Shirika la Umeme Tanzania TANESCO katika masuala ya Utawala bora, Undeshaji, Miradi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

March 5, 2012

Shirika lawapongeza mafundi wa kikosi maalumu cha karabati umeme Dar.



Meneja Uhusiano, Bi. Badra Masoud, akisakata rumba 
pamoja na mafundi wa KAUDA.
Baada ya Kikosi maalumu cha kukarabati umeme Dar es salaam(KAUDA), kumaliza kazi ya kufikisha umeme kwa muda mfupi, wa siku kumi na nne, Shirika lawapongeza kwa tafrija fupi iliyofanyika katika viunga vya Chuo cha TANESCO, Masaki.

TANESCO na JICA waimalisha ushirikiano


         Wakarabati kituo kidogo cha kupoza umeme cha Ilala kwa pamoja.
 
Naibu Mkurugenzi wa TANESCO Usafirishaji
 Mwandisi Decklan Muhaki, akijadili jambo na  
Mmoja wa Wataalamu toka JICA
JICA, wakala wa Japan katika kusaidia nchi za Afrika katika kuzijengea uwezo kimaendeleo. Imekuwa na ushirikiano mzuri na Shirika la  Umeme Tanzania (TANESCO), Ambapo wamekuwa wakilisaidia shirika la TANESCO katika kuwajengea uwezo wataalamu wake  katika kuboresha utendaji kazi wao.

TANESCO mkoa wa Ilala wafungua Ofisi mpya ya wilaya ya Tabata, Gongolamboto na Ofisi ya TANESCO Viwandani

Dada Penina wa kitengo cha dharura, wilaya Gongolamboto
 akiwa katika kazi zake za kila siku.
Katika kuboresha na kusogeza huduma kwa wateja wa huduma ya umeme mkoani Ilala, Shirika la Tanesco limefungua ofisi ya wilaya ya Tabata. Kabla ya ofisi hii mteja toka Tabata alitakiwa kwenda ofisi za TANESCO Mkoa  Ilala zilizopo katikati ya mji ili kufuata huduma mbalimbali zinazotolewa na TANESCO mkoa. Kwa sasa mteja wa TANESCO wilaya ya Tabata wataenda Tabata shule nyuma , ambapo ndipo ofisi za wilaya zilipo.

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME


Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala  kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

TAREHE:   07/03/2012 (Jumatano) na 09/03/2012 (Ijumaa)
                    
MUDA:        3:00 Asubuhi - 12:00 Jioni

SABABU:     Kufanya matengenezo, kubadilisha nguzo na kukata matawi ya miti katika Line ya  
                      Msongo mkubwa ya Fz III-II

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:-
Tabata Kisiwani,Tabata Kimanga,Kisukulu,Bonyokwa,Tabata segerea,Tabata Kinyerezi,Tabata Bima,Ukonga Segerea,Moshi Bar,Kipunguni,Mazizini,Kisarawe,Pugu Mikongeni, Kajiungeni, Chanika, Markuz,Chuo cha kampala,Ukonga Magereza,Majohe,Namera Group,Karakata,Sitaki shari na Tabata Chang’ombe.

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:-
022 213 3330, 0784 768586, 0715 768586 ofisi ya mkoa Ilala, 0715 76 85 84 au 0688 00 10 71 ofisi ya wilaya ya Gongo la Mboto, 0684 00 10 68 ofisi ya wilaya ya Tabata na 0684 00 10 66 ofisi ya wilaya ya viwandani.
Namba za kituo cha kutoa huduma kwa wateja( Call centre numbers) ni 2194400 au 0768 985 100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


Imetolewa na:       Ofisi ya Uhusiano,
                               TANESCO – Makao Makuu

March 3, 2012


Mwili wa Bw. GODLISTEN baada ya kupigwa shoti 
ambayo ilisababisha kifo 
Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Godlisten, amefariki dunia kwa kupigwa shoti ya umeme, akituhumiwa kujaribu kuiba mafuta ya transifoma, iliyoko katika Kituo kikuu cha mabasi, Arusha mjini.

TUNAOMBA RADHI KWA WATEJA WETU


Shirika la Umeme Tanzania  – TANESCO linapenda kuwaomba radhi wateja wake wote wanaoishi maeneo ya Gongo la mboto, Ukonga, Segerea, Moshi Bar, Kipunguni,  Mazizini, Kisarawe, Pugu Mikongeni,Pugu Kajiungeni,Chanika,Markaz,Chuo Cha Kampala, Ukonga Magereza, Majohe, Kiwanda cha Namera, Tabata Kisiwani, Tabata Kisukulu, Bonyokwa, Tabata Segerea, Tabata Kinyerezi, Tabata Bima, Tabata Chang’ombe, Karakata, Stakishari, Kisarawe na baadhi ya Maeneo ya viwanda vilivyopo  kandokando ya barabara ya Mandela hadi Mwananchi kutokana na tatizo la kukatikakatika kwa umeme kwenye maeneo hayo.

Tatizo hilo limesababishwa na kuharibika kwa transfoma kubwa iliyoko katika kituo chetu cha umeme cha Kipawa iliyokuwa inasambaza umeme kwenye maeneo hayo.Tatizo hilo lilipelekea kutumia njia mbadala ya kusambazia umeme ya kutoka Ubungo badala ya ile ya awali ya Kipawa ambayo kuanzia mwezi wa Januari, 2012 hadi sasa imezidiwa kutokana na ongezeko kubwa la matumizi ya umeme. Mikakati ya dharura ya kulishughulikia tatizo hilo inaendelea ikiwa ni pamoja na kukarabati njia hiyo ya kusambazia umeme kwa kuimarisha maungio,kubadilisha nguzo zilizooza na kukata matawi ya miti yanayoizonga njia hiyo.

Pia ujenzi wa njia mpya unaendelea ili kuhamisha wateja wa kisarawe na Gongo la Mboto kupata umeme kupitia kituo cha Ilala.Mikakati ya muda mrefu ni pamoja na kushughulikia upatikanaji wa transfoma kubwa ya Kipawa na upanuzi wa kituo hicho.
Kwa msaada na  matukio ya dharura tafadhali piga simu namba zifuatazo:-
022 213 3330, 0784 768586, 0715 768586 ofisi ya mkoa Ilala, 0715 76 85 84 au 0688 00 10 71 ofisi ya wilaya ya Gongo la Mboto, 0684 00 10 68 ofisi ya wilaya ya Tabata na 0684 001066 ofisi ya wilaya ya viwandani. Nama za kituo cha huduma kwa wateja (Call centre numbers) 2194400 au 0768 985 100
Shirika linasikitika kwa usumbufu wowote unaojitokeza kutokana na tatizo hili.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu




March 2, 2012

TANESCO yafanikiwa kukamilisha ahadi ya Rais,kwa kufikisha umeme Mabwepande



Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Badra Masoud alipotembelea 
Makazi ya waathirika wa Mafuriko , Mabwepande.
Hatimaye Tanesco imekuwa taasisi ya kwanza kumaliza kuweka miundombinu mipya ya umeme kwa waathirika wa mafuriko waliopewa makazi mapya Mabwepande. Kufuatia janga la mafuriko lilitokea sehemu kadhaa za viunga vya Mji wa Dar Es Salaam na Serikali kuamua kuwahamishia wakazi wote waliokuwa katika maeneo hayo hatari kwa kuwapatia maeneo nje kidogo ya mji, Mabwepande kuwa makazi yao mapya na ya kudumu.