KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
linasikitika kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni
Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme litakalotokana na
matengenezo katika kituo cha Mbezi Substation Siku ya Jumamosi tarehe
31/08/2013 kuanzia saa
0300 Asubuhi hadi saa
0900 Mchana.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Maeneo ya Mwenge, Lugalo Military base, Lugalo Hospitali, Maeneo yote ya Kawe, Maeneo ya Mbezi Beach na vitongoji vyake,
Tafadhali usishike waya uliokatika, na toa taarifa kupitia simu zifuatazo kwa dharula yeyote
022 2700367, 0784 768584, 0716 768584 Au Call centre namba 2194400.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na: Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO,MAKAO MAKUU