Rais wa Benki ya Maendeleo ya Africa Dkt .Akinumwi A . Adesina,
ametembelea kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Zuzu kilichopo Mkoani Dodoma, na kujionea jinsi kituo hicho kilivyo saidia kuboresha
hali ya upatikanaji wa umeme katika Mkoa huo.
Kituo hiki ni miongoni mwa vituo
vilivyo karabatiwa kupitia mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Mkoani Iringa hadi Shinyanga
ya msongo wa Kilovolti 400 ujulikanao kama "Backbone project" ulio
jengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
pamoja na Benki ya Maendeleo ya Africa.
Vituo vingine vilivyo karabariwa
katika mradi huu ni pamoja na kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha
Tagamenda kilchopo Mkoa wa Iringa, Kituo cha kupoza na kusambaza umeme
cha Singida pamoja na Kile cha Ibadakuli Shinyanga.
Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Waziri wa Nishati Mheshimiwa Subira
Mgalu, alimshukuru Dkt. Adesina pamoja na Uongozi wote wa Benki ya AfDB kwa kuipa kipaumbele miradi ya maendeleo ikiwepo miradi mikubwa ya
umeme ambapo Tanzania ni mmoja wa wanufaika wa miradi hiyo.
Kwa upande wake Waziri
wa Fedha Dkt. Philip Mpango alitoa shukrani kwa Benki ya Maendeleo ya
Afrika kwa ufadhili wa miradi mbali mbali ikiwemo ya umeme, Kilimo
,pamoja na miundombinu.
Dkt. Mpango alimhakikishia Rais wa Benki ya AfDB
kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Uongozi wa MheshimiwaRais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli itahakikisha fedha zote zinazotolewa na Benki hiyo zinatumika vema katika miradi iliyo lengwa ili kuhakikisha
kuwa Tanzania inapata maendeleo kupitia miradi hii kama ilivyo
tarajiwa.
Naye Mhandisi Peter Kigadye kwa niaba ya Mkurugenzi wa TANESCO
aliwahakikishia wageni wote kua kupitia mradi huo Mikoa ya Kanda ya
kati imekuwa na umeme wa uhakika pia kupitia mradi huo zaidi ya vijiji
121 vitanufaika kwa kupatiwa umeme kwa gharama nafuu ya shilingi 27,000
tu ,pia baadhi wa wakazi walio vunjiwa nyumba zao kupisha mradi
wamenufaika kwa kujengewa upya nyumba za kisasa kabisa , hii ni pamoja
na majengo ya taasisi mbali mbali kama makanisa zahanati shule pamoja na
misikiti iliyovunjwa kupisha mradi ilijengwa upya . Zaidi Mradi huu
umemaliza tatizo la umeme katika migodi iliyo kanda ya ziwa kwani kwa
sasa eneo lote la migodi hii linapata umeme wa uhakika na wa kutosha .