Nguzo ya HT laini ya 11KV M2 eneo la Sekei Arusha imeanguka. Mafundi wamefungua jumper.
Maeneo yanayoathirika ni Oligli, Bangata Star TV, Visima vya maji na Midawe.
Mafundi wameanza kazi ya kubadilisha nguzo
December 27, 2014
December 9, 2014
TAARIFA KWA WATEJA WA MAENEO YA UPANGA NA AZIKIWE
Shirika la
Umeme Tanesco linawatarifu wateja wake wa maeneo ya Upanga na mtaa wa
Azikiwe kuwa kumetokea shoti kubwa muda wa saa
11.30jioni baada ya Mkandarasi wa mradi wa Hifab kukata waya mkubwa wa
msongo wa kilovolti 11 na hivyo kusababisha Kituo cha Kupooza na
Kusambaza Umeme cha Mjini Kati (City Centre) kuzima ghafla. Mafundi wa
Karakana ya Umeme kutoka Makao Makuu wanashugulikia
tatizo na tunatarajia umeme utarudi kesho mchana baada ya kuunga waya
huo na kubadili vifaa vilivyoungua kwenye Kituo cha City Centre. Uongozi
unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza. Imetolewa na Ofisi ya
Uhusiano Tanesco Makao Makuu.
December 8, 2014
KATIZO LA UMEME – MKOA WA ILALA
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa
Wilaya ya Tabata kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama
ifuatavyo:-
TAREHE: Alhamisi 11, Disemba,
2014 na Jumatano 17 Disemba 2014
MUDA: Saa 03:00 Asubuhi hadi 11:00
jioni
SABABU: Kubadilisha nguzo zilizooza na kukata miti
iliyopita kwenye laini
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
11th December 2014
Segerea, Kinyerezi,
Bonyokwa, Kifuru, Bangulo na maeneo ya jirani.
17th December, 2014
Tabata kimanga, Kisukuru, Makoka,na maeneo ya jirani.
Tafadhali usiguse waya wowote uliokatika toa taarifa TANESCO kupitia
namba Kitengo cha dharura ilala: 022 213 3330, 0784 768586 au namba za huduma kwa wateja 2194400 au 0768
985 100 na Kitengo cha dharura Tabata 0684 001068, 0715768589
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote
utakaojitokeza.
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO
– MAKAO MAKUU.
December 7, 2014
TANGAZO KWA WATEJA WA MKOA WA ILALA
Shirika la Umeme Tanesco linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Ilala kuwa jana, saa 4 usiku kumetokea hitilafu ya dharura kwenye kituo chake cha kupooza umeme cha Ilala hivyo kusababisha ukosefu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya Kurasini, kigamboni, Mbagala, Changombe, Nyerere rd, Mafundi wa karakana ya umeme wanashugulikia tatizo na tunatarajia umeme utarudi saa 10:00 jioni leo.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
IMETOLEWA:
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
IMETOLEWA:
OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU
December 4, 2014
TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKOSEKANA KWA UMEME
KWA BAADHI YA MAENEO NCHINI
Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) linanapenda kutoa
ufafanuzi kwa wateja wake kuhusu sababu za kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya
maeneo nchini kwa nyakati tofauti kama ifuatavyo:-
Mosi, Kuanzia Novemba 26, 2014 hadi Desemba 1, 2014 Mikoa yote iliyoungwa
kwenye gridi ya taifa ilikuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo
kutokana na kuharibika kwa mashine moja ya Mtambo wa Kufua Umeme wa Kidatu yenye
uwezo wa kufua megawati 50. Mtambo huo kwa sasa umetengamaa na hakuna Mkoa
wenye upungufu wa umeme.
Pili, Novemba 29, 2014 Kulitokea hitilafu ya kulipuka na kuungua kwa
Kikata Umeme (Circuit Breaker) kwenye Kituo cha Kupooza na Kusambaza Umeme cha
Ubungo upande wa msongo wa kilovolti 33 na hivyo kusababisha gridi nzima ya
taifa kutoka saa 11.38jioni na kurejesha saa 3.03 usiku kwa mikoa yote baada ya
kutengeneza kifaa kilichoharibika. Hata
hivyo baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) yaliendelea kukosa
umeme kwa siku 2 mfululizo hadi tulipo funga Kikata Umeme kingine. Tatizo hilo
limesha patiwa ufumbuzi na Mkoa huo kwa sasa unapata umeme kama kawaida.
Tatu,
Kuanguka kwa
nguzo kwa baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam kutokana na kuanza kwa
kipindi cha mvua.
Nne, Matengenezo yanayoendelea ya ukarabati wa miundombinu kwa mikoa
yote ya nchini. Kazi zinazofanyika kwenye zoezi hilo kwa sasa ni kubadilisha
nguzo zilizooza, kunyanyua nguzo zilizoinama, kuvuta nyaya zilizolegea na kukata
miti inayogusa nyaya za umeme. Zoezi kama hili hufanyika kwa kila mkoa kwa nchi
nzima kama tahadhari kabla ya kuanza kwa kipindi cha masika ambacho kinaambatana
na mvua na upepo mkali.
Kwa sababu hii kubwa, kumekuwa na usumbufu
wa kukatwa kwa umeme kwa baadhi ya maeneo kwa nyakati tofauti kulingana na
ratiba ya mkoa husika ili kupisha zoezi hilo ambalo tunatarajia litakamilika
mwezi huu wa Desemba.
Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa
usumbufu wowote uliojitokeza.
Imetolewa
na
Ofisi
ya Uhusiano,
December 3, 2014
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUKOSEKANA KWA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linanapenda kutoa
ufafanuzi kwa wateja wake kuhusu kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo ya
jiji la Dar es Salaam kwa sababu mbalimbali kama ifuatavyo:-
Mosi, Kuanzia Novemba 26, 2014 hadi Desemba 1, 2014
Mikoa yote iliyoungwa kwenye gridi ya taifa ikiwemo Dar es Salaam ilikuwa na
upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo kutokana na kuharibika kwa mashine moja
ya Mtambo wa Kufua Umeme wa Kidatu yenye uwezo wa kufua megawati 50. Mtambo huo
kwa sasa umetengamaa na hakuna Mkoa wenye upungufu wa umeme.
Pili, Novemba 29, 2014 Kulitokea hitilafu ya
kuungua kwa Kikata Umeme (Circuit Breaker) kwenye Kituo cha Kupooza na
Kusambaza Umeme cha Ubungo upande wa msongo wa kilovolti 33 na hivyo
kusababisha baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Kinondoni Kusini (Magomeni) kukosa
umeme kwa siku 2 mfululizo. Tatizo hilo limeshapatiwa ufumbuzi na Mkoa huo kwa
sasa unapata umeme kama kawaida.
Tatu, Kuanguka
kwa nguzo kwa baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam kutokana na
kuanza kwa kipindi cha mvua.
Nne, Matengenezo yanayoendelea ya ukarabati wa
miundombinu kwa mikoa yote ya Dar es Salaam. TANESCO inaendesha zoezi la
ukarabati wa miundombinu yake kwa mikoa ya Kinondoni Kusini (Magomeni),
Kinondoni Kaskazini (Mikocheni), Ilala na Temeke. Kazi zinazofanyika kwenye
zoezi hilo kwa sasa ni kubadilisha nguzo zilizooza, kunyanyua nguzo
zilizoinama, kuvuta nyaya zilizolegea na kukata miti inayogusa nyaya za umeme.
Zoezi kama hili hufanyika kwa kila mkoa kwa nchi nzima kama tahadhari kabla ya
kuanza kwa kipindi cha masika ambacho kinaambatana na mvua na upepo mkali.
Kwa sababu
hii kubwa, kumekuwa na usumbufu wa kukatwa kwa umeme kwa baadhi ya maeneo mara
moja kwa siku ili kupisha zoezi hilo ambalo tunatarajia litakamilika mwezi huu
wa Desemba.
Uongozi wa
Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na
Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO MAKAO MAKUU.
Subscribe to:
Posts (Atom)