October 2, 2012


KUOMBA RADHI WILAYA YA KAHAMA

TANESCO inawaomba radhi wateja wake wa Wilaya ya Kahama kutokana na kukosa umeme kwa sababu ya matengenezo yanayofanywa katika njia ya umeme ya Wilaya hiyo ili kuboresha upatikanaji wa umeme.

Umeme umekatika saa 3:00 asubuhi na utarejea saa 10:00 jioni.

Uongozi unawaomba radhi wateja wote kutokana na usumbufu wanaoupata.

Imetolewa na;
OFISI YA MAWASILIANO
TANESCO MAKAO MAKUU



TANESCO Mpya Iweje

Wapendwa wateja wa TANESCO na wananchi wote kwa ujumla, Shirika la Umeme Tanzania TANESCO ni mali ya Umma kwa kuwa linamilikiwa na Serikali kwa asilimia 100. Hivyo TANESCO ni mali ya watanzania.
Kwa kulitambua hilo, Uongozi wa Shirika umeanzisha mchakato wa kufanya mabadiliko ya KIMUUNDO na KIUTENDAJI kwa Shirika, ili kuhakikisha kuwa TANESCO inatoa huduma zake kwa ufanisi zaidi na kwa matakwa ya wananchi na wateja wake.
Tunakaribisha maoni, ushauri, mapendekezo kutoka kwa wananchi, wateja wote wenye mapenzi mema na maendeleo ya TANESCO na nchi yetu kwa ujumla.
Tafadhali tutambue kuwa nia ya mchakato huu ni kujenga, hivyo tutoe maoni kwa nia njema.
Unaweza pia kutoa maoni yako kwa kupitia
tanesco.iweje@tanesco.co.tz,
communications.manager@tanesco.co.tz au facebook kwa kutafuta neno
‘tanesco iweje’au kwa kupiga simu namba +255222451185

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.