August 17, 2015

TAARIFA

TAARIFA YA KUKATIKA UMEME KWA BAADHI YA MAENEO YA JIJI LA
 DAR ES SAALAM.

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linawaatarifu wateja wake wa jiji la Dar es Salaam kuwa,kumetokea hitilafu ya kiufundi kwenye kituo kikuu cha kupooza na kusambaza umeme cha Ubungo upande wa msongo wa kilovoti 132 leo saa 3:30 asubuhi Agosti 17, 2015.

Kutokana na hitilafu hiyo baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Saalam yanakosa umeme.

Mafundi tayari wapo eneo la tukio na jitihada zinafanyika ili kurejesha umeme mapema iwezekananyo.

IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO
                                TANESCO MAKAO MAKUU