Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama
ifuatavyo:-
TAREHE: 30 Oktoba 2013 (Jumatano)
SAA: 3.00 asubuhi hadi saa 11.00
jioni.
SABABU: kubadilisha nguzo zilizooza na kukata miti iliyo chini ya laini za umeme
za TG3,TG4 na TG5
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:-
Wazo/Tanganyika Portland Cement, Salasala Magengeni, Bagamoyo
na Bunju, Bahari beach, Ununio, Ras Kilomoni, Budget hotel, Njia panda ya wazo
factory, Teget, Boko, Boko Maliasili, Boko National Housing, Ndege beach, Mbweni
Kijijini, nyumba 151 za Serikali, Bakili Muluzi school, Mbweni Ofisi ya Raisi
flats, Marando street. Kunduchi yote, Kunduchi Recruitment Training School (RTS)
of TPDF, Mbuyuni, MECCO, JKT machimbo, baadhi ya maeneo ya Salasala, Shule ya Green
Acres, Baadhi ya maeneo ya Kilongawima, Mbezi Africana, Mbezi Majumba sita, Lugalo
Salasala, Kinzudi na maeneo yanayozunguka.
Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo
2700367, 0716 768584 na 0784 768584, kituo cha miito ya simu namba 2194400.
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO – MAKAO