NA Mwandishi wetu
MRADI
wa Umeme wa Kenya-Tanzania Power Interconnection
(KTIPIP) ZTK tayari umeanza kutekelezwa ambapo kazi ya kutengeneza
misingi ya kusimika minara (towers) imeanza.
Mratibu wa Mradi huo Mhandisi Peter Kigadye aliwaambia Wahariri wa Vyombo vya Habari waliotembelea kambi ya Wakandarasi iliyoko Kijiji cha Nanja kilichoko barabara ya Bababti-Arusha Wilayani Munduli Januari 22, 2019.

Mradi
huo ni sehemu moja ya mradi mzima wa Regional Power Connection ambao lengo lake ni kuunganisha Mfumo wa Umeme wa Tanzania
na Afrika Mashariki (East Africa Power Pool) kwa upande wa Kaskazini, na
baadaye utekelezaji wa sehemu nyingine ya tatu ambayo itakuwa inaunganisha
mifumo ya nchi Kusini mwa Afrika, kupitia chombo kinachoitwa Southern Africa
Power Pool (SAPP)
“Tanzaania
tumebarikiwa tutakuwa na sehemu tatu, sehemu ya kwanza ni mradi wa Backborn ambao
umejengwa katikati ya nchi yetu, ulikuwa na kilometa 670 ambao unaanzia Iringa
hadi Shinyanga, sehemu ya pili ni kuunga kutoka Singida hadi mpakani na Kenya kuna
kituo kimoja kinaitwa Isinya, jumla hapo kuna kilometa 510.7 na hizo ndio
kilomita za mradi tunazoanza kuutekeleza hivi sasa.” Alisema Mhandisi Kigadye.
Aliongeza kuwa sehemu ya tatu ni kuanzia Iringa kwenda Kusini ambapo kuna mradi utakaoitwa Zambia Interconector ambao una kilometa 624 na kusema Tanzania itakuwa imekamilisha msongo wa kilovoti 400
Aidha, Mhandisi Kigadye alisema kuhusu kuunganiushwa kwa umeme kwenye nchi za Ukanda wa Mashariki na Kusini lengo ni kuunganisha nchi yetu na nchi za Kikanda kuanzia Kaskazini kuungana na Kenya na Kusini kuungana na Zambia.

Alisema
mradi wa Kenya-Tanzania Power Interconnection
(KTIPIP)ZTK, utakamilika Aprili 2020, wakati ule Zambia Connector unatarajiwa kukamilika utakamilika
mwaka 2022.
"Tutakuwa tumemaliza mikongo hii mitatu (3)na nchi yetu itakuwa tayari kushiriki kwenye biashara ya umeme Kikanda", aliongeza Mhandisi Kigadye.
"Tutakuwa tumemaliza mikongo hii mitatu (3)na nchi yetu itakuwa tayari kushiriki kwenye biashara ya umeme Kikanda", aliongeza Mhandisi Kigadye.
Akifafanua
zaidi kuhusu mradi huo wa Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK alisema sehemu ya kwanza itahusu ujenzi wa njia za kusafirisha umeme
(transmission lines) na ujenzi wa vituo vya kupozea umeme.
Mradi
mzima una urefu wa kilometa 510 na umegawanyika kwenye sehemu nne, ambazo ni
Isinya Kenya hadi Namanga Kilometa kilomita 96, sehemu ya pili unahusu
Namanga - Arusha Kilometa 114, sehemu ya tatu Arusha-Babati kilometa 150, na
Bababti-Singida kilometa 150.
Kwa
upande wake, Mhandisi
Emmanuel Manirabona ambaye ni Meneja Mwandamizi Miradi, alisema tayari vifaa vya kutekeleza ujenzi wa mradi huo
vimewasili kwa kiasi kikubwa cha kazi imeshaanza.
Akieleza
zaidi Mhandisi Manirabona alibainisha kuwa kila kitu kiko sawa na Wananchi wote
ambao wako kwenye sehemu mradi unakopita, tayari Serikali imeshawalipa fidia na
ndiyo maana Mkandarasi anaendelea na kazi.
Meneja Mwandamizi Miradi Miradi, Mhandisi
Emmanuel Manirabona, akifafanua mambo mbalimbali yahusuyo utekelezaji wa mradi huo.
Mratibu wa Mradi huo, Mhandisi Peter Kigadye, akifafanua jambo kwa wahariri eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha.
Vifaa viko site tayari
Vifaa viko site tayari
Zege linamwaga kwenye msingi wa kusimika mnara wa kupitisha nyaya za umeme mkubwa
Eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kisongo.
Mhandisi Peter Kigadye
Mhandisi Peter Kigadye
Meneja Mwandamizi Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona (kushoto), akiwa na Meneja Mkazi, Mradi wa Kenya-Tanzania Interconnection Project-Lot2 SBU Power Bouygues ya Ufaransa, Christophe Batholome
Mhandisi Mshauri Mradi wa umeme wa Kenya-Tanzania Interconnection-Lot2(KTPIP-Lot2), Gilles Allard kutoka kampuni ya Intec
Mhariri wa gazeti la Majira, Bw. Imma Mbuguni akizungumza jambo.
Mashimo manne ya nguzo nne za mnara (tower) moja. mafundi wanasubiri kumwaga zegu.
Mafundi wakiwa wamesimama mbele ya moja ya shimo litakalotumika kusimika mnara (tower). Kwa kawaida Mnara mmoja nashikiliwa na nguzo nne, hili shimo ni la kusimika nguzo moja kati ya hizo.
Mhandisi Kigadye akifafanua jambo eneo la uchimbaji na usimikazji minara ambapo kazi ya kumimina zege kwenye mashimo imeanza
Waandishi na wahariri wakinukuu taarifa muhimu eneo la utendaji huko wilayani Monduli.
Mafundi wakiwa kazini.
Vifaa viko site tayari
Vifaa viko site tayari
Zege linamwaga kwenye msingi wa kusimika mnara wa kupitisha nyaya za umeme mkubwa
Eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Kisongo.
Meneja Mwandamizi Miradi, Mhandisi
Emmanuel Manirabona (kushoto), akimsikiliza Mhandisi Mshauri Mradi wa umeme wa Kenya-Tanzania Interconnection-Lot2(KTPIP-Lot2), Gilles Allard kutoka Kampuni ya Intec, kwenye eneo la ujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme kinachojengwa eneo la Kisongo nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Mhandisi Herini Mhina. Meneja wa TANESCO jijini Arusha. Mhandisi Peter Kigadye
Mhandisi Peter Kigadye
Meneja Mwandamizi Miradi, Mhandisi Emmanuel G. Manirabona (kushoto), akiwa na Meneja Mkazi, Mradi wa Kenya-Tanzania Interconnection Project-Lot2 SBU Power Bouygues ya Ufaransa, Christophe Batholome
Mhandisi Mshauri Mradi wa umeme wa Kenya-Tanzania Interconnection-Lot2(KTPIP-Lot2), Gilles Allard kutoka kampuni ya Intec
Mhariri wa gazeti la Majira, Bw. Imma Mbuguni akizungumza jambo.
Meneja Mkazi, Mradi wa Kenya-Tanzania
Interconnection Project-Lot2 SBU Power Bouygues ya Ufaransa, Christophe Batholome(kulia), akibadilishana mawazo na Meneja wa TANESCO jijini Arusha, Mhandisi Herini Mhina, (katikati) na Msimamizi wa ujenzi kutoka Tanesco.