November 26, 2010

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuwaomba radhi wateja wake na wananchi kwa ujumla kutokana na kukosekana kwa umeme katika baadhi ya maeneo nchini kutokana na kuharibika kwa baadhi ya mitambo jana asubuhi Jumanne Novemba 23, 2010.
Bila kutarajia baadhi ya mashine katika mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi wa Ubungo, Songas na Kidatu  zilipata hitilafu ya kiufundi na kusababisha umeme uliozalishwa kutotosheleza mahitaji.
Upungufu huo ulisababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme kuanzia asubuhi saa nne hadi saa nne usiku kwa tarehe iliyotajwa hapo juu.
Hata hivyo, Shirika linaendelea na juhudi za kutatua hali hiyo ili kusiwepo na mgawo wa umeme.
Miongoni mwa jitihada zinazofanywa ni pamoja na kutumia mitambo yote ya kuzalisha umeme iliyopo kwa kiwango cha juu.
Wakati huo huo Shirika linapenda kuwatoa hofu wateja wote wa umeme wanaotumia LUKU kwamba hakuna tatizo la upatikanaji wa huduma hiyo isipokuwa kuna baadhi ya vituo vya LUKU ambavyo vimeishiwa na LUKU na badala yake wamekuwa wakisingizia au kuhusisha tatizo hilo na mtandao wa shirika.
Ifuatayo ni ratiba ya mgawo wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam kutokana na kuharibika kwa transfoma kubwa katika eneo la Kipawa.

Saa 12 asubuhi – 8 mchana :-
Maeneo yatakayoathirika,
SEGEREA, KINYEREZI, BANGULO, TANDIKA YOTE, TEMEKE, MTONI MASHINE YA MAJI, YOMBO VITUKA, YOMBO BUZA, YOMBO KILAKALA, MBAGALA KILUNGULE, MAENEO YA VIWANDA  YA VINGUNGUTI, KARAKATA, BANANA, KIPUNGUNI, KIVULE, KITUNDA NA MWANAGATI, AIRPORT TERMINAL ONE, AIR WING AND AIR BP

Saa 8 mchana – 4 usiku
Maeneo yatakayoathirika,
MAENEO YA CHANG'OMBE, TEMEKE MTAA WA YOMBO, KEKO TOROLI , NYERERE ROAD KUNZIA BARABARA YA KAWAWA MPAKA TAZARA NA VINGUNGUTI NA KIWALANI YOTE
Saa 4 Usiku – 12 Asubuhi
Maeneo yatakayoathirika,
SEGEREA, KINYEREZI, BANGULO, TANDIKA YOTE, TEMEKE, MTONI MASHINE YA MAJI, YOMBO VITUKA, YOMBO BUZA, YOMBO KILAKALA, MBAGALA KILUNGULE,MAENEO YA VIWANDA  YA  VINGUNGUTI, KARAKATA, BANANA, KIPUNGUNI, KIVULE, KITUNDA NA MWANAGATIAIRPORT TERMINAL ONE, AIR WING AND AIR BP.
Transfoma ya kituo cha kusambazia umeme cha Kipawa ya uwezo wa MVA 45 iliharibika Jumamosi saa 10:23 jioni na kusababisha baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam kukosa umeme.


Badra Masoud,
MENEJA MAWASILIANO.

3 comments:

  1. sisi wakazi wa toangoma tunauliza ni lini mtasambaza miundo mbinu ya umeme sehemu zote? tunashangaa kuona nguzo za umeme ziliingilia barabara ya machimbo ya pili na kuishia kwenye nyumba moja( ),tunahoji nini kifanyike ili nasi tuliombele ya nyumba hiyo tupate umeme?kwani viwanja hivi vya mradi vinastahili kupata umeme

    ReplyDelete
  2. Tanesco,tanesco,hebu waangalieni wenzenu posta na simu,siku za nyuma ilikuwa issue tata kupata simu ya mezani,mara mambo yakabadilika makampuni kibao ya simu za mkononi yakaingia sokoni,watu wakahama gafla kama nyuki mwaaaaa wengine voda,airtel,nk.Leo nani anawafata watu wa posta na simu tena?hata nyie wote mnasimu za mkononi ,jifunzeni kwa hawa muache nyodo,toeni huduma kwa watu hata kama baadaye kukitokea upinzani watu watupe jongoo ila wabaki na mti wake.

    ReplyDelete
  3. Nikipita barabara za katikati ya mji hasa ile itokayo airport,Ali hasan,kumewekwa nguzo zenye taa za barabarani,ukweli panapendeza na pana ongeza hali ya usalama.Ninashangaa kuona barabara zingine hazijawekewa taa,umeme upo lakini barabara zote za giza ,vibaka wanatumia sana mwanya huo kufanya uharifu.Ukitembelea barabara ya kilwa hasa mbagala mpaka kigamboni ni giza nene ,je ni lini hizi barabara zitawekewa taa ili nasi watu kama wa mbagala tuweze hata kuyaona hayo majalala mbele ya nyumba zetu na mitaa yetu ili tusije kanyaga nyoka na vinyesi tukafa kabla ya siku zetu?

    ReplyDelete