Kasi ya ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere
(JNHPP) kwenye Mto Rufiji Mkoani Pwani “imemkuna” Waziri wa Nishati Dkt. Medard
Kalemani baada ya kutembelea eneo la mradi huo Septemba 8, 2019 na kukuta hatua
muhimu ya ujenzi wa ADIT (njia ya kufika kwenye handaki la kuchepusha maji) (diversion
tunnel) ikiwa imekamilika.
“Hii ni mara yangu ya nane kutembeela mradi huu tangu
uanze, leo nimetembelea ili kuangalia masuala makubwa matatu, kasi ya ujenzi,
usimamizi na utawala na masuala yote ya ujenzi wa miundombinu wezeshi ili kuona
kama imekaa sawasawa.” Alisema Dkt. Kalemani.
Alisema baada ya kuangalia masuala hayo amefurahishwa na
hatua iliyofikiwa ambapo amewapongeza wasimamizi wa mradi huo TANESCO na
TANROADS ambao Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
alitoa maelekezo kuwa lazima ujenzi huo usimamiwe na Watanzania wenyewe na
ukamilike katika muda uliopangwa ambao ni miezi 42, ambapo miezi 36 ni ya
ujenzi na miezi 6 ya mobilization kwa maana ya maandalizi ya vifaa na watumishi
ambapo kazi ilianza Juni 15, 2019 na kazi inakwenda vizuri.” Alifafanmua Dkt.
Kalemani.
Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema hadi sasa tayari
wakandarasi wamekwishatumia miezi nane 8 kati ya 42 na kazi ambazpo zilikuwa
zinaendelea kufanyika ni ujenzi wa njia za kuchepusha maji (diversion tunnel),
nilikuja Julai 22, 2019 na nikaelekeza kazi hii ifanyike ndani ya siku 45 na
ikamilike umbali wa Mita147.6 nashukuru wamemaliza na wameokoa siku 7 kabla ya
muda niliotoa.
“Nimatarajio yetu mkataba unaisha Juni 14, 2022 na
nimatumaini yetu kwamba watatukabidhi mradi huo siku hiyo saa 9;30 alasiri
wataukab idhi na mimi niukabidhi kwa Watanzania na asitokee mtu atakaejaribu
kuuchelkewesha mradi huo, sisi kama serikali tutahakikisha tunaanza kumchelewesha
yeye kwanza kabla hajatuchelewesha sisi kukamilisha mradi huo.” Alionya.
Awali akitoa taarifa ya mafanikio ya utekelezaji wa mradi
huo yaliyofikiwa hadi sasa, Mratibu wa Mradi huo Mhandisi Steven Manda ambaye
pia ni Meneja Miradi wa TANESCO alisema, pamoja na kukamilika kwa ujenzi wa
handaki la kuchepusha maji, pia daraja namba mbili kwa maana ya miundombinu
wezeshi nalo limekamilika na sasa mashine kubwa na vifaa vya ujenzi vinavushwa
kutoka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kupitia daraja hilo.
Daraja namba mbili la kukatisha mto Rufiji eneo la ujenzi wa mradi wa umeme wa maji wa Julius Nyerere (JNHPP) likiwa limekamilika. |
No comments:
Post a Comment