Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na TANESCO, leo Mei
26,2021, imeingia makubaliano ya mkopo wa Dola milioni 140 kutoka Benki
ya Maendeleo ya Africa (ADB) kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa kufua
umeme wa megawati 49.5 kupitia maporomoko ya maji ya Mto Malagarasi
uliopo Mkoani Kigoma.
Mradi wa Maragalasi utachochea ukuwaji wa shughuli za maendeleo ya
kijamii pamoja na kiuchumi kwa wakazi wa Mikoa ya Kaskazini Mashariki
mwa Tanzania.
Mradi huu, utahusisha pia uimarishaji gridi ya Taifa itakayorahisisha
biashara ya mauziano ya Nishati ya umeme baina ya Tanzania na Nchi
majirani.
Aidha gharama za mradi huo kwa ujumla ni takriban Dola milioni 144.14,
ambapo Serikali ya Tanzania itachangia kiwango kinachobakia cha Dola
milioni 4.14 kukamilisha fedha za Ujenzi wa Mradi huo muhimu kwa Mikoa
ya ukanda wa Kaskazini Mashariki na Tanzania kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment