Jana majira ya saa 1.19 usiku gridi ya taifa ilitoka na
hivyo kusabisha nchi nzima kikosa umeme. Umeme ulirejeshwa kwa nchi
nzima saa 4:48 usiku baada ya kuwasha mashine zote bila tatizo
kuonekana.Kutoka kwa gridi ya taifa kuna sababu mbili kuu: Moja kama kukitokea
hitilafu , mmoja wa mitambo yetu ya kuzalisha umeme mfano: Kidatu,
Mtera, Kihansi, Hale, New Pangani, Nyumba ya Mungu, Ubungo 1&2 au
Tegeta gridi inaweza kutoka. Yaani kwa lugha rahisi ni kwamba mitambo
yote ya kuzalisha umeme inabeba mzigo mmoja. Kama mtambo mmoja ukitoka,
unasababisha ombwe (vacancy) ambapo mitambo inayobaki inashindwa kuubeba
na hivyo nayo kuachia mzigo na hatimaye mashine zote hutoka (huzima).
Sababu ya pili mitambo ya wateja wetu wakubwa kama vile, migodi na
viwanda vikubwa vya uzalishaji, wateja hao wakubwa mitambo yao ikipata
hitilafu na kuzima ghafla, inaweza kusababisha mfumo wa gridi kutoka kwa
mtindo huo huo wa kuzidiwa kwa mzigo kwa mitambo yetu. Hivyo baada ya
gridi kutoka mafundi kwenye vituo vyetu wakishirikiana na kituo cha
kudhibiti mifumo ya gridi waliweza kuwasha mashine zote salama na umeme
kurejeshwa nchi nzima saa 4.48. Kwa hivyo mpaka sasa bado tunafanyia
kazi taarifa/data zilizorekodiwa na Kituo cha kudhibiti mifumo cha
Ubungo ilikujua haswa chanzo cha kutoka kwa gridi jana usiku. Kitendo
cha jana tutkichukulia kua ni dharura na ghafla (emergency) ni nadra
sana kutokea gridi yote kutoka.
Kwa nchi za wenzetu gridi haiwezi kutoka kwa kuwa wanazalisha umeme wa
ziada (spinning reserve) kwa kuwa wanazalisha umeme kwa njia kama ya
makaa ya mawe ambao ukishauwasha huwezi kuuzima, hivyo wanaumeme ambao
uko standby, ukipungua tu kwenye gridi basi spinning reserve inaziba
hilo ombwe.
Adrian Severin - Kaimu Meneja Uhusiano Tanesco
No comments:
Post a Comment