TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UPOTOSHAJI WA GAZETI LA MTANZANIA
Gazeti
la Mtanzania la Mei 30, 2014 toleo namba 7476 lilichapisha taarifa
yenye kichwa cha habari “ Vigogo TANESCO wadaiwa kutafuna Sh milioni
408” kwenye ukurasa wa tisa na gazeti hilo hilo la Juni 4, 2014 toleo
namba 7481 lilichapisha tena mwendelezo wa taarifa hiyo ikiwa na kichwa
cha habari “Vigogo TANESCO watoa vitisho”.
Taarifa
hiyo inalishutumu Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuwa limekumbwa
na kashfa nyingine kwa madai kwamba viongozi kadhaa wa Shirika wamekula
kiasi hicho cha fedha, ambazo
ni posho za wafanyakazi 36 kutoka mkoa wa Dar es Salaam.
Uongozi wa TANESCO unakanusha vikali taarifa hizo na kwamba hazina ukweli wowote.
Kwanza
taarifa hiyo inamakosa mengi ya kiuandishi. TANESCO ina makubaliano
na Shiririka la Maendeleo la Watu wa Japani (JICA) kuwafundisha
wafanyakazi wake kwenye mpango ujulikanao kama ““Capacity Development of
Efficient Distribution and Transmission Systems” yaliyosainiwa mwaka
2009. Hakuna Kampuni inayoitwa
Jaica inayofanyakazi na Shirika kama mwandishi alivyoandika kwenye habari zake zote mbili.
Pili
katika
makubaliano hayo, JICA wanachangia wataalamu na vifaa vya kufundishia
kwa njia ya vitendo na nadharia wakati TANESCO walichangia ujenzi wa
majengo na wanaendelea kulipia
posho za wafanyakazi wanafunzi katika vyuo vyake viwili vilivyopo
jijini Dar es Salaam eneo la Masaki na Stesheni.
Wanaofundishwa
chini ya mradi huu ni wafanyakazi ambao ni mafundi yaani mafundi
sadifu, mafundi mchundo na wahandisi. Mradi huu ambao unafundishwa kwa
pamoja na wataalamu kutoka
TANESCO na JICA (Japan) unategemewa kukamilika Agosti mwaka huu na
baadae, TANESCO wataendelea kutoa mafunzo hayo kwa mtindo ambao
wameuanzisha pamoja na JICA.
Tatu,
mapungufu ya taarifa hiyo
Mwandishi
wa taarifa hiyo alikuwa na ufahamu mdogo wa mpango wenyewe. Ukweli ni
kwamba Mradi una taratibu mbili za ufundishwaji. Kundi la kwanza ni
ufundishaji wa wafanyakazi wanaopewa
mafunzo ya darasani kwa nadharia na kwa vitendo ndani ya maeneo ya Chuo
na wamatoka mikoani. Kundi ya pili ni wafanyakazi mafundi wanaopewa
mafunzo ya vitendo tu kwenye miundombinu ya Shirika iliyopo baada ya
kumaliza mafunzo ya awali kwenye maeneo ya Chuo.
Mafunzo haya yanajulikana kama ‘On Job Training’ (OJT).
Wafanyakazi
wanaodaiwa kulalamika ni wanaofanya mafunzo kwa vitendo wakati wakiwa
kazini (OJT) nje ya Chuo na wamepewa kazi ya kuboresha miundombinu ya
umeme katika jiji la Dar es
Salaam na wanatoka mikoa ya Kinondoni Kaskazini (Mikocheni), Kinondoni
Kusini (Magomeni) na Kituo cha Karabati Umeme Dar es Salaam (KAUDA).
Mradi
wa kuboresha miundombinu kwa mkoa wa Dar es Salaam ili kuondokana na
kukatika katika kwa umeme ulianza mwaka 2009 kwa ushirikiano kati ya
JICA na TANESCO nia ya mpango huu
ilikuwa ni kujenga uelewa wa kiufundi zaidi baada ya mafunzo ya
darasani ambapo mafundi hupelekwa maeneo yao ya kazi kufanyakazi kwa
vitendo.
Nne,
Utaratibu wa Shirika
Kulingana
na taratibu za Shirika na Sheria za kazi, TANESCO hutoa posho ya siku
kwa wafanyakazi wanaohudhuria mafunzo ya darasani yakiandamana na
vitendo vinavyofanywa ndani ya eneo
la Chuo Masaki. Lakini hawa wafanyakazi wanaolalamika kwa mujibu wa
kumbukumbu za Shirika hawatambuliki kama wanafunzi tena. Walishamaliza
mafunzo ya darasani na ya vitendo katika eneo la Chuo lilipo Masaki
jijini Dar es Salaam na wakalipwa posho kwa mujibu
wa taratibu na sasa wapo mitaani wanatekeleza yale waliyojifunza
darasani. Hawa ni wafanyakazi kama wafanyakazi wengine na wanapokea
misharara yao na marupurupu mengine yote kila mwisho wa mwezi.
Kwa
jinsi Shirika linavyowajali na kutambua kazi wanayoifanya, licha ya
mishahara yao na marupurupu mengine, wakati huu wanapofanya kazi kwa
vitendo wakati wapo kazini (OJT) kwenye
Mpango huo maalum wa kuboresha mifumo ya usambazaji umeme kwa jiji la
Dar es Salaam, wanalipwa kiasi cha fedha kama motisha kutoka kwenye
vituo vyao vya kazi kwa kupimwa kupitia malengo waliyoyafikia kwenye
(OJT).
Tano,
mwendelezo wa habari hiyo
Kama
vile haitoshi, gazeti hilo limeiendeleza habari hiyo kama vile ina
ukweli wowote na mbaya zaidi gazeti hilo halijafanya jitihada zozote za
kutafuta ukweli kutoka TANESCO. Aidha
linadai kuwa wafanyakazi hao wanatishiwa, sababu ambayo haina msingi
wowote.
Mwisho.
Uongozi wa Shirika umesikitishwa kwa taarifa hizo ambazo zimechafua
taswira ya Shirika na linautaka uongozi wa Gazeti la Mtanzania kwa
ajili ya kuendeleza Uhusiano mzuri uliopo baina ya Shirika na vyombo vya
habari kukanusha taarifa hizo kwenye gazeti hilo hilo na kuuomba radhi
uongozi wa TANESCO kwa udhalilishaji ambao umepotosha
umma.
Imetolewa na: Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment