Kabla ya matengenezo kuanza mnamo Januari 2019
Kituo hiki cha kupoza umeme cha Ubungo kimekuwa kinapokea umeme kutoka katika
vituo vya Uzalishaji umeme vilivyopo upande wa msongo wa kilovolti 220 kupitia transfoma mbili zenye uwezo wa MVA 150 kila moja, zenye kupokea umeme wa msongo wa Kilovolti 220 na kuushusha hadi kuwa msongo wa Kilovolti
132 katika transforma namba sita na namba saba za kituo cha Ubungo
na vituo vya
uzalishaji umeme vilivyoungwa kwenye msongo wa kilovolti 132 ambavyo
vimeungwa moja kwa moja kwenye mfumo mkuu wa usambazaji umeme kwa Dar es Salaam na Zanzibar.
Kutokana na matengenezo yanayoendelea
vituo vya uzalishaji umeme vilivyoungwa kwenye msongo wa kilovoti 132 na 33
vimekuwa nguzo kubwa ya upatikanaji wa umeme. Vituo hivyo ni Ubungo II na
Tegeta.
Shirika kupitia wataalamu wake tayari limefanya jitihada
kubwa za kupunguza athari za upungufu wa upatikanaji wa umeme kwa wakaazi wa Dar
es salaam na Zanzibar kwa kufanya yafuatayo:
Mosi, Kufungua laini
ya msongo wa kilovoti 132 kati ya Kilimanjaro na Hale: Hili hufanyika ili
kutoruhusu umeme wa kutoka Dar es Salaam na Morogoro kwenda Kilimanjaro hivyo Mkoa
huu kuchukulia kwenye upande wa msongo wa kilovolti 220 kutoka Arusha.
Pili , Kuwezesha upatikanaji wa umeme
katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Dar
es salaam, kwa kuunga baadhi ya njia za Usafirishaji umeme kutoka Kituo cha Kinyerezi, Gongolamboto
hadi Mbagala ili kuwezesha maeneo hayo kupata umeme bila kupitia kituo cha Ubungo
ambacho kipo katika matengenezo.
Tatu, Kufungua njia ya umeme ya kilovolti
132 itokayo Kituo cha Kunduchi hadi Mlandizi na kuunga maeneo hayo katika
njia ya umeme ya kilovolti 132 itokayo Morogoro ili kuwezesha jiji la Dar es salaam
kuwa na umeme wa uhakika.
Nne, Kufungua laini
ya msongo wa kilovolti 132 kati ya Ubungo na Chalinze upande wa Ubungo ili
kutozihusisha transfoma za Ubungo kwenye mzigo wa mikoa mingine na hivyo
kutumika kuhudumia wateja wa Dar es Salaam na Zanzibar pekee.
Tunatarajia matengenezo haya yanayokwenda kwa awamu
yatakamilika ifikapo mwezi Juni 2019.
TANESCO
itaendelea kutoa taarifa ya Maendeleo ya kazi ya matengenezo ya kituo cha
Ubungo yenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika Dar es salaam na
Zanzibar kwa siku zijazo.
Imetolewa na: Ofisi
ya Uhusiano
TANESCO-Makao Makuu
No comments:
Post a Comment