December 9, 2010

Kakakuona aonekana TANESCO Mtera

Mnyama ambaye huonekana kwa nadra Kakakuona ameonekana katika kituo cha kuzalisha umeme wa maji  cha Mtera kinachoendeshwa na Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania TANESCO. Wakazi wa eneo hili walijumuika kufanya tambiko kama ilivyo kawaida ambapo mnyama huyo hutakiwa kutoa utabiri. Kwa mujibu wa Mzee Magomba ambaye ni mmoja wa wazee walioongoza tambiko hilo alisema ni muda mrefu tangu Kakakuona alipoonekana eneo hilo hivyo wanategemea neema kubwa. Baada ya kumaliza tambiko Kakakuona aliruhusiwa kuondoka.

Mzee Magomba akimpaka mafuta na maji Kakakuona kama ishara ya kumuonyesha upendo

Mzee Magomba akihojiwa na vyombo vya habari vilivyofika eneo hilo

1 comment:

  1. Wakazi wa viwanja vya mradi Bunju BDecember 23, 2010 at 5:26 AM

    Wakazi wa viwanja vya mradi Bunju B said...

    Bunju B viwanja vya mradi tuna shida ya umeme, tuelezeni tufanye nini zaidi ya maombi ya umeme ili tuwe na mwanga usiku.
    Hela zakulipia gharama tunazo, hela za luku tunazo, sasa kazi kwenu mtuongeze kwenye "customer base" yenu, ambayo ndio msingi wa biashara yenu.
    Kazi kwenu TANESCO.

    ReplyDelete