December 17, 2010

Kishoka mwingine mikononi mwa polisi

Kishoka Abdallah baada ya kukamatwa



Afisa Usalama Mkoa wa Kinondoni Kusini Bw. Lugazia Cyprian alifanikiwa kumtia mbaroni kishoka Jidah Abdallah akiwa na mfuko wenye sare (koti la mafundi wa TANESCO) na viatu vya kupandia nguzo vyote vikiwa mali ya TANESCO.

Kishoka huyo alikamatwa baada ya purukushani nzito na kufuatiliwa kwa takribani saa nzima hadi maeneo ya Ubungo NBC alipotiwa mikononi mwa Polisi. Kishoka huyo yupo rumande kituo cha Polisi Kati kwa jalada namba CD/RB 15840/2010 na CD/IR/4655/2010 akisubiri kupelekwa mahakamani

1 comment:

  1. Wakazi wa viwanja vya mradi Bunju BDecember 23, 2010 at 5:28 AM

    Wakazi wa viwanja vya mradi Bunju B said...

    Bunju B viwanja vya mradi tuna shida ya umeme, tuelezeni tufanye nini zaidi ya maombi ya umeme ili tuwe na mwanga usiku.
    Hela zakulipia gharama tunazo, hela za luku tunazo, sasa kazi kwenu mtuongeze kwenye "customer base" yenu, ambayo ndio msingi wa biashara yenu.
    Kazi kwenu TANESCO.

    ReplyDelete