KATIZO LA UMEME –
MKOA WA KINONDONI KASKAZINI
Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) linawatarifu
wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa na katizo la umeme
kama ifuatavyo:-
TAREHE: 7 Septemba, 2016 (JUMATANO)
MUDA: 3:00
Asubuhi hadi 10:00 Jioni
SABABU:
Kuzimwa kwa laini ya Bahari Beach (BB1), kwa ajili ya
kubadili nguzo zilizooza na nyaya zilizochakaa ili kuboresha hali ya
upatikanaji wa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Baadhi ya maeneo ya Kondo
village, Bahari beach, Ununio, Rasi Kilomoni, Bulget Hotel, Chumvini, Mbweni pamoja na maeneo ya jirani.
TAREHE: 8 Septemba, 2016.
(ALHAMISI)
MUDA: 3:00
Asubuhi hadi 10:00 Jioni
SABABU: Kuzimwa
kwa kituo cha kupoza umeme cha MASAKI
kwa ajili ya kuhamisha laini ya msongo wa 11KV na kupisha ujenzi wa
laini mpya ya msongo wa 33KV ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Eneo lote la Masaki, Msasani, Oysterbay pamoja na
maeneo ya jirani.
Tafadhali usishike
waya uliokatika, toa taarifa kupitia
namba za simu zifuatazo: - Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784
768584, 0716 768584 au Kituo cha miito ya simu 022 2194400 / 0768 985 100.
Uongozi
unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na :
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO - MAKAO MAKUU.
No comments:
Post a Comment