KUANZIA SEPTEMBA
MOSI MWAKA HUU, SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO) LITAANZISHA OPERESHENI
KABAMBE NA ENDELEVU YA KUKUSANYA MADENI YA WADAIWA WAKE WOTE KWA NCHI NZIMA.
UONGOZI WA SHIRIKA UNATOA MUDA WA SIKU 10 HADI AGOSTI 31, 2014 KWA WATEJA WAKE WOTE
BINAFSI NA TAASISI ZOTE ZA SERIKALI AMBAO HAWAJALIPIA ANKARA ZAO ZA UMEME
KWENDA KULIPIA HARAKA IWEZEKANAVYO. BAADA YA MUDA HUO KWISHA, HUDUMA YA UMEME
ITASITISHWA BILA TAARIFA ZAIDI.
OFISI ZA TANESCO ZITAKUWA WAZI SIKU ZA JUMAMOSI NA
JUMAPILI ZA TAREHE 23, 24, 30 NA 31 ILI KUTOA NAFASI ZAIDI KWA WADAIWA WOTE
KULIPIA ANKARA ZAO.
UONGOZI UNASISITIZA KUWA ZOEZI HILI LINAHUSU WATEJA
WAKE WOTE, WATU BINAFSI NA TAASISI ZA SERIKALI.
KUEPUKA USUMBUFU, KALIPIE BILI YAKO SASA.
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA
MKURUGENZI MTENDAJI,
TANESCO
MAKAO MAKUU.
No comments:
Post a Comment