Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linaomba radhi wateja
wake wote wa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Shinyanga, Mwanza na Manyara
kwa kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti siku ya Jumapili na Jumatatu
Septemba 21 na 22, 2014.
SABABU za kukosekana kwa umeme kwa baadhi ya maeneo katika
mikoa hiyo, ilikuwa ni hitilafu kwenye mashine mbili za kufua umeme katika
Kituo cha Pangani na hitilafu kenye njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa
kilovolti 132 kutoka Chalinze hadi Hale.
Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote
uliojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya
Uhusiano,
TANESCO
Makao Makuu.
No comments:
Post a Comment