UONGOZI wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),
unapenda kuutaarifu umma kuwa Bw. Tom Mwaisupule (pichani juu) aliyekuwa mwajiriwa
wake Mkoa wa Temeke kama Fundi Umeme (Linesman), si mwajiriwa tena wa TANESCO
kuanzia Agosti 19, 2014.
Kwa
sababu hiyo, Shirika linatoa tahadhari kuwa
halitahusika na kazi au makubaliano yoyote yatakayofanywa na Bw. Tom Mwaisupule
kwa niaba ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Imetolewa
na: Ofisi ya Uhusiano,
TANESCO - Makao
Makuu.
No comments:
Post a Comment