Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) linawatarifu
wateja wake wa Mkoa wa Arusha kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.
Watakosa umeme
kwa siku za Jumamosi Agosti 21, Jumapili
Agosti 22, na Jumanee Agosti 23
SABABU: Kuzimwa kwa kituo cha
kupooza na kusambaza kusambaza umeme cha Mount Meru na laini ya 66kV ili
kupisha Mkandarasi (TEDAP) kuunganisha njia mpya ya umeme kwenye kituo cha
kupooza na kusambaza umeme cha Njiro.
MUDA: kuanzia SAA 2:00
Asubuhi hadi Saa 11:00 Jioni
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:
Mkoa wote wa Arusha
Sababu za Kujengwa
kwa Mradi huu wa TEDAP ni
·
Kuongeza upatikanaji wa umeme wenye ubora
(Voltage improvement) na upatikanaji wa umeme wa uhakika.
·
Kuepusha kukatika kwa umeme mara kwa mara kutokana na vituo kuzidiwa uwezo na
kuweka ring circuit kwa maeneo ili
kuwahudumia wateja pindi upande mwingine unapokuwa na hitilafu .
·
Kujiandaa na changamoto za maendeleo za
ukuaji wa viwanda na ukuaji wa mji (new master plan).Mfano Satelite cities
plan( Salian City, Safari city, Bondeni city
n.k) , Maendele ya viwanda hasa uwepo wa wewekezaji wa viwanda vikubwa
na upanuzi wa vilivyopo mkoani Arusha. Na kwa kuzingatia sera za serikali yetu
tukufu ya Awamu ya tano.
Tafadhali
usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka toa taarifa kupitia namba
za simu zifuatazo: - kituo cha miito ya simu 2194400 na 0768 985100
Uongozi
unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
Imetolewa na:- OFISI
YA UHUSIANO,
TANESCO
– KINONDONI KASKAZINI
No comments:
Post a Comment