TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Shirika la Umeme
Tanzania (TANESCO) linapenda
kuutaarifu Umma kuwa kupitia mradi wake wa uboreshaji wa miundombinu ya umeme
ya Jiji la Dar Es Salaam kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Japani (JICA) kutakuwa na uboreshwaji wa kituo
kikubwa cha Kupooza na Kusambaza umeme Ilala, cha Msongo wa Kilovolti 132 Ubungo
- Ilala. Kuanzia siku ya tarehe: 03
Septemba mpaka tarehe 25 Septemba, 2016. Katika kipindi hicho kituo cha Ilala
kitakuwa kinazimwa ili kufanya maboresho.
Sababu za uboreshwaji
wa miundombinu ya umeme kwa Jiji la Dar Es Salaam
·
Kuongeza upatikanaji wa umeme wenye ubora kwa kumruhusu Mkandarasi (TAKAOKA) kubadilisha
vikombe na nyaya na kuweka zenye uwezo mkubwa za laini mbili za msongo wa
kilovolti 132.
·
Kuboresha vituo vya kupooza na kusambaza
umeme vya Ubungo na Ilala kwa kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa zaidi .
·
Kubadilisha vifaa vya kupima umeme kwenye
laini mbili za Ubungo - Ilala.
Wakati wa
uboreshaji huu wateja wetu wataathirika kwa tarehe 03, 04, 10, 11, 17, 18, 24 na 25 Septemba,
2016, muda ni kuanzia saa 02 asubuhi hadi saa 11 jioni.
MAENEO
YAFUATAYO YATAATHIRIKA:
Maeneo yote ya kati kati ya jiji, Maeneo yote
ya Upanga, Maeneo yote ya Kariakoo, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya
Ilala, Mbagala yote, Chang’ombe yote, Kiwanda cha Saruji Maweni, Wizara ya
Utalii, Tusiime Mission, Tanzania Oxygen, Ofisi ya Manispaa ya Temeke,
Unilever, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Temeke, Uwanja wa Taifa, Makao Makuu ya Puma,
Temesa, Jamana Printers, Quality Plaza, Notco, Bima ya afya, Bandari geti na
maeneo ya jirani.
Maboresho
haya ya miundombinu ya umeme yanalenga kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana
katika jiji la Dar Es Salaam na Tanzania kwa ujumla.
Imetolewa na:- OFISI
YA UHUSIANO,
TANESCO
– MAKAO MAKUU
No comments:
Post a Comment