Umeme tayari nikafaa ambacho akihitaji mtandao wa
umeme katika nyumba isiozidi vyumba viwili au kimoja, kifaa hiki nikizuri na
kinafaa kwa mtu ambae hajafanya mtando
wa umeme katika nyumba yake na endapo
jamii husika imeshindwa kufanya mtandao wa umeme katika nyumba (vyumba viwili
au kimoja) kifaa cha umeme tayari ni kitamfaa zaidi.
Kifaa
hiki kina sehemu zifuatazo:- kikata umeme(Sockect
Braker),swichi kubwa (main switch), njia kuu tatu,taa moja kubwa na sehemu kuu
sita za kupitisha umeme kwenda maeneo usika ya nyumba yako.
Kikata umeme (Sokect Braker), hili ni eneo mojawapo
liliopo katika kifaa cha umeme tayari, sehemu hii ya kikata umeme nikuu kwa
kusaidia madhara au itilafu yoyote isitokee katika nyumba yako, kwamfano umeme
ukija kwa wingi vifaa vya mteja haviwezi kupata athari.
Swichi kubwa (main switch), ni eneo liliopo kwenye
umeme tayari ambalo linahusika na kuwasha, kuzima umeme na endapo shida yoyote
itakapotokea inajizima yenyewe ili kuepusha uharibikaji wa vifaa au nyumba
kuungua.
Njia tatu za kifaa hiki zinaweza kutumika kwa
matumizi tofautitofauti kama ya kupikia, kupiga pasi, na nyingine nyingi.
Mtumiaji wa kifaa hiki anatakiwa asiwe umbali wa
mita 30 kutoka nguzo ya umeme ilipo na matumizi yake hayapishani na ya nyumba
iliyofanyiwa mtandao wa umeme.
Ni kwa maeneo yote mijin na vijijin?
ReplyDeleteGharama ikoje
Bei yake sh ngap
DeleteMawasiliano ni yapi?
ReplyDelete