Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amesema kuwa mradi wa kupooza umeme wa Dege-Kigamboni jijini Dar es salaam, utaimarisha hali ya upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Kigamboni, Kurasini na Ilala.
Akizungumza katika eneo la ujenzi wa mradi huo alipokwenda kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi ,Oktoba 17, Waziri Kalemani amesema kuwa mradi huo umekamilika kwa asilimia 80 na kuitaka TANESCO kukamilisha mradi huo mapema zaidi
"Mradi huu unajengwa na TANESCO wenyewe,na wemeniambia mradi huu utakamilika Disemba mwaka huu, lakini Mimi naagiza mradi huu ukamilike mwezi ujao yaani Novemba 2020" alisema Dkt.Kalemani
Aidha, alioogezea kuwa mradi huo utaimarisha upatikanaji wa umeme kwa maeneo ya Kigamboni, Ilala na Kurasini kwa kuwa kwa sasa wanasambaziwa umeme kutoka katika kituo kimoja Cha kupoza Umeme cha Kurasini lakini baada ya kukamilika kwa kituo hicho, maeneo ya Kigamboni hayatapata shida ya umeme tena.
"Natambua kuwa kuna maeneo ya Kigamboni hayana umeme lakin niwaambie tu kuwa tatizo la umeme linakwenda kuisha kwani mara baada ya kukamilika kwa mradi huu maeneo mengi ya Kigamboni yatapata Umeme"alisema Dkt. Kalemani
Waziri pia amesema sekta ya Nishati Nchini imeimarika kwakuwa kwa sasa Kuna vituo vya kupooza umeme 107, ambapo ndani ya miaka 5 vituo vikubwa 43 na vituo vidogo 7, vimejengwa ndani ya miaka mitano.
Ameongeza kwa kusema kuwa changamoto ya kuharibika kwa miundombinu wakati wa mvua inakwenda kuisha kwani matumizi ya Nguzo za zege yameaza kutumika.
"Mradi huu umetumia Nguzo za zege, kama mnavoziona hapo nje na Nguzo hizo zimeanza kutumika maeneo yenye majimaji, ili kuepuka hali ya kukosa umeme inayotokana na Nguzo kuoza kwasababu ya maji" alisema Dkt.Kalemani.