February 26, 2018

"Zoezi la msako wezi wa umeme ni endelevu" Mhandisi Njavike

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kupitia kikosi kazi maalumu limeendesha Kampeni kabambe ya kubaini na kutokomeza matukio ya wizi wa umeme pamoja na uhujumu miundombinu y Mkoani Njombe ikiwa ni mwendelezo wa jitihada endelevu za TANESCO katika kudhibiti upotevu wa mapato ya Shirika.

Akiongea katika kampeni hiyo, Mhandisi Fredrick Njavike ambaye ni Meneja wa Kitengo cha udhibiti Mapato (RPU) alisema, ndani ya siku tano (5) kupitia kampeni hiyo tayari wamekagua takribani Wateja 2000 katika Wilaya ya Makambako pekee huku Njombe Mjini wakitarajia kukagua Wateja 1000.

  Aliongeza, katika idadi ya Wateja waliokaguliwa, baadhi waligundulika kujihusisha na vitendo vya wizi wa umeme hivyo kwa kushirikiana na vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Njombe wahalifu hao walichukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kulipa gharama za kiasi chote cha umeme walichokuwa wakiliibia Shirika baada ya kupigiwa mahesabu.

"Zoezi hili la ukaguzi na msako wa wezi wa umeme ni zoezi endelevu linalofanyika nchi nzima, niwatahadharishe wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo kuacha mara moja, kwani ni lazma watagundulika na hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na malipo ya fidia ya kiasi cha umeme walicholiibia Shirika". Alisema Mhandisi Njavike.

Alitoa rai kwa Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kufichua watu wenye viashiria vya wizi wa umeme.

" Lakini pia niwaombe wateja wetu kutoa taarifa TANESCO pale wanapona hitilafu zozote katika mita zao pamoja na kuepukana na vishoka wanaowashawishi waibe umeme kwani kupitia zoezi hili wezi wote watabainika." Alisisitiza Mhandisi Njavike

Kwa upande wake Meneja TANESCO Mkoa wa Njombe, Mhandisi Emmanuel Kachewa ametoa Wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Njombe kuendelea kushirikiana na TANESCO katika kuwafichua wezi wa umeme popote walipo ili waweze kuchukuliwa hatua na kuokoa upotevu wa mapato ya Shirika kwa ujumla.

Baadhi ya Wananchi waliozungumza na Afisa Uhusiano wetu wameipongeza TANESCO kwa kuendesha zoezi hili na kuongeza matukio ya wizi wa umeme yapo mtaani na wakati mwingine yamekuwa yakisababisha hata vifo kwa wahusika kunaswa na umeme wakati wakijaribu kuiba umeme hivyo ni vyema TANESCO pia wakatoa na Elimu juu ya madhara ya Wizi wa umeme kwa Wananchi wote wafahamu.

Aidha, TANESCO imekuwa ikiingia hasara kutokana na vitendo vya Wateja wachache ambao kwa makusudi kabisa wamekuwa wakiliibia Shirika umeme kwa katika maeneo mbalimbali na hivyo kulikosesha Shirika mapato stahiki na kurudisha nyuma jitihada za TANESCO na Serikali Katika kusambaza umeme nchi nzima na hivyo kufifisha kasi ya Uimarishaji wa Miundombinu ya Uzalishaji, Ufuaji na Usambaza umeme Nchini.


February 23, 2018

Kituo cha Kupoza Umeme cha Mbagala chawashwa.

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu Februari 22, 2018 amewasha Kituo  cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala chenye uwezo wa 50 MVA na hivyo kuimarisha upatikanaji wa umeme katika baadhi ya maeneo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar s Salaam, Mhe. Mgalu alisema kuwashwa kwa  Kituo hicho kutaondoa changamoto ya umeme iliyokuwa ikiyakabali maeneo ya Mbagala, Kigamboni, Mkuranga, Tandika na Kurasini, Maeneo hayo yatapata umeme wa uhakika.

Aliongeza kituo cha Mbagala kilikuwa kimezidiwa kutokana na mahitaji makubwa ya umeme katika maeneo hayo, kutokana na mitambo kuwa chakavu.

“Niwashukuru Bodi ya TANESCO kwa kusimamia hili vizuri, Menejimenti pamoja na Watendaji wa TANESCO kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuboresha miundombinu ya umeme”. Alisema Mhe. Mgalu.’  

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi aliwataka Wananchi wa Mbagala kuchangamkia fursa hiyo, kwani umeme wa uhakika sasa utapatikana katika maeneo hayo. “Ndani ya siku tatu Wananchi wa Mbagala wataanza kuona tofauti, hii ni kutokana na kuwashwa kwa Kitu”. Alisema Dkt. Kyaruzi.


February 21, 2018

"SERIKALI IMEKIONGEZEA UWEZO KITUO CHA KUFUA UMEME CHA MTWARA" NAIBU WAZIRI NISHATI
Naibu Waziri Nishati Mhe. Subira Mgalu (MB), amekagua mashine mbili zenye uwezo wa kufua jumla ya Megawati nne (4) zitakazofungwa katika kituo cha kufua umeme kwa ktumia  gesi asilia cha "Mtwara Gas Plant".

Katika ziara hiyo, Mhe. Mgalu aliambatana na Viongozi wa Wizara, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander L. Kyaruzi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Khalid James na Uongozi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Alisema, Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inaendelea kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa umeme Mikoa ya Mtwara na Lindi na hatua mojawapo zinazochukuliwa ni kukiongezea uwezo kituo hicho.

Aliongeza, kituo cha Mtwara kina miaka kumi (10) tangu kujengwa kwake na kina jumla ya mashine tisa (9) zenye uwezo wa kufua Megawati 18, na kwa juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati  zinaongezwa mashine mbili zenye uwezo wa kufua Megawati nne (4) hivyo kufikia Jumla ya Megawati ishirini na mbili (22).

"Kutokana na kukua kwa mahitaji ya umeme kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi, Serikali iliona ipo haja ya kuongeza mashine nyingine mbili zenye uwezo wa kufua Megawati nne ili ziungane na zilizopo na hivyo kufikisha Megawati ishirini na mbili ambazo zitakuwa na uwezo wa kutosheleza mahitaji katika Mikoa ya Mtwara na Lindi". Alisema Mheshimiwa Naibu Waziri.

Mahitaji ya juu ya umeme kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi ni zaidi ya Megawati 16, hivyo ujio wa mashine hizi unatarajiwa kuimarisha zaidi hali ya upatikanaji wa umeme katika Mikoa hiyo.

"SERIKALI IMEKIONGEZEA UWEZO KUTUO CHA KUFUA UMEME CHA MTWARA" NAIBU WAZIRI NISHATI


Niabu Waziri Nishati Mhe. Subira Mgalu (MB), amekagua mashine mbili zenye uwezo wa kufua jumla ya Megawati nne (4) zitakazofungwa katika kituo cha kufua umeme kwa ktumia  gesi asilia cha "Mtwara Gas Plant".

Katika ziara hiyo, Mhe. Mgalu aliambatana na Viongozi wa Wizara, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander L. Kyaruzi, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Khalid James na Uongozi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani.

Alisema, Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) inaendelea kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa umeme Mikoa ya Mtwara na Lindi na hatua mojawapo zinazochukuliwa ni kukiongezea uwezo kituo hicho.

Aliongeza, kituo cha Mtwara kina miaka kumi (10) tangu kujengwa kwake na kina jumla ya mashine tisa (9) zenye uwezo wa kufua Megawati 18, na kwa juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati  zinaongezwa mashine mbili zenye uwezo wa kufua Megawati nne (4) hivyo kufikia Jumla ya Megawati ishirini na mbili (22).

"Kutokana na kukua kwa mahitaji ya umeme kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi, Serikali iliona ipo haja ya kuongeza mashine nyingine mbili zenye uwezo wa kufua Megawati nne ili ziungane na zilizopo na hivyo kufikisha Megawati ishirini na mbili ambazo zitakuwa na uwezo wa kutosheleza mahitaji katika Mikoa ya Mtwara na Lindi". Alisema Mheshimiwa Naibu Waziri.

Mahitaji ya juu ya umeme kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi ni zaidi ya Megawati 16, hivyo ujio wa mashine hizi unatarajiwa kuimarisha zaidi hali ya upatikanaji wa umeme katika Mikoa hiyo.

February 2, 2018

TANESCO yamaliza tatizo la umeme Bagamoyo

Na Severin Mvungi,
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limepatia ufumbuzi tatizo la kukatika umeme mara kwa mara katika wilaya ya Bagamoyo ambalo limekuwa ni kero kwa wakaazi wa mji huo na viunga vyake.

Kwa kipindi sasa wakaazi wa mji huo wamekuwa wakipata adha ya kukatika kwa umeme mara kwa mara kutokana na hitilafu mbalimbali za mifumo na miundombinu ya umeme ya Shirika hilo.

Meneja wa Mkoa huo Mhandisi Martin Madullu alieleza kuwa tatizo kubwa la kukatika umeme kwenye Wilaya hiyo lilitokana na upepo na mvua ambazo zilikuwa zikinyesha na kuangusha nguzo zinazovusha umeme kutoka Dar es Salaam katika eneo la Mapinga darajani kwenye mto Mpiji.

Madullu aliongeza kuwa sababu nyingine ilikuwa ni wilaya hiyo kutegemea njia moja ya umeme ambayo pia inagawa umeme kwa wateja wengine ikitokea Tegeta kwenye Kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Kunduchi.

“Kwa sasa ukipita Mapinga darajani utashuhudia kazi kubwa iliyofanywa na wataalamu wetu ya kuvusha umeme kwenye mto mpiji na ni matarajio yetu kuwa hata mvua zikinyesha nguzo hizo haziwezi kuanguka tena au kufikiwa na maji” alisema Mhandisi Madullu.

Kuhusu sababu ya pili, Mhandisi Madullu alisema mafundi wa TANESCO Mkoa wa Pwani kwa kushirikiana na wa Tegeta na wataalamu kutoka Makao makuu wamejenga njia maalum “dedicated line” kwa ajili ya Wilaya ya Bagamoyo tu ambayo haitaunganishwa na wateja wengine.

“Bagamoyo tumeitafutia njia ya peke yake ya kupeleka umeme ambayo itakuwa inatoa umeme mkubwa kutoka Kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Kunduchi hadi Bagamoyo. Hii itaondoa matatizo yote ya kukatika umeme mara kwa mara ambayo yalikuwa yanasababishwa na hitilafu za wateja wengine waliokuwa wameungwa njiani” aliongeza Mhandisi Madullu.

Aidha Mhandisi Madullu alisisitiza kuwa wateja wa Wilaya ya Bagamoyo na viunga vyake wategemee umeme wa kutosha na wauhakika kwa sasa kwani pamoja na njia hiyo inayotokea Kunduchi pia njia inayoleta umeme kutokea Kituo cha kupooza na kusambaza umeme cha Mlandizi kuja Bagamoyo nayo imeimarishwa. 

Bagamoyo ni moja ya miji mikongwe nchini  yenye historia ya Taifa letu na inayotembelewa na wageni wengi kujionea makumbusho ya taifa hasa magofu ya Kaole ambayo yaliyokuwepo tangu karne ya 13 na 15.