October 29, 2013

Katizo la umeme mkoa wa Kinondoni KaskaziniShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini  kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-


TAREHE:      30 Oktoba 2013 (Jumatano)
                    
SAA:               3.00 asubuhi  hadi saa 11.00 jioni.

SABABU:     kubadilisha nguzo zilizooza na kukata miti iliyo chini ya laini za umeme za TG3,TG4 na TG5
   
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:-
Wazo/Tanganyika Portland Cement, Salasala Magengeni, Bagamoyo na Bunju, Bahari beach, Ununio, Ras Kilomoni, Budget hotel, Njia panda ya wazo factory, Teget, Boko, Boko Maliasili, Boko National Housing, Ndege beach, Mbweni Kijijini, nyumba 151 za Serikali, Bakili Muluzi school, Mbweni Ofisi ya Raisi flats, Marando street. Kunduchi yote, Kunduchi Recruitment Training School (RTS) of TPDF, Mbuyuni, MECCO, JKT machimbo, baadhi ya maeneo ya Salasala, Shule ya Green Acres, Baadhi ya maeneo ya Kilongawima, Mbezi Africana, Mbezi Majumba sita, Lugalo Salasala, Kinzudi na maeneo yanayozunguka.

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo 2700367, 0716 768584 na 0784 768584, kituo cha miito ya simu namba 2194400.
                              
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na:          OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO

Katizo la umeme mkoa wa Kinondoni Kaskazini

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA TEMEKEShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Temeke kuwa, kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

TAREHE:      Jumatano   30/10/ 2013     

MUDA:           03:00 Asubuhi – 11:00 jioni

SABABU:      Kufanya ukarabati kwenye laini ya umeme.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Mkuranga, Mtoni kwa Azizi Ally, Mtoni Sabasaba, Mtaa wa Wandengereko, Mtoni kwa Kidandasi, Achimwene, Mkunguni, Mbagala Mission, Container Terminal, Chuo cha Uhasibu,  Charambe, Majimatitu, Kimbangulile, Chamanzi, Mbande, Msongola, Saku, Maeneo ya viwanda, Kiburugwa, Kingungi, Nzasa, Kilungule, Kizuiani, Kwa Manganya, Sabasaba, Bugudadi, Mtoni Kizinga, Kibondemaji, Dar Cement, Mbagala Jeshini, Kijichi, Mbagala kuu, Mission KTM, Miande na maeneo ya jirani.

Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia Dawati la dharura Mkoa wa Temeke:- 0222138352, 0732 997361, 0712 052720, au Kituo cha miito ya simu 022 2194400 /0768 985 100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


Imetolewa na:          OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.
 

KATIZO LA UMEME MKOA WA MWANZAShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa mkoa wa Mwanza kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya ALHAMISI tarehe 31/10/2013 kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.

Sababu ni kubadilisha nguzo zilizooza na kukata matawi ya miti kwenye njia ya kusafirishia umeme kutoka kituo cha Nyakato hadi Wilaya za Nyamagana, Misungwi na Ngudu.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA NI:-
Ngudu Mjini, Nyambiti, Iyoma, Malya, Mwabuki, Misungwi,Ukiriguru, Usagara, Mkolani na maeneo yote ya Nyegezi.

Tafadhali usishike, usikanyage wala kusogelea nyaya za umeme zilizolala chini, toa taarifa  TANESCO Mwanza  kupitia   namba za simu zifuatazo 028 250 0090 , 028 250 1060.

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na:  OFISI YA UHUSIANO
                          TANESCO -  MAKAO MAKUU.    

October 25, 2013

Tusiisahau mitambo ya hydro-Wabunge


 • Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wameitaka Serikali na TANESCO kutoisahau na kuitelekeza mitambo inayotumia nguvu ya maji kutokana na mitambo inayotumia nguvu ya gesi kuanza kutumika.
  Wabunge hao waliyasema hayo wiki hii, walipofanya ziara katika mitambo inayotumia nguvu ya maji kuzalisha umeme ya New Pangani, Kidatu, Mtera na Kihansi ili kujionea hali ya mitambo hiyo na jinsi inavyochangia umeme katika gridi ya taifa.
  Mbunge wa Same Mashariki Mhe. Anne Kilango Malecela alisema kwa hakika wao kama wabunge hawakujua kama Serikali kupitia TANESCO imewekeza rasilimali kubwa na zenye thamani kwenye nchi kama ilivyo kwenye mitambo inayotumia nguvu ya maji kuzalisha umeme.
  “Mimi nasema nitapamba na yeyote atakayesema kwamba Serikali haikuwekeza, oneni jinsi utaalamu mkubwa ulivyotumika hapa na rasilimali nyingi zimewekezwa hapa kwenye mitambo hii”.
  “Tunaiomba Serikali kuangalia tulikotoka na ihakikishe mitambo hii haipuuzwi na kusahaulika eti kwa sababu sasa tumeanza kutumia mitambo ya gesi,  tusigeuke kuwa na tabia za wanaume wengi kwamba akioa mke mdogo basi humsahau na kumtelekeza mke mkubwa, sasa na sisi tusihau mitambo ya hydro”, alisema Mhe. Kilango kwa msisitizo.
  Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ndiyo aliyekuwa kiongozi na Mwenyekiti wa msafara huo Mhe. Jerome Bwanausi alisema Wabunge wamejifunza mambo makubwa ambayo wasingeyajua kuhusiana na umeme kama wasingefanya ziara hiyo kwenye mitambo hiyo.
  Mhe. Bwanausi alisema kazi ya uzalishaji umeme, kuusafirisha hadi kumfikia Mwananchi ni kubwa tofauti na watu wengi wanavyodhani kwa hiyo ni muhimu kwa TANESCO kutoa elimu kwa wananchi kwa kuonyesha hatua zote ambazo umeme unapitia hadi kumfikia Mtanzania wa kawaida.
  “Ni muhimu sana kwa sisi wabunge na hata viongozi wa Serikali kutembelea mara kwa mara mitambo hii na kujiona hali halisi na maendeleo yake kwa kuwa hizi ni rasilimali kubwa za taifa letu”, alisisitiza Mhe. Bwanausi.
  Naye Mhe. Devotha Likokola alisema kutokana na uwekezaji mkubwa katika sekta ya umeme nchini ni muhimu kwa TANESCO kushirikiana na Wabunge hususan wa Kamati ya Nishati na Madini katoa elimu ya matumizi bora ya umeme kwani umeme ni gharama na uwekezaji wake unatumia rasilimali nyingi.
  “Nasema TANESCO acheni kukaa kimya tushirikisheni sisi wabunge ili tukawaeleze wabunge mambo mazuri yanayofanywa na TANESCO na pia juu ya matumizi bora ya umeme, sisi ndiyo wawakilishi wa wananchi, na mimi ndiyo nitakuwa wa kwanza kuwa balozi wa kutoa elimu hiyo najitolea,” alisisitiza Mhe. Likokola.
  Mhe. Juma Njwayo aliitaka TANESCO kushiriki katika kuisaidia jamii (Corporate Social responsibility) katika maeneo ambayo ya mitamboni ili wananchi waione hiyo mitambo ni mali yao kwa kuijali na kuilinda.
  Aidha, Mhe. Njwayo alisema kwamba mbali na jamii hata wafanyakazi ambao wanafanyakazi kwenye mitambo hiyo lazima wapewe vivutio vya kuwafanya wafanye kazi kwa moyo na wasijione kama wametengwa ama kupelekwa kwenye mitambo hiyo ni adhabu.
  Mhe. Dkt. Dalali Kafumu alisisitiza kwa wafanyakazi wa mitambo hiyo kupelekwa kusoma mara kwa mara kwa kuwa teknolojia ya mitambo hubadilika nayo kila wakati.
  Mhe. Murtaza Mangungu alisisiza kwa Serikali kuhakikisha mitambo hiyo inafanyiwa matengenezo haraka pale inapopata hitilafu badala ya kuicha na hatimaye taifa kupoteza mapato ambayo yangepatikana kwa uzalishaji umeme.
  “Ninasikitika sana kusikia kwamba mtambo mmoja wa Hale uliharibika tangu mwaka 2004 hadi leo umeachwa, tunataka Serikali itueleze kwa nini imefanya hivyo na lini mtambo huo wataurekebisha, ituambie ‘revenue loss’ kutokana na kuharibika kwa mtambo huo”, alihoji Mhe. Mangungu.


   Waheshimiwa Wabunge wakiwa katika ukumbi wa mkutano kwenye kituo cha Hale wakipata maelezo juu ya hali ya mitambo na namna inavyofanya kazi kuchangia umeme kwenye gridi ya taifa

   kutoka kushoto aliyevaa koti ni Meneja wa Mtamno wa New Pangani Mhandisi John Skauki akitoa maelezo kwa Wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini katika eneo la Bwawa la New Pangani Falls.
   kutoka kushoto aliyevaa koti ni Meneja wa Mtamno wa New Pangani Mhandisi John Skauki akitoa maelezo kwa Wabunge wa Kamati ya Nishati na Madini katika eneo la Bwawa la New Pangani Falls.
   katikati aliyenyoosha mkono ni Meneja anayesimamia mitambo ya umeme inayotumia nguvu ya maji Mhandisi Costa Rubagumya akitoa maelezo kwa wabunge waliofika kwenye Bwawa la New Pangani falls kuangalia hali ya maji kwenye Bwawa hilo.
   aliyenyoosha mkono ni Mhandisi wa New Pangani Bw. Makunga akiotoa maelezo ya jinsi mitambo ya maji inavyofanya kazi
   Katikati mwenye miwani ni mbunge wa Same Mashariki, Mhe. Anne Kilango Malacela na wenzake wakimsikiliza Mhandishi wa mitambo wa New pangani Falls akiwapa maelezo namna maji yanavyogonga turbine na umeme kuzalishwa


   

October 24, 2013

Tanesco yatoa ushauri kwa mashirika makubwa juu ya matumizi bora ya umeme

 Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Mhandisi Sophia Mgonja akifungua mjadala na wawakilishi wa makampuni makubwa juu ya utumiaji bora wa umeme.


Mwakilishi wa  idara ya mfumo wa uthibiti umeme Mhandisi Issa Abubakar akielezea jinsi ya utumiaji bora wa nishati inayo patikana.Mwakilishi wa LIBRA (T) LTD Mhandisi Sylvester Mkaka akiongelea juu ya kifaa ambacho kinatumika kuthibiti matumizi ya umeme. 

Mshiriki akitoa ushauri katika sekta ya umeme kuwe na ufuatiliaji mzuri. Mshiriki akichangia maada kwa kueleza sekta ya viwanda inahitaji kuwa na umeme wa kuaminika ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa.
Mwakilishi kutoka wizara ya nishati na madini Mhandisi Styden Rwebangila akijibu maswali ya kutoka kwa waandishi juu ya changamoto za kitalaam zinazo patikana juu ya matumizi bora ya nishati ikiwa ni pamoja na ukosekanaji wa uelewa kwa wateja.


 

Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Tanesco Mhandisi Sophia Mgonja akijibu maswali ya kutoka kwa waandishi juu ya utumiaji bora wa umeme bila kuathiri uzalishaji wa bidhaa.

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA WA PWANIShirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Pwani  kuwa kutakuwa na katizo la umeme siku ya JUMAMOSI tarehe 26/10/2013 kuanzia saa 4:00 Asubuhi hadi saa 11:00 Jioni.  Sababu ni kufanya matengenezo, kubomoa spar laini na kubadilisha nguzo zilizooza katika laini ya msongo wa 33Kv, Mkuranga.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Vikindu, Kisemvule, Mkuranga

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo: 0657 108782 au Kituo cha kupokelea miito ya simu namba 2194400 au 0768 985 100

Uongozi unasikitika Kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


Imetolewa na:-         OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.