February 23, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


UFAFANUZI KUHUSU UAMUZI WA MAHAKAMA KUU KUHUSIANA NA SHAURI KATI YA TANESCO NA DOWANS.Mkurugenzi Mtendaji Wa TANESCO, Eng. William Mhando, akifafanua Jambo kwa Wahandishi Wa habari, Kulia ni Meneja Uhusiano TANESCO, Bi. Badra Masoud.


Kufuatia uamuzi wa  Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi ya ombi la TANESCO kukata rufaa juu ya pingamizi lililowasilishwa na Dowans dhidi ya ombi la TANESCO, kumekuwa na taarifa sisizo sahihi zilizoandikwa aidha kwa kutokufahamu au kwa sababu zingine na kutangazwa  na baadhi ya vyombo vya habari ambazo TANESCO inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo:

  1. TANESCO iliwasilisha ombi la kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama kuu uliotolewa na Jaji Emilian Mushi tarehe 28 Septemba, 2011 ambao uliamuru  pamoja na mambo mengine uamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICC) usajiliwe rasmi na mahakama ya hapa Tanzania.

  1. Aidha, kwa mujibu wa taratibu za rufaa TANESCO iliomba ruhusa (leave to appeal) toka Mahakama Kuu ili iruhusiwe kuwasilisha rufaa yake rasmi mbele ya Mahakama ya Rufaa Tanzania.

  1. Sanjari na ombi la ruhusa, TANESCO iliwasilisha ombi la kuitaka Mahakama Kuu isitishe kukaza hukumu ( application for stay of execution) ya tozo ya ICC kama ilivyoamriwa tarehe 28 Septemba 2011 na Mahakama Kuu.

  1. Dowans kwa upande  wake waliwasilisha pingamizi dhidi ya ombi la TANESCO  la kukata rufaa kwa madai kuwa uamuzi wa ICC kama ulivyoridhiwa na Mahakama Kuu haukatiwi rufaa, kwa mujibu wa sheria

Tarehe 20 Februari, 2012, Mahakama Kuu  kitengo cha biashara chini ya Jaji Dk. Fauz  Twalib ilitolea uamuzi maombi ya  TANESCO hali kadhalika pingamizi la Dowans kama ifuatavyo;
 
1.        Pingamizi lililowekwa na DOWANS dhidi ya TANESCO lilikuwa halina sababu ya kuwepo kwa kuwa TANESCO wana haki ya kisheria kupinga maamuzi ya ICC kama yalivyoridhiwa na Mahakama Kuu katika Mahakama ya Rufaa. Pingamizi hilo lilitupiliwa mbali.

2.        Ombi la kukata rufaa lililowasilishwa na TANESCO  lilionekana kuwa si la lazima  kwa vile TANESCO tayari walikuwa na haki ya kisheria  kukata rufaa .

3.        Kuhusu ombi la kusitishwa kukaziwa hukumu kama lilivyowasilishwa na TANESCO, Mahakama iliamuru ombi hilo  lisikilizwe tarehe 18 April 2012

Tunaomba vyombo vya habari kuwa makini wakati wa kuripoti taarifa ya kesi hii kati ya DOWANS na TANESCO ili kuepuka upotoshwaji ambao kwa namna moja au nyingine huenda ukaleta tafsiri tofauti na ukweli wa maamuzi ya mahakama.


Badra Masoud
Meneja MawasilianoTAARIFA YA KATIZO LA UMEME MKOA KILIMANJARO


Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Kilimanjaro kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

TAREHE:   24/02/2012, siku ya Ijumaa pamoja na Jumamosi 25/02/2012
                    
SAA:          2:00 Asubuhi- 10:00 Jioni

SABABU:   MATENGENEZO KATIKA LAINI YA K50 TOKA KIDOGO CHA UMEME KIYUNGI HADI  BOMAMBUZI .

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA: Moshi mjini, maeneo ya viwandani Soweto,  
SIDO,Majengo,Ngangamfumuni,Bomambuzi,Pasua,Kaloleni,Mabogini Kahe,Sango.Old moshi,Mnazi mmoja, Msaranga,  Himo,Kilema, Holili  Marangu, Mwika,Rombo na  Tara kea.

Tafadhali usishike waya uliokatika, toa taarifa kupitia simu zifuatazo: 027 2755007, 027 2755008Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na katizo hili.


Imetolewa na:     Ofisi ya Uhusiano
                              Tanesco-Makao Makao

February 21, 2012

Hivi ndivyo vishoka na wafanyakazi wa TANESCO wasio waaminifu wanavyohujumu shirika letu (TANESCO)

Hii ni mita iliyotumika ambayo haikusajiliwa 
na TANESCO..

Maafisa wa Polisi kutoka Kituo cha Kati wakishirikiana na Maafisa Usalama wa Tanesco mkoa wa Temeke, wamefanikiwa kuzibaini nyumba mbili zilizounganishiwa umeme kinyemela na kujenga nguzo tisa kwa kutumia vishoka katika la Vigozi lililoko Mbagala jijini Dar es Salaam.