March 31, 2015

KUKANUSHA TAARIFA KUHUSU HUDUMA YA LUKU

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA- TANESCO

KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA HUDUMA YA LUKU ITAKOSEKANA KWA WIKI MBILI

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linakanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya jamii kwamba huduma ya kununua umeme kwa LUKU itasitishwa kwa wiki mbili.Taarifa hizi ni za uongo na zinazolenga kuharibu taswira ya shirika katika jamii.Mifumo yote ya LUKU ipo salama kabisa na Tanesco tunaendelea kuwahudumia wateja wetu kama kawaida.

Tunawaomba wateja wetu kuzipuuza taarifa hizo.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu.

March 17, 2015

TAARIFA KWA WATEJA WA KINONDONI KASKAZINI

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKOSEKANA UMEME KINONDONI KASKAZINI

Shirika la umeme Tanzania linawatangazia wateja wake kuwa,waya mkubwa wa njia ya kupeleka umeme maeneo ya Mwenge kutokea kituo cha kusambaza umeme cha Mbezi Beach imelipuka majira ya saa 5 asubuhi.Mafundi wanabadilisha waya huo na tunatarajia umeme utarudi leo leo kabla ya saa 1 usiku.Maeneo yanayokosa umeme ni baadhi ya maeneo ya Mwenge,baadhi ya maeneo ya Chuo kikuu cha DSM,Lugalo na baadhi ya maeneo ya Mbezi Tangi Bovu.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano
 TANESCO:Makao Makuu.