EVENTS


TANESCO YATOA ELIMU YA UMEME KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI DAR.


Shirika la umeme Nchini (Tanesco) Agasti 5 na 6, 2014 imetoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi Ubungo NHC na Mirambo za jijini Dar. 
Matukio katika Picha.
Meneja wa kitengo cha afya na usalama kazini Mhandisi Majige Mabulla akitoa somo kwa wanafunzi.
 
Kaimu Meneja Mahusiano Bw. Adrian Severini akitoa elimu ya umeme kwa wanafunzi wa shule ya Msingi Mirambo.


Wafanya kazi wa Tanesco pamoja na wanafunzi waliopata zawadi wakiwa katika picha ya pamoja

Baadhi ya walimu wa Shule ya Msingi Mirambo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO

Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Ubungo NHC akijibu swali kutoka kwa wataalamu wa TANESCO

Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Ubungo NHC wakifuatilia mafunzo.    










TANESCO YASAINI MKATABA WA KUWAUZIA UMEME SIMBA CEMENT.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO) Mhandisi, Decklan Mhaiki (wa pili kushoto) Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Reinhardt Swart (wa pili kulia) na Meneja Kiwanda wa TCCL, Ben Lema (kulia), wakisaini makubaliano maalum ya kuuza umeme, jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia  ni Meneja Sheria, Mikataba na Mahusiano ya Biashara wa Tanesco, Mwesiga Mwesigwa.
 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO) Mhandisi, Decklan Mhaiki Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Reinhardt Swart


 
 
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa (TANESCO) Mhandisi, Decklan Mhaiki (wa pili kushoto) akibadilishana makataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Saruji Tanga (TCCL), Reinhardt Swart (wa pili kulia). Wakishuhudiwa na Meneja Kiwanda wa TCCL, Ben Lema (kulia), Meneja Sheria, Mikataba na Mahusiano ya Biashara wa Tanesco, Mwesiga Mwesigwa.


 TANESCO YANUFAIKA NA MAFUNZO  YA TAGCO.

Idara ya mahUsiano TANESCO imenufaika na mafunzo yaliyoandaliwa na chama cha maafisa Habari Serikalini(TAGCO),Mafunzo hayo yametolewana Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo  prof.Elisante Ole Gabriel  katika ukumbi wa Karimjee, Dar es salaam.
Akitoa mafunzo hayo mwishoni mwa wiki, prof . Elisante alisisitiza kuhusu kutoa huduma bora kwa wateja,kwani wateja ndio sababu kubwa za kuwepo kwa taasisi za serikali,amesema wateja wanatakiwa kuhudumiwa kwa ukarimu na Nidhamu,huku sheria na taratibu za kazi zikizingatiwa.
Sanjali na mafunzo hayo ya huduma kwa wateja,pia  Maafisa uhusiano TANESCO walipata elimu kutoka kwa mtaalamu wa Idara ya itifaki,Wizara ya Mambo ya Nje BW. Kosato Chumi juu ya Itifaki na Protoko Serikalini.
Akizungumzia Itifaki , Bw. Kosato ameongelea taratibu zote serikalini ,ikiwemo na swala la mavazi maofisini,ya kuwa wafanyakazi hasa serikalini wanatakiwa kuvaa sawa sawa na taratibu zilizowekwa na serikali katika ofisi zake,na hasa Maafisa uhusiano wanatakiwa kuzingatia zaidi uvaaji wao hasa kwenye mazingira tofauti ya kazi zao  na matukio mbalimbali ya kiofisi ,kwani wao ni wawakilishi wa Taasisi zao.
Katika Mafunzo hayo TANESCO pia imepongezwa na Katibu mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo (WHVUM) Bi sihaka Nkinga kwa kuonesha  muitikio mkubwa wa mahudhurio kuliko taasisi  zingine  za serikali zilizoshiriki.
Huu ni mwanzo tu wa Chama Hicho cha wanahabari serikalini,ambacho kwa pamoja wamedhamiria kuimarisha utendaji bora wa shughuli zote za Fani ya Maafisa Uhusiano  na Habari serikalini,ambapo mafunzo mbalimbali yanatarajiwa kufanyika kila robo ya Mwaka,na hivyo kuen delea elimisha wanachama wake,TANESCO ikiwa mmoja wa wanachama hao.
 











MEI MOSI 2014:
Kilio chenu ni kilio changu: Kikwete



Wafanyakazi wa Shirika la Umeme nchini  TANESCO Mei 1, 2014, wameungana na wafanyakazi wengine Duniani  kusherehekea sikukuu ya wafanyakazi  Mei Mosi iliyofanyika kitaifa Mkoani  Dar Es Salaam. Kauli mbiu ya mwaka huu “UTAWALA BORA UTUMIKE KUTATUA KERO ZA WAFANYAKAZI.”
Mgeni rasmi katika sherehe  hizo  Mheshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa pomgezi kwa shirikisho la wafanyakazi TUCTA kwa kuratibu sherehe hizo na wanachi wa Dar Es Salaam  kupitia kwa Mkuu wa Mkoa kwa kujitokeza kusherehekea.
Akizungumzia kuimarika kwa Uchumi wa Taifa huku  kipato cha mtu mmoja mmoja kikiwa bado cha hali chini Mh. Raisi alisema kuimairika kwa uchumi wa Taifa kunategemea asilimia 7 ya  secta  ya mawasiliano, huku sekta ya  Madini, Viwanda na ujenzi vikichangia asilimia 70, sekta ya kilimo ambayo inakundi kubwa la wananchi ikiwa inakua kwa asilimia 4.3
“Sekta ya kilimo inakuwa kidogo sana ndio maana serikali ilianzisha mkakati wa kilimo kwanza ikiwa na shabaha ya kuimarisha sekta  hiyo.Pia Serikali inapambana  Kushusha mfumuko wa bei  akitolea mfano mwezi Mei mwaka jana ulishuka kwa asilimia 9, mpaka kufika  Mwezi mei mwaka huu mfumuko wa bei umeshuka mpaka asilimia 6.3 alisema na aliongeza.”.
“Nyongeza ya mshahara haitakuwa na tija kama hatutapambana na mfumko wa bei ndio maana Serikali inapambana kushusha mfumko wa bei ikiwa ni pamoja na kuagiza bidhaa kutoka nje mfano sukari kwani viwanda vya ndani havina uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosheleza mahitaji  ya watanzania.”
Alisema migogoro sehemu za kazi hutokea pale panapokuwa hakuna uwazi na ushirikishwaji wa wafanyakazi  na wakati huo akiwataka waajiriwa kumtendea haki mwajiri kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma na kuwataka waajiri kuwashirikisha wafanyakazi kwenye mabaraza ya kazi.  Kodi ya mapato kwa wafanyakazi ilikuwa asilimia 18.5 mwaka 2007, imeshuka mpaka asilimia 13 kwa sasa na kuahidi kuendelea  kulishugulikia swala hilo kwani malengo ni kufikia asilimia ya tarakimu moja.
Aliongeza madai ya wafanyakazi serikalini yatalipwa kabla ya mwaka huu wa fedha kumalizika, uhakiki wa madeni ya walimu unaendelea,   katika halmashauri 147 halmashauri 96 ndio uhakiki wake umekamilika, na wamebaini baadhi ya madeni si halisia ni ya kugushi. Alisema makampuni mengi hulazimika kuajiri watu kutoka nje kwa sababu ya dhana ya watanzania  hatuheshimu kazi na kujituma. “heshimuni kazi, usicheze na kazi chezea mshahara alisema”
Aliipongeza Wizara ya kazi kwa kufuta mawakala wa ajira kwani wamekuwa wanaajiri wafanyakazi na kuwapeleka kufanya kazi huku wakiwa waajiriwa wao, hali hii huwakosesha wafanyakazi  fursa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii, likizo, matibabu na kukatwa  mishahara yao huku akikiita kitendo hiki kama dhuluma, alisema malengo ya mawakala hawa ilikuwa watumike kama daraja la kuwaunganisha watafuta kazi na waajiri .

  
Mh. Raisi pia alitoa zawadi kwa wafanyakazi bora wa mwaka  huku mfanyakazi bora kitaifa kutoka Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini TANESCO Bw. Joel Peter Kibonge akiwa miongoni  mwa wafanyakazi bora 32waliopewa tuzo na Mh. Raisi.
Mgeni rasmi alimalizia kwa kushukuru  kupewa nafasi na kuahidi kutatua changamoto zinazo wakabili wafanya kazi  “kilio chenu ni kilio changu alisema” na kuahidi maslahi mazuri kwa wafanyakazi.

TANESCO YAWAPONGEZA WAFANYAKAZI BORA WA MWAKA 2014
Shirika la umeme nchini TANESCO Mei 1, 2014 limefanya hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi  bora wa matawi na idara  pamoja na mfanyakazi bora kitaifa mwaka 2014 Bw. Joel Peter Kibonge  ambaye ni fundi mchundo kutoka kituo cha uzalishaji umeme  Loliondo Mkoani Arusha. Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi waandamizi wa Shirika.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Kaimu mkurugenzi wa TANESCO Mhandisi  Decklan Mhaiki aliwapongeza waliochaguliwa kuwa wafanyakazi bora na kusema shirika limeona umuhimu wa kuwapongeza  na kuboresha zawadi kutoka radio  na kuwa TV za nchi 32.
Alisema zawadi hizo ziwe chachu kwa wafanyakazi kufanya kazi  kwa bidii, ufanisi, na ubunifu ili kuweza kujenga TANESCO yeneye ufanisi. Alimpongeza mshindi wa kitaifa na kusema hakupatikana kwa bahati balli vigezo vilizingatiwa na yeye kuwa mshindi.
Kwa mujibu wa  Mwenyekiti wa TUICO TANESCO Makao Makuu Bw. Ally Mkama alisema mfanyakazi bora wa mwaka ameweza kupata zawadi ya TV nchi 32, cheti, hundi ya pesa za kitanzania shilingi milioni 3 na pia atachagua Nchi yoyote Duniani atakayopenda kwenda kutembea pamoja na mwenza wake kwa muda wa siku saba.
Mshindi kitaifa Bw. Kibonge alisema anafurahia kuwa mfanyakazi  bora na kuwataka wafanyakazi wengine kufanya kazi kwa bidii na hari mpya pia kuongeza mshikamano katika utendaji.Pia alitumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa shirika na wafanyakazi kwa ujumla.

WATEJA MITA ZA KAWAIDA KULIPA BILI KWA NJIA YA MTANDAO   KIBENKI
Mei 2, 2014 Shirika la Umeme nchini TANESCO limezindua huduma ya malipo ya bili kwa njia ya mtandao na benki  kwa wateja wa Kinondoni kusini wanaotumia  mita za kawaida.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba alisema lengo la kuanza kwa huduma hii ni kuwawezesha wateja wanaotumia mita za kawaida kuweza kulipa bili zao pasipo kupata usumbufu wa kutembea umbali mrefu kwenda kwenye ofisi za TANESCO na kupanga foleni ili kulipia bili zao.
“Katika  kuboresha huduma zake kwa wateja shirika lipo kwenye mkakati wa kuanzisha mawasiliano na mteja  kwa njia ya SMS inapo tokea tatizo sehemu husika, akitolea mfano kukatika kwa umeme ama panapokuwa na matengenezo ya kuboresha miundo mbinu”.
Kwa sasa wateja waTANESCO  Kinondoni Kusini wanaotumia  mita za kawaida wanaweza kulipa Ankara kupitia simu zao za mkononi kwenye mitandao ya Tigo, Vodacom na Airtel pia kupitia  Mashine za Maxcom na Selcom  zitatoa huduma ya kulipia Ankara kama zinavyoweza kuuza umeme kwa wenye mita za LUKU alisema.
Nae Meneja Mwandamizi kanda ya Dar Es Salaam na Pwani Mhandisi Mahende Mugaya  alisema mkoa wa kinondoni kusini umefanikiwa kupunguza deni kwa kukusanya mapato, “ huduma hii mpya itakuwa na faida kwa wateja na TANESCO  kwani itamuwezesha mteja kulipa bili mahali popote alipo na kwa urahisi. Pia itaokoa muda na ni njia salama kabisa ya malipo alisema.”
Kwa upande wake Kaimu Naibu Mtendaji usambazaji na huduma kwa wateja Mhandisi Nicholaus Kamoleka  alisema utumiaji wa malipo kwa njia ya mtandao ni mpya kwa TANESCO , pia ni maagizo kutoka serikalini. “ Mwaka jana Shirika lilivuka malengo kwa kuwaudumia  wateja laki moja na elfu arobaini na tatu alisema.”

WIZARA  NISHATI  YAWAKABIDHI WAHANDISI  ZAWADI
Wizara ya nishati na madini imewazadia mafundi wa TANESCO jumla ya shilingi za kitanzania milioni 48.8 kutokana na kufanya kazi usiku na mchana kurejesha umeme katika kituo cha kupooza umeme cha Ubungo  Msongo wa  kilovoti 33.
Kituo hicho kilipata ajali ya kuungua moto Januari 11, 2014 na kuathiri upatikanaji wa umeme katika maeneo ya Magomeni, Ubungo, Ilala na maeneo ya chuo Kikuu.
Akikabidhi zawadi hiyo kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini Naibu Kamishina  Bw. Innocent  Luhoga alitoa sifa kwa wahandisi wa TANESCO kwa kufanya kazi kwa kujituma, akitolea mfano miundo mbinu inavyoathirika kipindi cha mvua,  waandisi hujitahidi kurejesha huduma kwa wakati.
Pia alitoa salamu kutoka kwa katibu mkuu wa wizara “katibu mkuu wa nishati na madini anawashukuru wafanyakazi kwa yote” Wizara inatambua mnavyo fanya kazi katika mazingira magumu licha ya wakati mwingine watu kuwasema vibaya ama magazeti  kuwaandika vibaya alisema.
Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia.