January 29, 2018

Mhe. Mgalu akagua Miradi ya REA Mkoani Kilimanjaro


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Subira Mgalu amekagua utekelezaji wa Miradi ya Umeme Vijijini Awamu ya Pili na Tatu (REA PHASE II & III) Mkoani Kilimanjaro wenye jumla ya Vijiji 18 katika Wilaya za Rombo, Mwanga na Same.

Aidha, Mhe. Mgalu alitumia ziara hiyo kuwatambulisha Wakandarasi kwa Wananchi na kuwataka kutokurudia makosa yaliyojitokeza awali na kuhakikisha wanakamilisha kazi ndani ya muda uliopangwa.

Pia alitembelea Bwawa la kuzalisha umeme la Nyumba ya Mungu kujioneo shughuli za uzalisha.

Mhe. Mgalu alikamilisha ziara hiyo Mkoani Kilimanjaro Januari 26, 2018.







 





January 25, 2018

TANESCO yaboresha Huduma kupitia Mfumo mpya wa GIS


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kuboresha huduma zake kwa Wateja kwa kubuni na kuanzisha mfumo mpya wa kiteknolojia utakaokusanya na kujumuisha taarifa zotemuhimu za miundombinu ya umeme na Wateja kupitia mfumo wa GIS (Geographical Information System).

Mfumo huu unaambatana na ramani ya miundombinu ya umeme na makazi ya Wateja, ambao kwa kiasi kikubwa utasaidia Wataalamu na kutoa huduma kwa muda mfupi na kwa haraka zaidi.


Dkt. Mwinuka afanya kikao na Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Morogoro


Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka amefanya kikao na Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Morogoro ikiwa ni pamoja na kuwatakia heri ya mwaka mpya  wa 2018.

Ikiwa ni kikao chake cha kwanza kukutana na Wafanyakazi tangu kuteuliwa kwake.

Dkt. Mwinuka alisema kukutana kati ya Uongozi na Wafanyakazi kunapunguza "Gape" na kuondoa malalamiko.

Alitumia nafasi hiyo kuwapongeza Wafanyakazi wa TANESCO kwa kufanya kazi nzuri mwaka uliopita wa 2017 kwani kwa kiasi kikubwa malalamiko ya Wateja kwa Mkoa huo yalipungua na pia Mkoa wa Morogoroulitekeleza vizuri Operesheni ya KA - TA. 

Akizungumzia hali ya kifedha ndani ya Shirika aliwataka Wafanyakazi kushiriki kila mmoja kuboresha kwa nafasi yake, kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kwa upaande wa vifaa vitoke stoo kwa mahesabu mazuri.

"Sehemu kubwa ya Wafanyakazi wa TANESCO ni waaminifu na wachapa kazi, lakini hao wachache  wanaohujumu waache ili Wafanyakazi wote tuwe waaminifu". Alisema Dkt. Mwinuka.

Aliwataka Wafanyakazi kuongeza nguvu zaidi ili kufikia malengo.

Wafanyakazi walitoa maoni na kuuliza maswali mbalimbali ambayo Uongozi uliyatolea ufafanuzi, na yaliyo yalihitaji utekelezaji uliyapokea.










January 23, 2018

Dkt. Kalemani akagua maendeleo ya maandalizi ujenzi Mradi wa Stiegler's Gorge



Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amefanya ziara ya kikazi kukagua maendeleo  ya maandalizi ujenzi wa Mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge ikiwemo  njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 33 kutoka Msamvu  hadi mto Rufiji.

 Njia hiyo ya umeme inajengwa na Kampuni Tanzu ya TANESCO  ETDCO.

Lengo la ziara hiyo ni kukagua maendeleo ya maandalizi ya ujenzi wa Mradi wa Stiegler's Gorge unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mapema mwezi Februari mwaka huu baada ya Mkandarasi kupatikana.

Dkt. Kalemani alisema katika utekelezaji wa Mradi huo Vijiji viwili vitanufaika kwa kuunganishiwa umeme kwa bei ile ile ya umeme Vijijini (REA).

"Moja ya matayarisho ya utekelezaji ni ujenzi wa njia ya umeme utakaowawezesha Wakandarasi kupata umeme wakati wa ujenzi".  Alisema Dkt. Kalemani.

Aliongeza katika utekelezaji Wizara tatu zinashirikiana ambazo ni Wizara ya Nishati, Wizara ya Miundombinu na Wizara ya Maliasili na Utalii.

Mradi huo unaotarajiwa kuchukua miaka miwili hadi mitatu mpaka kukamilika kwake baada ya Mkandarasi kuwa ameanza kazi.


Aidha, Mradi unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia miamoja.

Akiongelea hali ya upatikanaji wa umeme nchini Dkt. Kalemani alisema hivi sasa imeimarika tofauti na mwezi Novemba ambapo kulikuwa na ukkarabati mkubwa wa mitambo katika Vituo vya kuzalisha umeme.

Aliwataka Wananchi kusaidia kutoa taarifa panapotokea hitilafu ili ziweze kurekebishwa kwa haraka.

"Tutaendelea kukarabati miundombinu ya umeme ili kuimarisha hali ya upatikanaji umeme".Alisisitiza Mhe. Waziri. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Kebwe Stephen Kebwe aliomba kwa Mhe. Waziri Wizara ya Maji ishirikishwe pia katika Mradi huo kusaidia vijiji unaopiti

 










January 10, 2018

TANESCO yawashukuru Wateja kwa mchango mkubwa mwaka 2017


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji TANESCO Dkt. Tito E. Mwinuka amewashukuru Wateja, wanahabari na wadau wote kutokana na mchango mkubwa kwa Shirika ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ambazo zimeisaidia TANESCO katika kuboresha huduma zake.

Aidha, amesema hali ya uzalishaji umeme unaendelea vizuri kutokana na kuanza kufanya kazi kwa mashine mbili kutoka kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi II, kukamilika kwa ukarabati wa mashine ya kufua umeme Kidatu, na kuongezeka kwa kina cha maji kwenye bwawa la Mtera, kuimarika huku kumepelekea TANESCO kuwa na umeme wa ziada.

Akizungumzia njia za kusafirisha umeme, alisema ukarabati wa miundombinu unaendelea katika njia za kusafirisha umeme.

“Suala la kukatika kwa umeme Kigamboni, ufumbuzi wake utapatikana baada ya kukamilika kwa mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 132 ambapo njia hiyo imefika kituo kipya cha Mbagala”. Alisema Dkt. Mwinuka.

Aliongeza hivi sasa Kigamboni inatumia umeme kutoka njia ya umeme ya kilovolti 32 ya Kipawa – Chang’ombe ambayo pia inatumiwa na Viwanda.

Alisema, licha ya mvua kuwa na changamoto ya uharibifu wa miundombinu ya umeme lakini inafaida kwa TANESCO katika mabwawa kwani inachangia asilimia 41.5.

January 7, 2018

Waziri Mkuu: “Umeme ni fedha, Kuwepo kwa Umeme ni Ajira tosha”





Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Ruvuma ameweka jiwe la msingi la mradi wa njia ya kusafirisha umeme ya msongo wa kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea pamoja na ujenzi wa jengo la Ofisi ya TANESCO Mkoani Ruvuma.
Mheshimiwa Majaliwa amesema lengo la ziara hiyo ni kuwatayarisha Wananchi juu ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali huku akieleza msimamo wa Serikali ni maslahi ya nchi kwanza.

Aliongeza, mkakati wa Serikali ya Awamu ya Tano katika Sekta ya Nishati, ni kuona mtandao wa umeme unaenea pote nchini,  na katika Vijiji ambavyo ni vigumu kufikika kwa miundombinu ya umeme Vijiji hivyo vitatumia umeme wa jua (Solar System).
Ameipongeza Bodi ya Wakurugenzi TANESCO kupitia kwa Mwenyekiti wake Dkt. Alexander Kyaruzi, Menejimenti ya TANESCO pamoja na Wafanyakazi kwa kuunga mkono katika utekelezaji wa Sera za Serikali. 

“Nimpongeze Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO Dkt. Alexander Kyaruzi kwa namna Bodi inavyosimamia, hongera sana wana TANESCO kwa kuunga mkono jitihada za Serikali”. Alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha, alisema amefarijika sana kwa kuhakikishiwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Makambako hadi Songea kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti na jingo la Ofisi mwezi Machi mwaka huu.

Aliongeza kufika kwa umeme wa gridi kutafungua fursa za kibiashara kwa Wananchi wa maeneo hayo hivyo kutokuwepo malalamiko ya ukosefu wa ajira kwa watu kujiari, “Ndugu zangu Umeme ni fedha, Kuwepo kwa Umeme ni Ajira tosha, hivyo tuwekeze katika biashara ndogo ndogo za kutuingizia kipato”.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema katika kipindi cha Miaka miwili ya  Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kumekuwa na mafanikio katika sekta ya nishati nchini ambapo katika njia za kusafirisha umeme mkubwa zimejengwa mbili ambazo ni mradi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga na mmradi wa njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Makambako Mkoani Njombe  hadi Songea Mkoani Ruvuma wenye urefu wa kilometa 250.

Aliongeza kukamilika kwa njia ya kusafirisha umeme ya Makambako hadi Songea kutaipunguzia TANESCO gharama kwa kuacha kutumia mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia mafuta katika vituo vya Songea, Mbinga Namtumbo na Madaba .







January 4, 2018

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WATEJA WALIOHAMISHWA KUTOKA MITA ZA ZAMANI KWENDA LUKU WAKIWA NA MADENI



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tunawataarifu Wateja wetu wenye madeni, ambao walihamishwa kutoka mita za zamani (Conversional Metter) kwenda mita za LUKU kuwa,
Hapo awali walipokuwa wakifanya manunuzi ya umeme, nusu ya fedha ilikatwa kulipa deni la umeme, TANESCO sasa imebadilisha, na  kuweka mfumo mfumo ambao utawezesha madeni hayo kumalizika ndani ya miaka miwili (2).

Kwa wale ambao madeni yalitokana na wizi wa umeme yanatakiwa yakamilike ndani ya miezi sita (6).

Kwa mawasiliano toa taarifa kupitia,
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100
  
Tovuti: www.tanesco.co.tz, mitandao ya kijamii: Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,


IMETOLEWA NA: OFISI YA UHUSIANO
                                 TANESCO MAKAO MAKUU
                                  JANUARI 04, 2018