June 28, 2013

TANGAZO

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI TANGAZO

 Mkurugenzi wa TANESCO anawatangazia ndugu na jamaa wa Marehemu waliozikwa kwenye Makaburi yaliyopo ndani ya eneo la mradi wa upanuzi wa njia za umeme Kata ya Manzese, Mtaa wa Midizini na Kata ya Ubungo Mtaa wa Ubungo Kisiwani kwamba anakusudia kuhamisha Makaburi hayo 250 ili shughuli ya upanuzi wa njia ya umeme iweze kuanza.

 Kwa mujibu wa Sheria za mitaa (Mamlaka za Miji) ya mwaka 1982, kanuni ya mwaka 2008 namba 46(c) Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni itasimamia zoezi hili kwa kutumia wataalam wake.

Taarifa inatolewa kuwa watu wote wenye ndugu au jamaa waliozikwa kwenye eneo hilo wafike Ofisi za Afisa Mtendaji wa Kata za Manzese na Ubungo kujiandikisha wakiwa na barua ya utambulisho kutoka Ofisi ya Mtaa anaoishi kabla ya tarehe 25/07/2013.

 Makaburi hayo yatahamishiwa kwenye Makaburi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yaliyoko Tegeta Kata ya Kunduchi baada ya taratibu zote kukamilika.

                                                              (Imesainiwa na)
                                                     Eng. Mussa Natty Mkurugenzi wa Manispaa
                                                   HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI

June 20, 2013

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AKIZUNGUMZA NA UONGOZI WA KAMPUNI ZA UMEME MAREKANI.

Waziri wa nishati na madini Mh.Prof.Sospeter Muhongo akizungumza na uongozi wa kampuni za umeme za marekani za symbion na General Electric (GE) katika ukumbi wa wizara hiyo juu ya ujenzi wa mtambo wa kuzalisha umeme wa MW 400 mkoani Mtwara.

June 19, 2013

TAHADHARI WIZI WA MIUNDOMBINU YA SHIRIKA


SHIRIKA LA UMEME TANZANIA- TANESCO

TAHADHARI WIZI WA MIUNDOMBINU YA SHIRIKA

Kwa masikitiko makubwa, Shirika la Umeme Tanzania - TANESCO linasikitishwa na vitendo vinavyoendelea vya kuhujumu miundombinu ya Shirika ikiwepo kuibiwa nyaya za umeme huko Arusha mwezi mmoja uliopita, kuibiwa kwa vyuma vya nguzo huko Morogoro na siku ya Jumapili Juni 16, 2013 kuibiwa mafuta pamoja na winding za transfoma iliyopo Mbezi Kibamba kwa Tendwa jijini Dar es Salaam. Wizi huu unatokea wakati Shirika linajitahidi kuboresha huduma zake kote nchini.

 Kutokana na wizi huo, wateja zaidi ya 150 waliathirika kwa kukosa umeme tangu Jumapili hadi jana jioni Juni 17, 2013 ambapo Shirika ilibidi litafute na kufunga Transfoma nyingine ambayo ilikuwa imepangwa itumike kusambaza umeme kwa wateja wengine ambao hawajawahi kupata huduma ya umeme kabisa.

Uongozi wa Shirika unasikitika kwa vitendo hivi na unawaomba wananchi wote kutoa taarifa Polisi au Ofisi zozote za TANESCO zilizopo karibu nao wanapoona watu wanaowatilia shaka kutaka au kuhujumu miundombinu ya Shirika.

Au wasiliana nasi, Kituo cha Miito simu namba 2194400 au 0786985100 

 "Tuilinde Miundombinu ya TANESCO kwa maendeleo yetu na Taifa kwa ujumla"


 Imetolewa na:

                          OFISI YA UHUSIANO,
                          TANESCO - MAKAO MAKUU.

June 13, 2013

TAARIFA KUHUSU KATIZO LA UMEME MKOA WA TANGA

 TAARIFA KUHUSU KATIZO LA UMEME MKOA WA TANGA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Tanga linasikitika kuwataarifu wateja wake wa wilayani za Korogwe, Handeni, Lushoto na Muheza kwamba kutakuwa na makatizo ya umeme siku ya Jumamosi Juni 15, 2013 na Jumapili Juni 16,2013 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni. Sababu ni kufanya matengenezo muhimu katika laini zinazoingia na kutoka katika Kituo kipya cha sambaza umeme cha Songa. Maeneo yatakayoathirika ni: Wilaya yote ya Korogwe isipokuwa maeneo ya Hale, Segera, Michungwani, Kabuku, Mkata, Kwachaga hadi Manga. Wilaya yote ya Handeni, Wilaya yote ya Lushoto na, Wilaya yote ya Muheza Tafadhali usiguse waya ulidondoka au uliokatika, toa taarifa Ofisi yoyote ya TANESCO iliyokaribu nawe. Uongozi wa Shirika unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


 Imetolewa na:

                          OFISI YA UHUSIANO,
                           TANESCO MAKAO MAKUU

June 7, 2013

KATIZO LA UMEME MKOA WA PWANI

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA


 TAARIFA YA KATIZO LA UMEME – MKOA WA PWANI

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linasikitika kuwataarifu wateja wake wa Mkoa wa Pwani kuwa kutakuwa na katizo la umeme Siku ya Jumamosi, 08 Juni, 2013 kuanzia Saa 03:00 Asubuhi hadi 10:00 jioni.  SABABU ni Kufanya matengenezo, kubadilisha nguzo zilizooza katika Line ya Msongo  wa 33KV

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Mlandizi, Kongowe, Visiga, Kwa Mathias, Kwa Mfipa, Picha ya Ndege, Maili Moja, Miembe Saba, Kiluvya, Soga na maeneo yanayozunguka.

Tafadhali usiguse waya wowote uliokatika. Mwananchi usikate mti unaogusa au kukaribia line toa taarifa TANESCO kupitia namba No. 0232402850, 0655989935; 0688359998 au Call Centre No. 2194400 OR 0786985100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza
    

Imetolewa na:          OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.


TAARIFA YA KATIZO LA UMEME – MKOA WA DODOMA


                                                                SHIRIKA LA UMEME TANZANIA


  TAARIFA YA KATIZO LA UMEME – MKOA WA DODOMA

Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwaarifu wateja wake wa Mkoa wa Dodoma  kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo:-

TAREHE:          16/06/2013; Jumapili 
                    
SAA:                3:00 Asubuhi - 12:00 Jioni

SABABU:          KUWEZESHA KUUNGANISHWA KWA CIRCUIT BREAKER MPYA KATIKA KITUO CHA KUPOOZEA UMEME CHA MSONGO UMEME WA 220/33KV CHA ZUZU NA KUUNGANISHA KITUO KIPYA CHA MSONGO UMEME WA 33/11KV,10MWA CHA MZAKWE

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
VISIMA VYA MAJI VYA MZAKWE, VYEYULA, MAKUTOPOLA JKT, MSALATO, MIPANGO, MIYUJI, MAILIMBILI, CHANG’OMBE, CHINANGALI, CHAMWINO, AREA A, AREA C, AIRPORT, UHINDINI

HOSPITALI YA MKOA, JAMATINI, UZUNGUNI, MLIMA WA IMAGI, MAKULU, KILIMANI, GEREZA LA ISANGA, HOSPITALI YA MILEMBE, NZUGUNI

CBE, MAKOLE, VETA, OFISI ZA BUNGE, CHADULU, SWASWA, AREA D, MARTIN LUTHER, IPAGALA
UDOM, KISASA, HOMBOLO, IHUMWA, MAENEO YOTE YA WILAYA ZA BAHI, CHAMWINO, KONGWA, MPWAPWA, NA GAIRO na maeneo yote yanayozunguka.
 

Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:  026 2321728, 0732961270,
 au Call centre namba 2194400  au 0768 985 100

Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza


Imetolewa na:   Ofisi ya Mawasiliano,
                        TANESCO – Makao Makuu.

June 5, 2013

TAARIFA YA KATIZO LA UMEME – MKOA WA KINONDONI KASKAZINI
na Shirika la Umeme Tanzania TANESCO linasikitika kuwataarifu Wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa kutakuwa katizo la umeme kama ifuatavyo:-

TAREHE:       06/06/2013 (Alhamisi)   
                    
SAA:               3:00 Asubuhi hadi saa 11:00 Jioni.

SABABU:       Matengenezo katika laini ya msongo mkubwa, Kubadilisha nguzo zilizooza na
kukata Miti.

MAENEO YATAKAYOATHIRIKA:
Tegeta CCM, Chanika, Njia panda ya wazo factory, Tegeta Masaiti, Tegeta Namanga, Boko Basihaya, Boko CCM, Boko Maliasili, Boko National Housing, Ndege beach, Mbweni Kijijini, nyumba 151 za Serikali/Mh.Magufuli, Bakili Muluzi school, kwa Kala mweusi, Mbweni Mpiji, Kota za Wazo, Dogodogo centre, uwanja wa Nyuki, Ofisi ya Raisi flats, Marando street Bunju, Presidents Office Mbweni, Mbweni Kijijini, and Mabwepande na baadhi ya maeneo ya Bagamoyo.

Tafadhali kuwa makini na nyaya za umeme zilizo chini. Ukiwa na wasiwasi piga simu Usishike waya wa umeme  TANESCO Tegeta: 0717 650878, 0688 650878 au  Kinondoni Kaskazini: 022 2700367, 0784 768584, na  0716 768584 Au namba za huduma kwa wateja  022-2194400  au  0768 985 100.
          
Uongozi unasikitika kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.


Imetolewa na:            OFISI YA UHUSIANO,
                                    TANESCO – MAKAO MAKUU.