October 22, 2016

TANESCO YAJENGA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME KUPITIA ARDHINI KATIKATI YA JIJI LA DAR ES SALAAM,


 Kaimu Meneja Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Umeme Jijini Dar es Salaam, Mhandisi Iddi Rashidi, akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme ardhini, (Underground Transmission Lines), unaopitia Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam, Oktoba 22, 2016.


SHIRIKA la Umeme Nchini (TANESCO), limekamilisha Ujenzi wa  Mfumo wa Njia ya Usafirishaji Umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) ,  kutoka shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani jijini Dar es Salaam na kutoka kituo cha umeme cha Makumbusho kwenda kituo kipya cha kupozea umeme kilichoko katikati ya jiji cha City Centre cha ukubwa wa 100MVA (2X50MVA), 132/33KV.
Akizungumzia maendeleo ya Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Umeme Jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Mradi huo, Mhandisi Iddi Rashidi, alisema, kukamilika kwa ujenzi wa  mfumo huo ambao utahusisha ujenzi wa mfumo wa njia za usambazaji umeme chini ya ardhi (Underground Distribution Lines), wa kilomita 4.3 ya msongo wa kilovolti 33 kwa ajili ya kuunganisha kituo cha City Centre na vituo vingine vitatu vya Kariakoo, Railway na Sokoine.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Rashidi alisema, ujenzi wa mfumo wa njia ya usafirishaji umeme chini ya ardhi (Underground Transmision Lines),  kwa msongo wa Kv132 kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre tayari umekamilika na ule wa kutoka Shule ya Sekondari ya wasichana Jangwani kwenye City Centre pia umekamilika.
“Faida kubwa ambayo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam watarajie ni kupata umeme wa uhakika (reliable power supply ulio kwenye viwango stahiki, (Acceptable quality power supply) hususan kwa wale wa maeneo ya katikati ya jiji,” Aliongeza Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali.
Akieleza zaidi, Mhandisi Nangali alisema, “Mradi huu unaviwezesha vituo tajwa kuwa na njia mbili za kuvipatia umeme na hivyo kuwezesha kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia moja kati ya hizo itakuwa na hitilafu.” Alifafanua.
Alisema kuongezeka kwa kituo cha City Centre cha 100MVA, kunafanya jiji la Dar es Salaam pekee kuwa na jumla ya vituo 9 vya aina hiyo.
“Hivi sasa tunaweza kusema, ujenzi umekamilika kwa zaidi ya asilimia 98, kinachoendelea ni kukamilisha ujenzi wa mfumo wa njia ya kusafirisha umeme kupitia juu (Overhead Transmission Lines), wa kilomita 1.3 wa msongo wa kilovolti 132 kutoka kituo kikubwa cha kupozea umeme cha Ilala hadi shule ya sekondari ya wasichana Jangwani ambapo utaungana na mfumo wa usafirishaji umeme chini ya ardhi, (Underground Transmission Lines) kwenda kituo kikubwa cha City Centre.” Alifafanua.
kutoka Makumbusho kwenda kituo cha City Centre, umekamilikakatikati yan jiji utekelezaji wa Mradi huo, unaofadhiliwa kwa pamoja na Serikali ya Tanzania na Finland, unahusisha ujenzi wa kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji umeme (Distribution SCADA System), katika msongo wa kilovolti 33 na 11.
“Tayari ujenzi wa kituo cha City Centre umekamilika kwa asilimia 100 na sasa tuko katika hatua za majaribio.” Alisema Mhandisi Rashidi.
Naye Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, amewaomba wakazi wa jiji kuwa wavumilivu wakati zoezi hili la kuboresha miundombinu likiendelea kwani huwa panatokea kukatika kwa umeme sehemu Fulani Fulani ili kutoa nafasi kwa mafundi kufanya kazi kwa usalama zaidi.




 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala, Mhandisi Athanasius Nangali, (kulia), akiwa na Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashidi wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu mradi huo
 Meneja wa TANESCO Mkoa wa Ilala,  Mhandisi Athanasius Nangali, (katikati), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Iddi Rashid, (kulia), Afisa Habari na Mawasiliano wa TANESCO, Henry Kilasila, wakitembelea eneo la ujenzi wa Mfumo huo shule ya sekondari Jangwani jijini Dar es Salaam
 Hizi ndio njia za kusafirisha umeme ardhini zilizojengwa kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani jijini Dar es Salaam
 Nguzo ya kusafirisha umeme wa juu kutoka Kituo cha Ilala kuelekea Shule ya Sekondari ya Wasichana Jangwani, ambapo zitaungana na Mfuko wa njia ya kusafirisha umeme ardhini kupelekea katikati ya Jiji

 Mafundi wakiwa kazini


 Mhandisi  Nangali, (mbele), Kaimu Meneja Mradi, Mhandisi Rashid, (kulia), wakiangalia moja ya roller lenye nyaya.

October 7, 2016

TANESCO, yasaini mkataba wa ujenzi 400kV utakao unganisha nchi za Kenya na Tanzania

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), akibadilishana hati za mkabata na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa Kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton baada ya kusaini, mradi wa ujenzi wa njia ya umeme (transmission line) itakayounganisha Tanzania na Kenya, Makao Makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, Oktoba 7, 2016. TANESCO imeingia mkataba na Makampuni matatu kutekeleza mradi huo (KTPIP), wa Msongo wa KV400 unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB) na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya dola za Kimarekani
309.26


NA HENRY KILASILA/Dar

SHIRIKA la Umeme Nchini Tanzania, (TANESCO), limesaini mkataba na Makampuni matatu kujenga njia ya umeme, (Transmission lines), ya Msongo wa Kilovolti 400 njia hii ya umeme itaziunganisha Nchi za Tanzania na
 Kenya.
Hafla ya kutiliana saini mikataba hiyo, imefanyika Oktoba 7, 2016 Makao Makuu ya TANESCO Jijini Dar es Salaam, ambapo TANESCO imetiliana saini mikataba hiyo na makampuni ya Bouygues Energies Service, Energoinvest na Kalpa-Taru.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Felchesmi Mramba alisema, Ujenzi wa Mradi huu wenye urefu wa Kilomita 414, utaanzia Mkoani Singida,-Babati-Arusha hadi Namanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.
Kisha Mradi utaunganishwa na njia ya Msongo wa Kilovolti 400 yenye urefu wa kilomita 96 kutoka eneo la Isinya, Nairobi, nchini Kenya hadi eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya, (Namanga) ambapo utaunganisha na njia ya umeme wa wa Msongo wa Kilovolti 400kv kwa upande wa Tanzania.
“ Napenda niwahakikishie kuwa, huu ni mfululizo wa miradi mikubwa inayotekelezwa na Serikali kupitia TANESCO na utawezesha usafirishaji wa umeme wa Megawati 2000 katika pande zote kenya na Tanzania”. Alifafanua Mhandisi Mramba.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Mramba alsiema, utekelezaji wa mradi huu unaofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, (AfDB), na Shirika la Misaada ya Maendeleo la Japan, (JICA), kwa gharama ya Dola za Kimarekani, Milioni 309.26 utakamilika katika kipindi cha miezi 24, sawa na miaka 2.
“Dola za Marekani Milioni 258.82, zitatumika kujenga upande wa Tanzania na  Dola za Kimarekani Milioni 50.45 zitatumika kujenga mradi upande wa Kenya,” alifafanua Mhandisi Mramba.

Aidha Mhandisi Mramba aliwataka wakandarasi waliopewa kazi hiyo kuitekeleza kwa wakati kwa mujibu wa mkataba.
“ Angalizo, kwenu ninyi wakandarasi, kamilishini mradi ndani ya muda kama ambavyo tumekubaliana kwenye mkataba, kushindwa kukamilisha ujenzi kwa mujibu wa mkataba ni kushindwa kufanya kazi na sisi, TANESCO hatutakubaliana na hilo.” Alionya Mhandisi Mramba.
Naye mwakilishi Mkazi wa (AfDB), Tonia Kandiero, alitoa hakikisho kuwa Benki hiyo itaendelea kusaidia miradi mikubwa kama hii, kwa manufaa ya eneo lote la Afrika.
Kwa upande wake, Afisa Miradi msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, aliungana na AfDB, kutoa hakikisho la ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na JICA, katika kusaidia kutekeleza miradi ya maendeleo kama huu uliosainiwa.



 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara ya Kimataifa wa kampuni ya Bouygues Energies&Service, Patrick Canton wakisaini mkataba huo
 Mhandisi Mramba, (kushoto), na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, wakisaini mkataba
 Mhandisi Mramba, akibadilishana hati na S.K. Sarotra, Makamu wa Rais msaidizi wa Kampuni ya KALPA-TARU, baada ya kusaini mkataba.
 Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakisaini mkataba kutekeleza mradi huo
 Mhandisi Mramba, (kushoto), na Mkurugenzi wa Kampuni ya Energoinvest, Bisera Hadzialjevic, wakibadilishana hati
 Mkurugenzi Mkazi wa AfDB nchini, Tonia Kandiero, akizungumza kwenye hafla hiyo
 Mhandisi Mramba, (kulia) na Kandiero, wakifurahia jambo wakati wa hafla hiyo
 Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bibi. Kandiero
 Afisa Mipango Msaidizi wa JICA, Apolei Rosina, (kushoto), akizungumza
Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, (kushoto), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Bi. Rosina wa JICA
 Mhandisi Mkuu wa Nishati, wa Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Salum Inegeja, akizungumza kwenye hafla hiyo
 Mratibu wa Miradi wa Shirika la Umeme nchini Tanzania, (TANESCO), Mhandisi Khalid James, (kulia), akizungumza wakati wa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Felchesmi Mramba.
 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Mramba, (wasaba kushoto), akipongezwa na Mwakilishi mkazi wa AfDB, hapa nchini, Tonia Kandiero, wakati wa picha ya pamoja na wawakilishi wa makampuni yaliyopata kandarasi ya ujenzi wa mradi huo
 Kutoka kushoto, Patrick Canton, S.K. Sarotra, Apolei Rosina, Mhandisi Mramba, Tonia Kandiero na Bisera Hadzialjevic, wakiwa katika picha ya pamoja mwishoni mwa hafla hiyo
 Afisa Mawasiliano na Uhusiano wa TANESCO, Henry Kilasila, (kualia), akizungumza mwanzoni mwa hafla hiyo. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Felchesmi Mramba.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, (Uwekezaji), Mhandisi Decklan P.Mhaiki, akiwakaribisha wageni kwenye hafla hiyo.
Meneja mradi huo wa KTPIP, Mhandisi Mhandisi Lewanga Tesha, (kulia), akiwa na wawakilishi wa kampuni ya KALPA-TARU