Hii ni mita iliyotumika ambayo haikusajiliwa na TANESCO.. |
Maafisa
wa Polisi kutoka Kituo cha Kati wakishirikiana na Maafisa Usalama wa Tanesco
mkoa wa Temeke, wamefanikiwa kuzibaini nyumba mbili zilizounganishiwa umeme
kinyemela na kujenga nguzo tisa kwa kutumia vishoka katika la Vigozi lililoko
Mbagala jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa maafisa wa Polisi waliofanikisha zoezi hilo Afande Sospeter Antony, wa Kituo
cha Kati, aliwata wamiliki wa nyumba hizo kuwa ni Mr. Ibrahim Mohammed Nyingila
pamoja na Bw. Said Rajab anayefanya kazi Mamlaka ya Bandari.
Hujuma
hii dhidi ya Tanesco iligundulika baada ya raia wema kutoa taarifa za kitendo
hicho kwa kikosi kazi cha kupambana na hujuma za namna hii, kilicho chini ya
Afande Sospeter na Maafisa Usalama wa Tanesco.
Baada
ya kuhojiwa na maafisa wa usalama, wamiliki wa nyumba hizo kwa nyakati tofauti
walikiri kujipatia huduma ya umeme kinyume na utaratibu, kwa kulipa zaidi ya milioni
kumi kama malipo ya ujenzi wa nguzo tisa kwa Vishoka, ambao hata hivyo majina
yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.
Walipotakiwa
kuelezea ni namna gani nguzo hizo zilifika katika eneo hilo, wamiliki hao
walisema zililetwa na gari la Tanesco
ambalo hata hivyo hawakufanikiwa kushika namba zake za usajili.
Katika
utafiti uliofanywa na maafisa wa Tanesco, waligundua kuwa nguzo zote, nyaya na
mita zilizotumika katika kutekeleza hujuma hiyo ni mali ya Tanesco.
Aidha
nyumba hizo zilikutwa na mita ambazo hazikujasajiriwa, na hivyo kutumia umeme
pasi na kuulipia.
Baada
Maafisa Usalama kuchukua vielelezo, mafundi wa TANESCO walizichomoa nyaya zote kutoka
kwenye nguzo, na taratibu za kisheria zinaendelea.
Kulia ni nguzo waliyochukulia umeme na kushoto ni nguzo ya kwanza katika tisa zilizojenga na vishoka |
Hii ndiyo nguzo ya kwanza kati ya
tisa iliyowekwa pasi utaratibu wa TANESCO na vishoka |
No comments:
Post a Comment